Wapi pazuri pa kuishi?

August_Shao

Senior Member
Nov 23, 2007
164
47
Jamani naombeni ushauri wenu....nataka nikapange kati ya TABATA au Maeneo ya kuanzia Banana ukonga hadi pugu......sasa sina uzoefu wa maeneo haya naombeni ushauri wenu....

Naombeni samahani kwa kuiweka kama "breaking news "
 
unaikumbuka hadithi ya mtoto kulia "chui! chui!" wakati akijua ni uongo? Siku alipolia chui ukweli watu walimpuuza na matokeo yake aliliwa na chui.
Haya unaita hii nayo ni breaking news jamani!?
 
Ndugu karibu Kinyerezi, kwa kweli ni sehemu nzuri sana kuishi bado hakujazana watu kama mbezi beach halafu mipango miji ni A,hakuna purukushani za makontena ya baa na kuna hali hewa nzuri sana,
 
TABATA kubwa BUT Chang'ombe is best and Mawenzi better as well Kisukuru good. I once lived dea
 
Unakaribishwa Mbagala jeshini, disco la kijeshi (mabomu ) kila wiki .

Hata hivyo usijali utazoea tu kama walivyo zoea watu wa Kipawa kelele za ndege!
 
Kuchagua sehemu ya kuishi kunategemea mambo mengi tu muhimu kama vile wapi ofisi yako ipo, huduma zako muhimu kama hospital, soko nk unapata wapi. Ni vigumu mtu kusema ama kushauri ukae hapa ama pale ilhali hujaweka bayana baadhi ya mambo, una familia, uko kivyako vyako nk. Mi maoni yangu hiyo njia ya Banana sijui Ukonga mpaka Pugu, mmh, labda uwe unajenga na umeamua kuishi kwako. Lakini kwa kupanga... sijui
 
Back
Top Bottom