Dkt. Mwigulu Nchemba yupo kimya kwa sasa anameza matonge makubwa makubwa!

Lyambalyetu

JF-Expert Member
Apr 6, 2021
265
240
Mjanja sana huyu jamaa!

Baada ya kuingia msituni na kudodosa kidogo nikagundua nyeti mabasi yake ya Esther kwa mwezi yanaingiza faida TU inayokadiriwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 80 - FAIDA tu baada ya kutoa gharama za uendeshaji.

Mwaka 2024 katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuwa hayupo popular kama mwanzo Jimboni kwake Iramba, amepanga kutumia fedha kuwaweka 50% ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kwa kutumia Bajeti anayoitaja yeye (kutoka kwa msiri wake pale Ndago) Shilingi 230,000,000/- hasa kwenye Vijiji vile ambavyo anaona vina utata kiasi, asilimia kubwa vikiwa ni kutoka Tarafa ya Kisiriri.

Inasemekana kwa Mwaka 2025 atatumia zaidi ya Shilingi 500,000,000/- ikijumuisha viongozi mbalimbali wa CCM wa Mkoa na Wilaya ili kuhakikisha anabaki madarakani.

Dkt. Mwigulu ambaye ni mtaalamu sana katika Planning ameendelea kueleza kwa chawa wake kuwa Uchaguzi wowote kipindi cha Mama Samia unatakiwa upambaniwe kwa akili na hadaa kubwa kwa sababu ubabe kama uliotumika kipimdi cha JPM utawekwa pembeni.

Kutokana na mtazamo huo, ndiyo maana kwa sasa ameamua kuwa kimya na kujilimbikizia mihela tu akiamini kwamba mwaka 2025 ni fedha tu ndizo zitakazomkwamua na si kingine!
 
Back
Top Bottom