Wapinzani wa nchi hii hawajui wanachotaka. Kila rais anaeingia madarakani hawamtaki

Mganguzi

JF-Expert Member
Aug 3, 2022
1,032
2,769
Wana laana isiyoisha au tuseme hawajui wanachotaka Mkapa walimwita dikteta na kumtukana Kila aina ya matusi, amemaliza salama amelala!

Kikwete alipoingia alikula matusi Kila mahali yaani huyu ndio rais mwenye roho ngumu kwa sababu huyu walimuonea kwa kuwa alikuwa anakaa kimya!

Matusi waliokuwa wanamtukana mengine huwezi kuyaandika humu baba yule kamaliza mhula wake yupo Msoga ametulia.

Ameingia Hayati Magufuli tinga tinga lile walifyata mkia kama hawapo! Yaani hata kukohoa walikoholea vyumbani, Sabaya na Makonda peke yao walikuwa wanaamua leo wakalale wapi na wanatii amri.

Wakalalamika sana, baadae kamanda yule amelala, kaja mama mpole, mvumilivu na msikivu kuliko wote huenda! Anawapa Kila wanachotaka.

Walikimbia hata nchi wamerudi kwa ajili yake baada ya kuona usalama wa uhakika upo ,Leo Tena hao wanamtukana na kukebehi.

Hawa sasa wametuchosha wakiingia balabalani watandikwe sana ,mpaka wasahau kwao na wakuwatandika sana ni wale viongozi
 
Aisee huo ndio upinzani mkuu .
Zumuni la chama Cha siasa ni kushika atamu,Dola Sasa uwezi shika Kwa kutoa matamko ya kumpongeza mtawala.
Unapaswa kuangalia madhaifu ya mtawala ndo unapita humo humo
 
Nchi hii imekua na ongezeko la wajinga badala ya kupungua.
Kwa taarifa Yako hata CCM wenye akili wanatamani uponzani uendelee kuwepo na uendelee kuipinga
 
Kwa hiyo unataka hao wapinzani na wenyewe wageuke kuwa CHAWA? Yaani muda wote ni kusifia tu. Hata kama ni kitu cha kijinga! Wao ni kusifia tu.
 
Back
Top Bottom