Waraka maalum kwa Wakristo Zanzibar (?)

Status
Not open for further replies.

Tumsifu Samwel

JF-Expert Member
Jul 30, 2007
1,407
160
Waraka maalum kwa Wakristo Zanzibar

Wapendwa katika Bwana,


NDUGU Wakristo umefika wakati tumeonelea kuwa ipo haja ya kuwaelezeni
machache ili kuona maendeleo yetu na mafanikio tuliokwisha yapata hapa
Zanzibar, yanaendelezwa na hayarudi nyuma kwa namna yoyote. Hapana
shaka kuwa munaelewa kuwa idadi yetu hadi sasa ni ndogo sana na wengi
wetu tungali katika kiwango na hadhi ya wahamiaji na sio Wazanzibar
kama wanavyosema wenyewe.



MAFANIKIO YETU


KABLA kugusia yale ambayo tunahisi ndio lengo la waraka huu hapana
budi kuwatajieni mambo machache ambayo tumefanikiwa kuyapata hadi
sasa. Pamoja na jitihada zetu za muda mrefu bado tunapaswa tumsifu
Bwana kwa msaada wake mkubwa kwetu dhidi ya maadui zetu. Tunaamini
kuwa kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu, Bwana atatupa ushindi na
mafanikio makuu zaidi ya haya na atawafumba macho maadui zetu wazidi
kulala ili mipango yetu yote ya kuibadilisha Zanzibar kidemografia
ifanikiwe katika kipindi kifupi kijacho. Mafanikio yetu yameenea
katika kila upande - katika uchumi, siasa, huduma za jamii, umiliki wa
ardhi, ujenzi, elimu na kadhalika ili kupata picha kamili ni vyema
tuorodheshe kwa ufupi mafanikio hayo:


Nafasi yetu kwa upande wa elimu imekuwa ya kuridhisha kupitia nafasi
za serikali. Hivi sasa ni rahisi na limekua jambo la kawaida katika
kila matangazo ya wito wa masomo kusikia majina ya Wakristo. Kati ya
vijana 7 hadi 10 ni lazima upate vijana wawili hadi watatu kutoka
katika makanisa yetu.


Sambamba na matangazo ya elimu, vijana wetu wamekuwa wanapata nafasi
nyingi za ajira katika serikali ya Zanzibar.


Hali ya kutoelewana
kisiasa baina ya Wazanzibari imetoa mwanya kwetu kuingiza vijana wa
Kikristo wenye asili ya bara kwa wingi kwani wamekuwa wanaaminika
zaidi kuliko vijana wa Zanzibar.


Hali tulioieleza juu imetuwezesha kuwa na Wakristo wengi katika nafasi
za juu serikalini na katika chama tawala. Hali hii ni lazima
iendelezwe katika ngazi zote kwani ndiko kunako mambo mengi ya kila
siku.


Tumepata fursa ya kutumia Taasisi za serikali kwa uendeshaji wa ibada
zetu. Hali hii imefanya tuzidi kukubaliwa na Waislamu na kuvumiliwa na
inaweza kutupa nafsi ya kuwavuta katika NENO LA BWANA.


Kwa upande wa mashamba (vijijini) tumepata wasaa mzuri wa kununua
ardhi toka kwa Waislamu ambao hadi sasa bado hawajashtuka. Ardhi hizi
zimetuwezesha kujenga makanisa kadhaa ambayo hapo awali hayakuwepo.

Idadi ya skuli na vituo vyetu (ambavyo licha ya picha ya juu kuwa
haviendeshwi kwa misingi ya Kikristo lakini kiukweli ni vituo vya
kimisionari) vimeongezeka kwa hali ya kuridhisha. Skuli hizi ni
kuanzia kwa watoto wadogo hadi vituo kama hichi kilichopo mji mkongwe
(Stone Town Youth Centre) na zinafanya kazi vizuri katika kupandikiza
mila za Kikristo.


Sera zilizopo hivi sasa kwa upande wa uingiaji na utokaji Zanzibar
imetusaidia sana katika uingizaji wetu (Wakristo) kutoka Bara na hivyo
kusaidia kufuta ile imani ya kuwa Zanzibar ni kisiwa cha Waislamu eti
Wazanzibari kwa zaidi ya asilimia 99 ni Waislamu.


Ujaji wa Wakristo kwa wingi kutoka Bara umewezesha kuongezeka kwa
idadi ya mabaa na kilabu za pombe. Hivi sasa ni jambo la kawaida kuona
magari ya aina mbalimbali yanayomilikiwa na eti Waislamu yamebeba
kreti za bia na pombe kali.


Kujiingiza kwetu katika taasisi za dola katika ngazi za mitaa
kumetuwezesha kupata nafasi ya kutangaza Ukristo kwa njia ya mihadhara
na wakati huo huo kudhibiti mihadhara ya wazi ya Waislamu kwa kutumia
madai ya kashfa na kutatanisha maelewano mazuri baina ya watu wa dini
tofauti.

Tumefanikiwa kupata viwanja vingi katika maeneo ya mjini ambayo
yangali mapya. Maeneo haya ni kama Tomondo, Mombasa, Mwanakwerekwe na

kadhalika ambayo tayari tumeshajenga makanisa yetu ingawaje kwa sasa
hayajawa na waumini wengi wa kuyatumia na bado yanaonekana ni matupu.

Ndugu wapendwa katika Bwana,

Mafanikio hayo yasitufanye tukalewa na kusahau jukumu la kanisa la
kuona kuwa utawala wa Bwana unashuka Zanzibar haraka iwezekanavyo.
Kosa lolote utakalofanya hivi sasa litaweza kuturudisha hatua kadhaa
na huenda nafasi hii tuliyonayo hivi sasa tusiipate kwa karne mpya
ijayo.


Mambo ya kufanya yanayotukabili ili kuimarisha nafasi yetu ni kuona
yale tuliyokwisha yapata hayatutoki na kuyafanya dira kwa karne ijayo
ni haya yafuatayo:


Tusahau tofauti zetu dhidi ya adui

Ingawaje tupo madhehebu nyingi lakini tunawajibika kuelewa kuwa
Waislamu na Uislamu wao ni adui yetu namba moja ambaye hatutofaulu
kupambana nae mmoja mmoja. Uislamu hapa Zanzibar ni dini iliofungamana
na mila na utamaduni hivyo kila itakavyowezekana tusahau tofauti zetu
ndogo ndogo na hata kubwa kukabiliana nao, vingienvyo tutarudi kama
wakati wa Karume.


Tuhakikishe tunapata ardhi

Hii ni mbinu kongwe katika usambazaji wa Ukristo. Wazee wetu
walipoleta Ukristo Zanzibar na katika Afrika, jitihada waliyofanya ni
kupata ardhi kuwa kwa ajili ya ujenzi wa maeneo yetu, majengo ya
hospitali, shule, zahanati na vituo vya chekechea, makanisa na
kadhalika. Tunahitaji ardhi kubwa ili kuziweka huduma hizo mahala
pamoja kwa ajili ya kueneza injili ya Bwana na Muokozi wetu.


Tununue nyumba na viwanja kwa ujenzi wa Makanisa

Inaonekana Waislamu wenye siasa kali na baadhi ya watendaji kwenye
serikali wameanza kushtuka na ongezeko kubwa la makanisa katika kisiwa
cha Unguja. Kuna dalili kuwa tunaweza kupata ugumu katika kupata
viwanja kwa ajili ya makanisa. Njia tunayoweza kuitumia kwa muda huu
ni kununuwa viwanja vitupu au nyumba za Waislamu kwa bei kubwa
itakayowashawishi kuziuza na baadaye tukaweza kuvijenga au kugeuza
nyumba hizo kuwa makanisa.


Tujenge shule na hospitali kwa wingi

Hizi ni taasisi ambazo tunaweza kueneza neno la Bwana kwa Waislamu
walio wengi hapa Zanzibar. Kwa kutumia umaskini unaowakabili wengi ya
Wazanzibari na uchache wa huduma hizo tunaweza kujitangaza vizuri,
tujitahidi kutoa huduma nzuri kuweka vifaa vya kisasa kuweka bei
ndogo, kuweka upendo ili vituo vya Waislamu au hata vile vya serikali
visiweze kuvikaribia vyetu. Shule ni sehemu muhimu ya kupandikiza
mafundisho yetu zaidi kwa watoto wadogo (Nursery).


Tunadai muda zaidi katika vyombo vya habari (TV na Radio)

Kwa muda mrefu sasa Uislamu na Waislamu wamehodhi vyombo hivi vya
habari mbali na kuwa siku ya Ijumaa ambayo yote humilikiwa na vipindi
vya Kiislamu vyombo hivyo hutenga siku nyingine kadhaa kwa vipindi vya
Kiislamu na hata kuthubutu kutia adhana kila wakati wa sala hali hii
inaudhi na inatoa picha ya wazi ya serikali kupendelea Uislamu
ingawaje inadai kuwa haina dini. Wakati wa kusherehekea miaka 25 ya
TVZ tulizungumzia suala hili lakini halikupata mtu wa kulifanyia kazi.
Sasa tuhakikishe kuwa Ukristo unapata muda zaidi katika vyombo hivyo
au Uislamu nao upunguziwe nafasi.


Tuongeze mhadhara wa wazi

Wakati Waislamu wamezuiliwa kufanya mihadhara ya wazi, sisi tujitahidi
kuhakikisha kuwa mihadhara yetu inaongezeka kwa kiwango kikubwa. Kwa
kuwa Waislamu hawahudhurii mihadhara hiyo, lazima tuone Wakristo wa
mjini na mashamba wanahamasishwa na kupatiwa nyenzo ili kuhudhuria.
Vipaza sauti vitumike kuhakikisha kuwa neno la Bwana linafika kila
pahala. Mihadhara ifanyike karibu na nyumba, Misikiti na kwenye
viwanja vya wazi.


Tuendelee kutumia shule na sehemu za umma

Ili kuwafanya Waislamu watuzoee na kuondosha chuki yao kwetu ni lazima
kuendelea kutumia mashule na sehemu za umma zilizo wazi kwa mambo yetu
ya ibada kwa kipindi kirefu hali hii inaweza kuwafanya washindwe kuona
tofauti yetu na wao.


Tufanye suala la uhamiaji Zanzibar kuwa jepesi

Uzoefu unaonesha kuwa ni jambo gumu kuwabatiza Wazanzibari Waislamu.
Hali hii inafanya ongezeko la Wakristo kuwa dogo au halipo kabisa
ukitoa wale wanaozaliwa katika familia za Kikristo.


Njia pekee ya kuhakikisha ongezeko la makanisa na taasisi zetu ni
kuongezeka kwa Wakristo. Jambo hili litawezekana kwa kuingiza Wakristo
wengi kutoka Tanzania Bara au wapagani ambao tutaweza kuwabatiza kwa
kutumia udugu wetu wa kikabila au asili ya Bara. Kwa kuwatumia ndugu
zetu waliomo serikalini (SMZ au SMT) tuhakikishe kuwa suala la
uhamiaji linabakia wazi na rahisi na linaendelea kwa kila hali.


Tuzuie jaribio lolote la kadi za uraia au vitambulisho

Wakrsito tunapaswa kuelewa kuwa iwapo serikali ya Zanzibar itaamua
kufanya chochote ili, kuwa na vitambulisho au kadi za uraia kwa
Wazanzibari basi jambo hilo litaathiri sana mipango yetu ya muda mrefu
kwa Zanzibar. Jitihada zozote za kuiimarisha Zanzibar kama Zanzibar na
nje ya Utanzania ni lazima tuelewe kuwa Uislamu utapata nguvu na kuwa
tishio kwa hapa Zanzibar na hata Bara. Iwapo tutawajibika kuunga mkono
ni kadi za Uraia na vitambulisho vya Watanzania kwa ujumla na sio
Zanzibar peke yake.


Tujipenyeze na kushika nafasi muhimu

Lazima tuelewe kuwa chama chochote cha siasa kinalenga kukamata
serikali ili kiweze kutekeleza yale yanayoaminika kuwa mazuri kwa
chama hicho. Tunapozungumzia vyama vya siasa kwa Zanzibar tunahusisha
zaidi kwenye CCM na CUF. Watu wetu wamefaulu kuingia kwa wingi katika
chama tawala na katika jumuiya zake.


Tuunge mkono sera za utalii

Hadi sasa wengi wa watalii wanaoingia Zanaibar hutokea nchi za
Kikristo. Desturi za watalii hupingana na zile za Kizanzibari na hata
za Kiislamu. Watalii wanasaidia kuongezeka kwa mabaa na vivazi ambavyo
Waislamu wanataka visivaliwe hasa na wanawake.

Tujenge mabaa na kuongeza pombe

Waislamu wengi huchukia pombe na huweza kuhama iwapo duka la pombe au
baa ipo karibu nao. Waislamu hatari ni wale wanaosoma na kupata muda
wa kujishughulisha na dini yao.

Pombe ni kitu ambacho humtoa Muislamu katika Uislamu wa vitendo na
kumkaribisha na Ukristo.


Uwafuate Wakristo waliosilimu ili warudie Ukristo

Watu wa aina hii wanakuwa bado hawajatulia na mara nyingi huwemo
katika matatizo. Pana haja ya kuwalenga watu hawa ili kuwarudisha
kabla hawajatulia au kupata elimu nzuri. Matatizo yao ndipo mahala pa
kuanzia ili Bwana atawateremshie roho ya utulivu. Uzima wa Ukristo ni
kuwa na wafuasi wengi kadiri iwezekanavyo.


Tuwafuate wanawake kwa misaada

Jumuiya zisizo za kiserikali zinaungwa mkono duniani kote na hasa zile
za wanawake na watoto tujiweke pamoja ili tuweze kuwavutia kwa jina la
kuwasaidia.


Tuongeze vituo vya mafunzo ya Kikristo

Kituo cha vijana cha mji mkongwe (Stone Town Youth Center) kimekuwa
kikifanya kazi yake vizuri kwani hadi sasa lengo lake la ndani bali
halijaeleweka na vijana wanaohudhuria hapo kwa shughuli mbalimbali,
jitihada zifanyike ili kuwa na vituo vya aina hii katika maeneo
mengine. Lengo kuu liwe ni vijana na wanawake bila ya kuonesha dalili
za kidini.


Tuwaoe wanawake wao kwa kusilimu kimajina

Jitihada za makusudi zifanyike ili kila itakapowezekana kuwaoa
wanawake wa Kiislamu ili tuweze kuwabatiza baadae, njia nzuri iwapo
patakuwa na ugumu ni kusilimu kiuongo ili kuruhusiwa kuwaoa wanawake
wao.

Tuanzishe NGOs na sisi tuwe viongozi

Kwa kuwa hivi sasa wafadhili wengi wameonesha hamu ya kuzisaidia NGOs
moja kwa moja badala ya serikali ni lazima tujitahidi kuunda jumuiya
zetu ambazo zitawashirikisha Waislamu lakini uongozi wa juu ni lazima
uwe mikononi mwetu. Hii itatuwezesha kuona sera zetu na malengo
yanatelekezwa kwa kivuli hicho.


Tujenge ukaribu na viongozi ili kuwadhibiti Waislamu

Mambo yetu mengi yamekuwa yanakwenda vizuri katika maeneo mbalimbali
baada ya wenzetu kuwemo katika kamati za masheha, na matawi ya vyama,
na kamati za maendeleo za maeneo mbalimbali. Hali hii ni lazima
iongezeke ili udhibiti wa shughuli za Waislamu uwe mzuri zaidi na
wakati huo huo kuona kuwa mambo yetu yanakwenda yakiwa na baraka ya
vyombo vya dola na vyama vya siasa.


Tuwachonganishe Mashehe wenye msimamo mkali

Mashehe wenye misimamo mikali wamekuwa ni tatizo kwa Ukristo kwani
wana wafuasi wengi na wamekuwa wakisema wazi na kushutumu maendeleo
yetu. Mashehe hao ni lazima wachonganishwe na serikali ili hali
ikiruhusu wazuiliwe kuendesha shughuli zao. Wakati tukifanya hivyo
hatuna budi kuwaunga mkono Mashehe wote ambao wamekuwa wakitusaidia
kwa njia mbalimbali.


Tulenge kuifuta Tabligh

Pamoja na kuwa na Tabligh sio hatari moja kwa moja kwa Ukristo lakini
bado inastahili kupigwa vita kwa sababu ina aina pekee ya mihadhara ya
Waislamu inayoruhusiwa humu Zanzibar. Tabligh inaweza kuwazindua
baadhi ya Waislamu ambao ni vema kubaki bila ya kuzinduliwa.

Tudai turudishiwe taasisi zetu


Serikali ya Zanzibar bado inaonekana kuwa ngumu katika milki ya
makanisa, ardhi na taasisi zetu. Dalili za huko nyuma zilionekana
nzuri kwani tulifanikiwa kupata hospitali yetu Walezo na eneo la
Kiugani hata hivyo panakuwepo na ugumu wa kurudishwa shule zetu. Kwa
kuwatumia wenzetu waliomo serikalini na baraza la wawakilishi
tuzidishe harakati na madai ya taasisi zote zilizobaki.


Tulete waumini kutoka mashamba kuanza makanisa

Hivyo sasa pameibuka wasi wasi kuhusiana na wingi wa makanisa ambayo
hayajapata waumini wa kuyajaza. Ili kuficha dosari hii na hoja kadhaa
utaratibu uliopo hivi sasa chini ya baadhi ya makanisa ni lazima
uungwe mkono. Wakristo wahamiaji wengi hufikia mashamba hivyo pawekwe
na utaratibu wa kuwaleta mjini ili kujaza makanisa.

Neno la mwisho

Wapendwa katika Bwana.


Miongozi hii ni mikubwa na inaweza kuwatisha baadhi ya waumini wa
Kikristo hasa wale ambao bado hawajampokea Roho Mtakatifu vizuri. Hata
hivyo, kwa uwezo wa Bwana Mungu wetu ni mpango rahisi. Suala la muhimu
ni haya kufahamika na kila Mkristo apendae kumtumikia Bwana. Pia
hatuna budi kuishukuru awamu ya nne ya serikali ya Mapinduzi ambao
imefungua milango kwa Ukristo na kushuhudia ongezeko la makanisa.



Bwana awe nasi!
 
huu waraka ni wa kipuuzi,na waandishi wa waraka huu ni waislamu waliandika kwenda kwa waislamu wenzao ili kuzidisha chuki kati ya waislamu na wakristo...Kwa watu wenye elimu hawawezi wakaa chini na kuandika ujinga kama huu,ndugu zanguni poleni sana kwa kukosa cha kufanya na inaonyesha ni jinsi gani msivyo elimika.Zanzibar yenyewe ni kama nusu mkoa wa Tz bara.Shule ni muhimu sana ndugu zanguni wa Zenji.
 
Kama na huu unyonge wa mawazo tunawarithisha mpaka watoto wetu basi kila kukicha hatutaisha kulalama. Hivi hatuna muda wa kufanya mambo yanayotuongezea vitu vya muhimu kulikoni kuundeleza huu udini unaotuletea uduni?
 
Kweli Tanzania Imeelemewa kabisa na Udini, sijui mwisho wa mambo haya utakuwa ni nini!?
 
Mada reeeefu pumba tupu. Juu ni uchochezi tu wala sio kingine. Udini hadi utosini. Kwishenei
 
sijui huu udini ni kaugonjwa kapya kameingia au kalikuwepo siku zote?
 
What a shame!!!! Yaani unatumia muda wako kutunga waraka wa uchochezi?? Siamini kuwa wakristo wanaweza kuandika upupu kama huu. Usitake kupandikiza chuki kati ya Waislam na Wakristo, usitake kuleta ugomvi na kuharibu amani yetu. Usilete udini hapa!!! Serikali wala katiba ya nchi haina udini japo wengine wanataka kupindisha ili walete udini!!!! Umaskini wa mawazo!!
 
Unajua waswahili wanasema anayedhania amesimama aangalie asianguke. Dini safi haina hila ndani yake wala agenda za kuona kina mama na watoto wanateseka bila sababu sababu ya vita. Kuna watu wanalao lakini wanataka kutumia mgongo wa dini kutimiza azma zao. Na wasindwe na kulegea. Hii sio Somalia, Sudan au Pakistani ni Tanzania.Lazima tuheshimiane kama tunataka kuishi kwa amani na sio huku kuzuriana na kupigana fitna kwa vigezo vya dini. Aibu kweli!!!
 
Waraka maalum kwa Wakristo Zanzibar

Wapendwa katika Bwana,



Tusahau tofauti zetu dhidi ya adui

Ingawaje tupo madhehebu nyingi lakini tunawajibika kuelewa kuwa
Waislamu na Uislamu wao ni adui yetu namba moja ambaye hatutofaulu
kupambana nae mmoja mmoja. Uislamu hapa Zanzibar ni dini iliofungamana
na mila na utamaduni hivyo kila itakavyowezekana tusahau tofauti zetu
ndogo ndogo na hata kubwa kukabiliana nao, vingienvyo tutarudi kama
wakati wa Karume.



Neno la mwisho

Wapendwa katika Bwana.


Miongozi hii ni mikubwa na inaweza kuwatisha baadhi ya waumini wa
Kikristo hasa wale ambao bado hawajampokea Roho Mtakatifu vizuri. Hata
hivyo, kwa uwezo wa Bwana Mungu wetu ni mpango rahisi. Suala la muhimu
ni haya kufahamika na kila Mkristo apendae kumtumikia Bwana. Pia
hatuna budi kuishukuru awamu ya nne ya serikali ya Mapinduzi ambao
imefungua milango kwa Ukristo na kushuhudia ongezeko la makanisa.



Bwana awe nasi!

Mpaka hapo nsha mjua huyu mpotoshaji na lazima nimuumbue wait a minute.......
 
hmm! kama unataka kujua kama unaweza kumpa mkeo ,kanunue then ujaribu kwake uone kama itafanya kazi,usiogope kujaribu,kujaribu ndio kujifunza kwenyewe huko.

naona ndugu yangu mkeo amekushinda hadi unataka kumuekea madawa? mlete kwangu nimpatie limbwata origino.
progress.gif

Wewe ndo unasema mkristo achakucheza na dini za watu.
 
huu waraka ni wa kipuuzi,na waandishi wa waraka huu ni waislamu waliandika kwenda kwa waislamu wenzao ili kuzidisha chuki kati ya waislamu na wakristo...Kwa watu wenye elimu hawawezi wakaa chini na kuandika ujinga kama huu,ndugu zanguni poleni sana kwa kukosa cha kufanya na inaonyesha ni jinsi gani msivyo elimika.Zanzibar yenyewe ni kama nusu mkoa wa Tz bara.Shule ni muhimu sana ndugu zanguni wa Zenji.

Acha matusi wewe, umejuaje kuwa Waraka huu umeandikwa na Waislam. Siri imetoka, Waraka wenu ueonekana sasa mnataka sema waliandika ni Waislam. Kila jambo ni Waislam japo mfanye nini, nani kakuambia kuwa Wazanzibar hawajasoma, na unatumia kigezo gani mtu kuwa msomi.

Acha chuki zako wewe na wenzako, sasa mliokuwa mnayafanya gizani yanatoka, unadhani ni ile miaka ya kupelekeshana bila kusikia kelele.

Pia jihadhari na matusi, toa hoja.
 
Acha matusi wewe, umejuaje kuwa Waraka huu umeandikwa na Waislam. Siri imetoka, Waraka wenu ueonekana sasa mnataka sema waliandika ni Waislam. Kila jambo ni Waislam japo mfanye nini, nani kakuambia kuwa Wazanzibar hawajasoma, na unatumia kigezo gani mtu kuwa msomi.

Acha chuki zako wewe na wenzako, sasa mliokuwa mnayafanya gizani yanatoka, unadhani ni ile miaka ya kupelekeshana bila kusikia kelele.

Pia jihadhari na matusi, toa hoja.

matusi yangu yako wapi? sina chuki na mtu/watu.ukweli ndio huo kuwa huu waraka ni wakipuuzi na mwandishi wake ni mpuuzi
 
Nakushukuru ThinkPad kwa data zako za maana, sasa tumeweza kumfaham huyu mchonganishi wetu. Tunaomba asirudie tena kuweka waraka usio na manufaa kwa Taifa letu. kama hana kitu cha kufanya basi alale au acheze bao kuliko kuleta uchonganishi katika nchi yetu. Kwa maoni yangu huu waraka ni wa KIPUUZI SANA!!!!!!!, kwani mtu mwenye akili huwezi kamwe kuandika haya. Lakini sisi tunamsamehe, kwani yawezekana hajui alitendalo.
Jamani tusikubali mada zozote zenye kutugawa katika misingi ya dini, kabila, rangi, jinsia, nk.
Mada kama hizi zisingepewa nafasi katika blog hii ya Great thinkers. Tusipoangalia kesho atakuja mtu na mada za ajabu kuliko hizi, za kutugawa.
 
matusi yangu yako wapi? sina chuki na mtu/watu.ukweli ndio huo kuwa huu waraka ni wakipuuzi na mwandishi wake ni mpuuzi

Matusi hakuna hapo, kama mtu akileta waraka wa kipuuuziiiiiiiiiiiiii kama huu lazima aambiwe, ili ajue hatumuungi mkono kabisa.
waraka wa kipuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Wewe ndo unasema mkristo achakucheza na dini za watu.
ThinkpPad ,uelewa wako unafanya kazi vizuri? nauliza hivyo kwa sabaubu nimeshangzwa na post zako hapa.hoja iliyoko hapa nitofauti na vitu ulivyokuja navyo.Mkuu sijacheza na dini za watu kwani nina heshimu imani za watu.hii hoja nimeichukua kwenye forum wanabidii baada ya kuisoma nakuona kilichomo ndani kina tatanisha,hivyo nimeichukua kuileta hapa ili kushare na wanaJF. Huko ndiko kucheza na dini za watu? hii post ili wekwa bidii na Leiila Abdulli jana na imeleta mzuzo sana.Waraka maalum kwa Wakristo Zanzibar (??????) From Who?? - Wanabidii | Google Groups

heshima ni kitu cha bure jamani.Mtu usikurupuke tu na kuropoka hovyo watu watakucheka kaachini fikiria kwanza kabla ya kuropoka.
 
ThinkpPad ,uelewa wako unafanya kazi vizuri? nauliza hivyo kwa sabaubu nimeshangzwa na post zako hapa.hoja iliyoko hapa nitofauti na vitu ulivyokuja navyo.Mkuu sijacheza na dini za watu kwani nina heshimu imani za watu.hii hoja nimeichukua kwenye forum wanabidii baada ya kuisoma nakuona kilichomo ndani kina tatanisha,hivyo nimeichukua kuileta hapa ili kushare na wanaJF. Huko ndiko kucheza na dini za watu? hii post ili wekwa bidii na Leiila Abdulli jana na imeleta mzuzo sana.Waraka maalum kwa Wakristo Zanzibar (??????) From Who?? - Wanabidii | Google Groups

heshima ni kitu cha bure jamani.Mtu usikurupuke tu na kuropoka hovyo watu watakucheka kaachini fikiria kwanza kabla ya kuropoka.

Utachukuaje taarifa usiyoijua na kuileta hapa, basi mwanzoni ungeweka angalizi kwamba hii siyo taarifa yangu, nimeitoa katika blog. Ungekuwa wa maana ungefanya utafiti japo kidogo tu kabla ya kuweka taarifa ya kipuuuzii kama hii.
Kuweka mada za kipuuziii ambazo hazijafanyiwa utafiti, mada na mwenye mada wote ni wapuuuziii, tena wakubwa.
Yatakiwa uombe msamaha kwa kosa hilo
 
Nadhani kuna vijiwatu vya hovyohovyo vinapandikiza chuki tz;ili wao wapate mwanya wa kufanikisha issue flani then waende canada;ole, ole, ole ,wenu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom