Wapo Wanasiasa waoga na wameshindwa kukabiliana vilivyo na Washindani wao

Philipo Mwakibinga

Senior Member
May 13, 2013
111
175
WENZETU WAMEWEZAJE KUWA VIBARAKA WA MABEBERU?

Uoga dhidi ya Washindani wao. Wapo Wanasiasa waoga na wameshindwa kukabiliana vilivyo na Washindani wao kisiasa katika Mataifa yao. Hivyo hufikiri na kuamini kuwa kwa kuomba msaada wa usaidizi kutoka kwa Mataifa ya Kigeni hususani ya Ulaya itawarahisishia wao kupambana dhidi ya washindani au maasimu wao kisiasa.

Ujinga na Ukosefu wa Uzalendo. Ujinga na ukosefu wa uzalendo miongoni mwa baadhi ya Wanasiasa kwa mataifa yao ni msukumo mwingine unaosababisha wakimbilie kuomba misaada kwa mabeberu kwasababu wanaamini Mabeberu wanauchungu na kushindwa kwao katika medani za kisiasa.

Roho mbaya na Fitina. Wapo wanasiasa ambao wamejivika roho mbaya na Chuki hivyo wamekuwa na roho ya tukose wote. Kwa tabia hii wanajua kabisa kuwa Wageni wa Kibeberu ni waharibifu wanaposaidia vibaraka walioomba msaada. Hivyo vibaraka hufurahi kuona jamii inaangamia na uongozi hautawaliki na uhisi kuwa hiyo ni kama njia nzuri ya kuwakomoa Wakinzani na mahasimu wao kisiasa.

Ndoto za Kibepari na Ubinafsi wa kiwango cha Juu. Wapo Wanasiasa wenye ndoto za kuwa Mabepari na wenye kumiliki mali nyingi kupitia siasa. Hivyo wakoradhi kuhakikisha Wanatafuta madaraka kwa njia iwayo yoyote ile ilimradi wanakua viongozi ili wachume mali kwa manufaa yao binafsi. Hivyo wanapokosa nafasi wapo tayari kushirikiana na yeyote kwa njia haramu ilikutimiza ndoto zaohizo hatimaye hutumbukia kwenye usaidizi wa mabeberu.

Kulipa Kisasi. Wapo wanasiasa waliopita maswahibu mengi na mapito magumu katika harakati zao za kisiasa ambapo kwa muda wote huamini kuwa madhira yote hayo wamesababishiwa na maasimu wao kisiasa. Hali hii husababisha wanasiasa hao kuomba msaada kwa mabeberu ili watimize adhima yao ya kulipa kisasi.

Lazima jamii itambue kuwa kwasababu yoyote ile hakuna taifa lolote lenye uchungu kwa hatima ya Tanzania zaidi ya Watanzania Wenyewe. Hivyo tabia ya baadhi ya Wanasiasa kuvuka mipaka na kwenda ng'ambo kuomba misaada ya hatima ya siasa zetu ni kujitia kitanzini na kuhatarisha taifa letu. Ni,tabia mbaya sana na hatari kwa ustawi wa jamii yetu tukome na tukomeshe hulka hii.

Philipo Mwakibinga
0758-910-403.
 
Hizi ni akili za hapo nyuma ambapo chief Mkwawa alikuwa kawazidi uwezo wa kinguvu walimuunga beberu kumpiga mwafrika mwenzao mwishoni tukatawaliwa wote huu unaofanyika sasa hauna utofauti na ule wa kitambo alafu unakuta mtu anasupport
 
Naliona vazi la kijani likikosa heshima mtaani, wamiliki amkeni mpangaji anazidi kita mizizi kujimilikisha kwa garama kubwa za kuharibu umoja na ustawi wa taifa letu.
 
We afisa kipeuo uchwara hebu nao wapinzani wamiliki jeshi , polisi, magereza silaha halafu ndio uwaambie wakabiliane nao Pimbi mkubwa .
 
Wewe shida yako siku zote hua ni kushibisha tumbo tu. Mbaya zaidi imeambiwa wakati huu teuzi hakuna maana zimejazwa na wenyewe.

Ulioandikwa hapa ni upuuzi na ujinga mtupu wa kujikomboa kama kawaida yako.

Watu wanatishwa wanatumiwa sms za vitisho, Kura zomeibiwa wazi wazi na dunia nzima inajua, mawakala wanazuiwa kuingia vituoni bila sababu msingi hili bilioni?

Eti ni watu wakiongea ukweli wamatumiwa na vibaraka, hopeless kabisa wewe na hujui kiti
 
MWAKIBINGA UNAWADHALILISHA SANA WATU WA MBEYA.

WAMECHOSHWA NA UNAFIKI WAKO.

Nikiona maandishi yako nakumbuka Hotuba ya Mwalimu Nyerere kuwa
" WANASIASA WANA TABIA ZA KIMALAYA MALAYA".
 
Huna lolote wewe, unapatana na aliye tayari kupatana. Mtu anayepora wenzie ilmradi atangazwe yeye kwa 99% hana mipango ya kupatana.

Hao unaowaita wajinga, wana mchango mkubwa ktk ustawi wa democracy ya nchi hii. Wewe unayejiona una akili mchango wako ni zero katika makuzi ya democracy yetu. Unaweka namba kutafuta ugali , huna lolote
 
Back
Top Bottom