BUGALIBOBADIMI
Member
- Sep 27, 2012
- 15
- 6
huyu MWIGULU ni kati ya watu watakaosababisha maafa makubwa hapa nchini,mbaya zaidi chama chake wanafikiri anawasaidia.
cdm kuweni na agenda moja sio kila kukicha huyu yupo mpanda, huyu karagwe kwa wakwe zake, mwingine tunduma duu hiki chama...haya sie tushapanga mambo yetu kwenye mabaraz ya katiba na tunaenda vizuri mkija kushtuka mchakato umeisha...tusilaumiane badaye na tukibadilisha katiba ss hv hadi miaka 300 ipite
Salaams,
Kila kukicha ni wewe na kila uchao unavuma kwa mambo ambayo hayana msingi na wala hayana mwelekeo wa kuiendeleza Iramba Magharibi. Yawezekana umesahau jukumu lako kama mbunge wetu matokeo yake unafanya kazi za CCM na serikali ndani ya Bunge. Kumbuka kuwa wewe haupo bungeni kuiwakilisha serikali, au usalama wa taifa au CCM, upo bungeni kwa niaba ya wana Iramba Magharibi. Mengi unayozungumza bungeni ni yale uliyonayo kichwani mwako na si yale ambayo wana Iramba wamekutuma.
Huna sifa za kuwa mwakilishi wa wana Iramba. Ulipoteuliwa na wana CCM kugombea ubunge wana iramba wengi walidhani wamepata mtu wa kuisogeza Iramba. Niliwaskitikia sana wana Iramba wenzangu kwa kuwa na mtazamo huo. Ni kwa sababu walikuwa hawakujui. Mie niliyepata kukufahamu japo kidogo nilisikitika sana. Nakumbuka ulipokuwa UDSM kipindi kile cha mgomo wa kushinikiza marehem Mkili atolewe magereza, kila uliposimama kutoa hoja watu walikuzomea na kukutaka ukae chini. Si kwa sababu walikuwa wankuchukua, ila kwa sababu hukuwa na uwezo wa kujenga hoja za kushawishi watu. Hilo liko wazi, watanzania walio wengi wanakuzomea kila uzungumzapo bungeni. Sidhani kama hiyo ni sifa nzuri kwa kiongozi mzuri.
Umekuwa ukihusishwa na mambo mengi ya hovyo, wahenga walisema lisemwalo lipo.... Sidhani sana kama unajitambua na unatambua uyafanyayo. Wakati mwingine huwa nafikiri huenda yale maisha yako ya kukaa porini kwa muda mrefu ukichunga ng'ombe yaliathiri ukuaji wako kiakili kiasi kwamba hujitambui, huwezi kujenga hoja zikashawishi watu, ukatumiwa na wenzako kwa kila aina ya jambo lisilojema na wewe ukalibebea bango pasipo tafakuri ya kutosha. Ama kwa hakika umekuwa limbukieni wa kila jambo. Kumbuka cheo ni dhamana, na hukuzaliwa kuwa kiongozi milele. Muda wako utakwisha watakuja wengine nao watapita. Ni vema sasa ukatumia muda huu kufanya mambo ambayo watu watakukumbuka nayo kwa wema.
Ulikuwa mchunga ng'ombe hebu kumbuka kufanya mambo ambayo yatawasaidia wale wachunga ng'
View attachment 93456Mr mchemba that is a nice advice hope you will take it up if only you are wise
Mwl Shukia ati mtaalamu wa lugha sasa sioni ujumbe kwenye thread yake imejaa mipasho tu na uCDM ndani....ati enzi zile pale UDSM wee Shuka nani alikuwa anakujua? Au ulikuwa unajulikana idarani kwako foreign languages? Ati alikufundisha mwenge ni mtaalam wa lugha yani ukishabijia hili liCDM basi uongeacho utamwagiwa sifa.
CDM kila kukicha Mwigulu duu kazi ipo...haya akirudi toka CHINA atawajibu maana hamlali mnamuota Mwigulu. Ndio maana mnajitoa kwenye mambo ya maana km katiba mnafanya siasa uchwara za kuimarisha kanda zenu za kusadikika. Mwigulu hatoki iramba huku CDM hakina hatamwakilishi mmoja hv mtashindaje? Viva Mwigulu
CCM ni kama kipande cha almasi halisi ,lkn CDM ni kama kipande cha chupa hv ambacho tunataka kubadilishiwa tukiamini ndio almasi halisi na tunaenda tunashangilia kama zuzu na kujuwa tumepata mkombozi kumbe tumepoteza, watanzania cyo kama hatutaki mabadiliko lkn cdm kwa jinsi wanavyotaka kutujenga watanzania cyo salama kbs naomba tuwachunguze kwa makini maana baadhi ya kauli zao na jinsi wanavyoendesha siasa zao ni hatari sana, maana huwezi kuwa unahubiri shari kila siku wakati kuna mambo ambayo serikali imekuwa ikiyafanya ni mazuri . Wanasiasa pinganeni lkn heshimianeni maana mwisho wa cku lazima mrudi kwa wananchi kupata ushirikiano ktk kujenga nchi bila nani alikupigia kura na nani
hakukupigia kura.Tunataka Amani tena ni Amri cyo ombi kwa yeyote anayeenda kinyume cha Haya.