Wapiga kura jimbo la Iringa Mjini wamshangaa mbunge wao, Msigwa ana kazi kubwa kutetea kiti chake

watu wengine bana .... yaani umeona uache kufanya kazi zako za siku zote zinazokupatia ujira na kipato halali huko london (freight agent) .... umeingia kwenye kazi za masalia ... kazi zenye kuhitaji kijidhalilisha, unafiki, chuki na kuuza uhuru wako

hongera sana chillisosi kwa kurudi nyuma nyuma katika maisha yako ... kunguru watasikiliza dua lako
 
Kwani wewe ni nani anayekufahamu? we ni monster
Weka jina lako kamili hapa...
Usilete Uchilisosi wa kwenye chipsi na jikoni kwenu hapa
Sema jina watu wakujue, kama utadhubutu!
Usikae mitandaoni kupiga majungu..
Kama unauwezo jitokeze sasa mbele ya wana Iringa uwaambie dhamira yako.
Chillisosi Utachacha wewe.

we ghost...kama siyo sema jina lako! na hapo iringa unakaa wapi ili ueleweke mapema.
jini wewe!!!!
 
Boss,
Iringa ni mji mkubwa sio kijiji OK?
Gari moja haliwezi kuzoa taka.
Siwezi kukuambia chilisosi ana mpango gani lakini haya ndio yatakuwa majibu yangu na sio moja na sitachangisha mtu
600

600

na kuna kitu kinaitwa wheel bins.
Let's see what happens next
YOU DONT NEED TO BE A GENIUS TO KNOW WHAT PEOPLE WANTS!

Meya ni mwanaccm, madiwani wote isipokuwa mmoja tu ni wa CCM, mtaa unaoongoza kwa uchafu kitanzini diwani wake ni Jesca Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa wote hawa hakuna wanachofanya, umeshawahi wauliza wao wamefanya nini kuondoa uchafu na kuleta maendeleo?

Wananchi wanatambua kuwa mnamhujumu Msigwa na pia Kwa taarifa yako wapo wanaccm wengi wenye mawazo kama yako na mtapoteza jimbo tena maana mnaendelea kufikiri kuw Iringa ya sasa ni ya mwaka 2000.
 
Wewe Chilisosi, kazi ya mbunge sio kuleta kwa fedha zake miundombinu mbalimbali, bali ni kuwaunganisha wananchi na kuishawishi serikali kuunga mkono juhudi za wananchi. ukikaa na wananchi, ukafanya usafi pamoja nao, ukawaelimisha kuhusu usafi, hautahitaji nguvu kubwa ya kuleta magari hayo ila wananchi watapunguza kasi ya kuchafua miji kwa kuona aibu kwamba wanamlazimisha kiongozi wao kuja site kufanya usafi.
 
Moja ya kazi za MSINGI kabisa za Mbunge ni mji wake kuwa msafi?Na akishindwa kufanya hivyo asichaguliwe uchaguzi ujao?

Tunaacha kuwabana wabunge wetu wafanye kazi ya kuidhibiti serikali na kuiuliza iweje deni la Taifa limefikia trillion 22 ili hali maisha yetu bado hayana afadhali(Deni la Taifa liko kubwa sana na litaifanya TZ isikopesheke na international monetary institutions na tutafirisika kama tu Ugiriki)

Hatuwaulizi wabunge wetu watunge sheria ya kulinda wakazi wa ilipogunduliwa mali asili
(Gas Mtwara na Lindi) ndiyo wawe wa kwanza kufaidika; Hatuongelei lolote kuhusu kila siku kupatikana makontena ya pembe za ndovu zikisafirishwa toka TZ kwenda huko Bara Asia;lkn leo hii eti tuwe shupavu kuwabana na kuwauliza wabunge wetu kwa kwa nn Mtaa wa Mtwavila na Mshindo sio msaafi?Hiki ni kichekesho cha karne kwangu!

Naanzia na wa Kwangu Kyela yaani ASIRUDI 2015 MAANA KYELA SIO SAAFI!Kwa maoni yangu hii ni hoja ya ajabu kabisa kuletwa JF labda toka forum hii ianzishwe!
 
Japokuwa mimi ni 'mwanaCCM' lakini ukweli lazima niuseme hapa.
*Mpaka sasa sijaona jimbo lolote linaloshikiliwa na CHADEMA kama linaweza kurudi CCM mwaka 2015, kwa sababu zifuatazo:
1/Wabunge wa CHADEMA ndio wameonyesha umahiri mkubwa sana ndani ya Bunge lililopo.

2/Wako karibu sana na wapiga kura wao katika kusikiliza kero zao, kufafanua mambo na kushirikiana nao kijamii.

3/Kila mmoja wao amekijenga chama chake cha CHADEMA kimtandao kwa sehemu kubwa sana katika jimbo lake toka kwisha uchaguzi wa 2010.

4/Wote wana uhakika wa kupitishwa tena na CHADEMA kutetea nafasi zao 2015.

*Kwa sababu hizo tu hapo juu, sio nafasi yoyote iwe kwa mwanaCCM yoyote awe Monica Mbega, David Mwakalebela au Christ Lukossi kuweza kumshinda Pastor Msigwa mwaka 2015 jimbo la Iringa mjini kama watataka kupambana naye.
 
Boss,
Iringa ni mji mkubwa sio kijiji OK?
Gari moja haliwezi kuzoa taka.
Siwezi kukuambia chilisosi ana mpango gani lakini haya ndio yatakuwa majibu yangu na sio moja na sitachangisha mtu
600

600

na kuna kitu kinaitwa wheel bins.
Let's see what happens next
YOU DONT NEED TO BE A GENIUS TO KNOW WHAT PEOPLE WANTS!

i dont think if it requires you a political position to assist the people of Iringa municipal,just your conscience,unless you can tell me that you ought to give something with an expectation of earning alot in the near future.
 
Watu wa Iringa ni waelevu wa kutosha sidhani kama watadanganyika kwa pipi na peprmrnde. Huyu Chilisosi akipata ubunge hata kaa akanyage Iringa maana kazi zake nyingi ziko UK. Acheni ujinga wa kushabikia watu kwa kuwa letea viraza wewe kama una maslahi binafsi na Kilaza mwenzako usije sababisha jamii ikapata shida kwa muda wa miaka mitano bila kuwa na mwakilishi. Viongozi wangapi nje ya nchi wanafanya usafi iweje la Dr Msigwa liwe kituko? watanzania ifike kipindi baadhi yetu hata kama hatuna akili basi tukope kwa kutusaidia kufikiri
 
Msigwa anapiga kazi sana huyu jamaa ila kuna baadhi ya magamba wakishirikiana na waandishi njaa kama Francis Godwin bila kuficha wanafanya mbinu za kumchafua Msigwa...kata karibia kumi na sita zote zinaongozwa na madiwani wa ccm na ukipita kwenye hizo kata kuna taka nyingi sana hao madiwani wanafanya nini kama sio chuki tu na unafki wenu?kuna meya wa mji anaitwa mwamwindi anafanya nini naye?Mbunge Msigwa kwenye mikutano yake amezungumzia sana suala la taka na hatua stahiki anazofanya ila anakosa sapoti kubwa sababu akiingia kwenye vikao vya baraza la madiwani...madiwani wa ccm wamekuwa wanaenda kinyume eti watampa Msigwa umaarufu huo ni upuzi kabisa.....Mbunge Msigwa ni mchapa kazi jamaa ni jembe sana...
 
Umechelewa japo hujachelewa sana. Rudi kamwambie alie kutuma kua HATUDANGANYIKI TENA NA CCM. Mmekwisha habar yenu!
 
Mbunge asimamie usafi? jamani huu ni utani wa mtoa maada hii, wakati mwingine tumia hata busara kidogo unajivunjia heshima yako, mpongezeni mbunge kwa initiative zake. Hongera Mch Msigwa wewe ni mfano wa kuigwa
 
Kati ya wabunge wa CDM wenye wakati mgumu kutetea kiti chake mchungaji anaongoza.Nahisi Kama itakula kwake
 
Mmmh,, utakuwa umemuonea mchungaji. lakini nina wasi wasi asije akawa anatumia sadaka za watu kuzolea taka kinyume na kanisa

Amemuonea kwani anatembea uchi? Acha maneno ya kejeli wewe sadaka zipi ametumia kwani kukodi gari kwa siku ni shillingi ngapi? Mnajisumbua bure kama ndo gia ya kusaka ubunge hata kwenye hicho chama chenu cha magamba kwenye kula za maoni hutoboi utajalalamika.
 
WAPIGA KURA JIMBO LA IRINGA MJINI WAMSHANGAA MBUNGE WAO



WAKATI mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (pichani )na viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) leo walijitolea kufanya usafi katika eneo la kitanzani mjini Iringa kama njia ya kuhamasisha usafi, wapiga kura wa jimbo hilo wameonyesha kutofautiana na uamuzi huo wa mbunge kufanya usafi huku baadhi yao wakidai kuwa jimbo hilo limemsinda kuongoza na ndio sababu ya uchafu kuzagaa kila kona ya mji .


" Mbunge wetu leo anajitolea kufanya usafi siku zote alikuwa wapi hadi uchafu unazangaa kiasi hiki mitaani .....tunamtaka Msigwa kufanya kazi kama wabunge wengine na kuachana na siasa za kuunga unga na kutafuta umaarufu kwa watu "


Wakizungumza l;eo kwa nyakati tofauti wananchi wa jimbo la Iringa mjini walisema kuwa mji wa Iringa umeendelea kuzidiwa na uchafu na kuwa mbali ya mbunge kujitolea kufanya usafi pamoja na wanachama wa Chadema ila bado hatua hiyo haiwezi kutatua tatizo la uchafu na badala yake uchafu wa Manispaa ya Iringa utaendelea kuwepo .


Juma Husein mkazi wa Kitanzini katika Manispaa ya Iringa alisema kuwa mbunge wao anatafuta umaarufu wa kisiasa na kusahau kuwa yeye ni mbunge wa jimbo la Iringa mjini na mwakilishi wa wananchi hao bungeni hivyo alipaswa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa uchafu katika jimbo lake badala ya kufanya usafi kwa misingi ya kisiasa huku akitambua kufanya hivyo ni kujichongea mwenyewe kwa wananchi kuwa kumbe ameonyesha kushindwa kuongoza jimbo hilo na ndio sababu ya taka kuzagaa kila kona.


Husein alisema ni vema mbunge Msigwa kwenda kujifunza katika jimbo la Moshi mjini ambalo pia linaongozwa na mbunge wa Chadema na kuona kama mbunge huyo ametumia mbinu kama hiyo kusafisha mji ama kuna mbinu nyingine inatumika badala ya hiyo ya zima moto inayotumiwa na mbunge Msigwa sasa ya kukodi magari ya usafi.


Aidha alisema kuwa kwa kuwa Manispaa ya Iringa inakabiliwa na tatizo la magari ya kusomba takataka na uhaba wa vyombo vya kuhifadhia takataka mbunge Msigwa kwa kutumia mfuko wa jimbo alipaswa kuanza kushughulikia kero hiyo badala ya kukodi magari kwa siku moja ili kutaka kuonekana kuwa ni mchapakazi wakati siku zote yupo mjini Iringa na uchafu huo upo.


Kwa upande wake mbunge Msigwa alipoulizwa na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na utaratibu huo alisema kuwa kazi ya mfuko wa jimbo si kwa ajili ya kusafisha mji na kuwa yeye ataendelea kusafisha mji kwa muda wa siku mbili hizi kabla ya kwenda bungeni .


Msigwa alisema kuwa kupitia ofisi yake tayari amekwisha changisha kiasi cha shilingi milioni 16 kwa ajili ya kununua gari ya kubeba taka katika Manispaa ya Iringa ili kupunguza tatizo la uchafu katika mji huo.


Afisa afya wa Manispaa ya Iringa Severin Tarimo alipotafutwa na mwandishi wa habari hizi ili kueleza mikakati ya Manispaa ya Iringa juu ya hali ya uchafu inayoendelea kuukumba mji huo alidai kuwa kwa sasa yupo likizo hivyo anayeweza kujibia hilo ni yule aliyemwachia ofisi.


"Nazungumza na nani ....sasa mimi nipo likizo bwana naomba uongee na mtu mwingine" alikata simu


MWISHO
Source FRANCIS GODWIN BLOG

My take,
Msigwa kuna mtu anaitwa Chilisosi anakuja hapo hivyo jiandae vyema
CHILISOSI FOR IRINGA 2015


hayo mawazo yako yakupikwa! Jaribu kufikiri kwa kutumia akili!
 
Una uhakika na unayosema,
Hizi gari zinabeba uchafu wa aina zote na zina u compress ili ziweze kubeba mwingi, suala la mifuko ni chaguo lako lakini kama uchafu ukiwekwqa kwenye ma binss maalumu hili gari linazoa lenyewe na sio bei sana kama shangingi la mbunge, shangingi moja unanunua haya matatu, na mie nitafanya hili kwa mfano

Shangingi ni gari lake la kutmbelea wewe kiraza kwani linabeba uchafu huoni kafunga tera? Unaona jinsi uelewa wako jinsi uko finyu unasema eti mabins maalum sasa nayo utayaleta na utagawa kila nyumba? hayo magari yatakuwa na uwezo wa kusomba taka menyewe bila nguvu kazi za watu? Acha kuwadanganya wananchi. Nia na mawazo yako wakupe kura kisha usiishi Iringa uwe unaishi DSM na huku unako fanyia kazi kwa maslahi yako. Hatunganyiki sasa hivi na watu sio wale wa enzi za mkapa sasa tuanfikiri kwa digital kaka si analogue tena
 
Back
Top Bottom