Waraka no 4 wa CCM: Chakula cha njaa kilitupa ushindi Igunga

Kakwambia nani kuwa mleta hoja ni kiongozi tena wa cdm? Mbona umepata mchecheto kuna nini hapo? Hivi hujui wamiliki wa Mtanzania ni kati ya waliopiga debe Igunga, mbona hukuwaambia walete mambo ya msingi (kama hili sio la msingi) waachane na ccm?

Sasa kwa taarifa yako habari hii ni muhimu sana kwa mustakabali wa nchi yetu hasa kuelekea 2015, na ili uamini kuwa ni kati ya habari muhimu hata ccm wameijadili kwenye vikao vyao vya chama na ndio chanzo cha kutufikia sisi, acha woga siasa siku zote ni kosa la mwenzako faida kwako na agenda kwa wananchi kama ccm inavyoshupalia swala la udini kwa cdm japo halina mashiko


Mikael P Aweda - 0784 583 330
Mjumbe Baraza kuu Taifa - Chadema
 
Hoja hapo ni kwamba serikali ilitumia resources zake kukisaidia chama tawala kishinde. Huo waraka ni ushahidi tosha mahakamani kwamba wenye chama walikiri kuwa mahindi ya msaada yalipelekwa Igunga ili kuwahadaa wananchi wawape kura.

Swali ni kwamba je kusingekuwa na uchaguzi hayo mahindi ya msaada yangepelekwa?
 
Nawapa pole sana wanaigunga CCM inawadhririsha,Watu wa Igunga badilikeni jamani ona CCM inavyowadharau,eti mkipewa chakula tu mnawapa kura BADILIKA IGUNGA.

Katika uchaguzi wa Igunga chakula cha njaa sio kigezo cha Ushindi kwa CCM, CCM igunga hawakushinda isipokuwa wamebaka matokeo na kujinyakulia jimbo bila ridhaa ya wananchi wa Igunga. ukitaka kuhakikisha njoo uulize angalau watu 10 tu kwa uchache utapata majibu na kwa mtazamo wangu kwa nini hadi leo hawajafika Igunga na kutoa shukrani kwa wanachi kama kweli walichaguliwa na wananchi wa Igunga?
 
Back
Top Bottom