Wapinzani, vigezo mnavyotumia ndiyo sumu yenu

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
245
312
Ukitizama chaguzi mfano UK na US utaona ikifika kuchagua nani apeperushe bendera ya chama wapinzani wanaangalia uwezo na mawazo ya watangaza nia. Kamwe hawachagui asiye na uwezo au mawazo bora. Sasa rudi Tanzania. Wapinzani wanatumia vigezo hivi kumpata mpeperusha bendera:

1. Mwanachama wa chama tawala aliyekorofishana na chama tawala.
2. Mtangaza nia anayeonyesha ufundi wa kukitukana chama tawala kushinda watangaza nia wenzake.
3. Mtangaza nia ambaye ana historia ya kuumizwa au kugombana na chama tawala kushinda wenzake.

Ndivyo vigezo vilivyotumika kwa kumteua Seif, Slaa, Duni, Mbowe, Lowassa, Membe na Lissu. Hawachagui aliye na sifa ya kuwa raisi! Kwao sifa ya kuwa raisi ni hivyo vigezo vitatu. Ukiwa navyo utapewa bendera!

Mfano mzuri ni huu wa CHADEMA. Japo watia Nia wote hovyo lakini Nyalandu ni bora kuliko Lissu. Tatizo Nyalandu alikosa sifa 2 kati ya hizo. Haswa sifa ya kuitukana CCM! Maneno yake ya busara kuhusu Marehemu Mkapa ndio yalimuondokea kabisa sifa Kwa wajumbe. Mpeperusha bendera wa chadema ni kosa la jinai kusifu!

CCM unaweza usiwapende lakini wanavyompata mpeperusha bendera wao ndio siri ya ushindi wao. Wanazingatia uwezo wa mtangaza nia.

Hata sasa jaribu kupima hawa: Seif Vs Hussein na Rais Magufuli vs Lissu/Membe. Wamepatikana kwa vigezo vipi? Jibu lake ndio jibu la oktoba licha ya vitisho vya kuingia barabarani na kudharau Mungu.
 
ficha hilo box tupu lako kichwani pengine utaonekana na busara sifa za kua raisi unazijua wew? zitaje hapa alafu niambie nani wa ccm anazo ambazo wa upinzani hana..
 
Kuna mgombea wenu mmoja, baada ya kuukwaa u rais alitamka hadharani kazi ni nzito hakujua alikua ana beep tu.

Hakuna mgombea wa upinzani aliyewahi ku peeb nafasi ya u rais.
 
Back
Top Bottom