Wapiga kura wa Mnyika wavamia Manispaa ya Kinondoni

Julius Mgaya

Member
Sep 20, 2011
25
4
Jana majira ya saa 3 Asubuhi wananchi wa Kata ya Goba, Makuburi na Ubungo ambao ni wapiga kura wa MNYIKA walivamia Manispaa ya Kinondoni wakitaka kuonana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg. F. Fwema ili kupata majibu kuhusu Matatizo ya Maji-Goba, Utekelezaji wa ujenzi wa Barabara ya Makoka-Makuburi pamoja na Ujenzi wa Daraja la External-Ubungo.

Wananchi hao wanasema licha ya fedha za ujenzi kutegwa ambapo Barabara ya Makoka-Makuburi imetengewa Milioni 101,840,00 Daraja la External-Ubungo limetengewa Bilioni 1.2 lakini hakuna hatua yoyote ya ujenzi iliyochuliwa na Manispaa ya Kinondoni ili kuharakisha ujenzi wa Miundombinu hiyo inaanza haraka licha ya juhudi kadhaa alizofanya Mbunge wao John Mnyika kushughulikia Matatizo hayo lakini Manispaa wamekuwa hawampi ushirikiano wa kutosha, hivyo kuona bora waje wenyewe kwa mkurugenzi huyo ili kupata majibu na lini utekellezaji wa ujenzi utaanza.

Kufuatia hatua hiyo afisa Utawala na Utumishi wa Manispaaa hiyo alilazimika kuomba msaada wa Polisi wa kutuliza ghasia FFU ili kuja kulinda usalama wa Manispaa hiyo kutokana na kundi kubwa la wapiga kura hao kusema hawatatoka mpaka wamuone Mkurugenzi huyo au waitiwe Mbunge ili aje kuwasaidia. Polisi hao walizingira mageti ya Manispaa hiyo kwa saa kadhaa na kisha kuondoka baada ya kuona wananchi hao hawakuwa na nia ya kufanya vurugu bali walikuja kwa amani.

Baada ya wananchi hao kukaa zaidi ya Masaa 4 wakimsubiri mkurugenzi huyo, Manispaa hiyo ililazika kumuita Mnyika ili kuokoa jahazi kutokana na hali kuwa mbaya katika ofisi kadhaa za Manispaa hiyo ambazo wananchi hao walizizingila mpaka wamuone Mkurugenzi. Baada ya kuja Mnyika, Mkurugenzi wa manispa hiyo alilamika kukatisha ziara yake na Mkuu wa mkoa na kuja kuongea na wananchi hao ambapo walimweka kitimoto mpaka majira ya saa 12:33 Jioni walipopata ufumbuzi wa masuala yao ambapo Mkurugenzi alihaidi kupitisha Grader katika barabara ya Externala na ya Makoka pamoja na kwenda kufanya ziara Goba siku ya Jumamosi ya tarehe 28/01/2012.
 
Sawa kabisa Nguvu ya Umma ndo kila ki2...nawapenda sana wananchi wa Ubungo make mda wote huwa tayari kumsaidia mbunge wao pale panaoonekana kuingiwa mizengwe

big up!
 
Kila Jimbo tungelifanya hivi. Huenda viongozi wetu waliopo usingizini wangeamka.

Hakuna Jimbo lisilo na matatizo / kero.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hongereni wananchi na wapiga kura wa jimbo la Ubungo kwa kuungana pamoja kusaidia juhudi za mbunge wenu Mh Mnyika,hii ni kwa faida yenu,siku zote nguvu ya umma ni silaha inayoshinda silaha zote,na imekuwa ni kawaida ya serikali hii ya CCM-Magamba kukwamisha shughuli za maendeleo katika majimbo yanayoongozwa na wabunge wa upinzani hasa CDM.na hii inaonekana kulikuwa na mizengwe katika kuondoa kero za wananchi wa jimbo la Ubungo licha ya fund kuwa allocated.endeleeni kukomaa mpaka kieleweke.
 
Hii ndio inatakiwa,
Haki yako unaifuata huko huko,
Hakuna kuisubiri, watapandia ndege
 
Back
Top Bottom