Wapi lilipo baraza la maaskofu?

Aug 5, 2011
11
1
msaada jamani nielekezeni wapi lilipo baraza la maaskofu kurasini. mimi natokea Sanza vatikani. nipande magari ya wapi na nishukie wapi? maana naenda kwenye interwiew j3
 
Lipo kurasini, kama ukija tokea mandera road ukifika mataa ya chuo cha Uhasibu kurasini basi ni unanyoosha nayo kwenda shmo la udongo, but hakuna magari ya abiria ya moja kwa moja ukija na mandera road so shukia kituo cha uhasibu, vuka upande wa pili panda gari la kariokoo wanaloita kariokoo shimo la udongo then utamwambia konda akushushe Baraza la maaskofu, offcoz sio mbali sana ukitokea uhasib bt kwa kua mgen panda gar! Kila la kheri mkuu!
 
panda gari la kariakoo, ukishashuka tafuta magari ya temeke au mtongani kupitia shimo la udongo, kituo ni baraza la maaskofu ambacho ni baada ya highway, au panda gari ya tandika ukifika tandika tafuta gari ya kariakoo kupitia bandari / shimo la udongo shuka baraza la maaskofu.
 
mimi nakushauri uchukue taxi mwambie akupeleke baraza la maaskofu. Usijioneshe sana kwamba una shida na maisha. Kwanza kwenye daladala utafika hususani hizo zinazopitia shimo la udongo utafika umechafuka sana
 
ukifika k/koo nenda pale kwenye geti la shule ya uhuru utakuta magari ya mtongani kupitia shimo la udongo mwambie konda akushushe baraza la masikofu.ukitoka highway kituo kinachofuata ndo hapo baada ya dalaja.mia
 
Sina uhakika na kituo cha kushukia lakini panda bus lolote linalopitia Shimo la Udongo (Bus hilo linaweza kuwa la Temeke, Tandika, Mbagala au Mtoni). Utamuuliza Konda atakuonyesha kituo lakini ni baada ya kupita ofisi za UDA. Mabus unapandia Posta Mpya au Kariakoo.
 
magari yanayopita shimo la udongo ni ya mtongani tu.mia
 
panda gari la kwenda mtongani au tmk ,shuka uhasibu
Vuka upande wa pili wa barabara panda gari yoyote inayopita shimo la udongo(zote zinaishia kariakoo),shukia biashara,angaza upande wa pili wa barabara utaona kibao cha mogas fuata hiyo njia kubwa bila kukata kona utafika,au ukishindwa ulinza walinzi kwenye mojawapo ya mageti maeneo hayo.
 
mimi nakushauri uchukue taxi mwambie akupeleke baraza la maaskofu. Usijioneshe sana kwamba una shida na maisha. Kwanza kwenye daladala utafika hususani hizo zinazopitia shimo la udongo utafika umechafuka sana

hivi huko shimo la udogno kwenyewe unakujua au?
 
msaada jamani nielekezeni wapi lilipo baraza la maaskofu kurasini. mimi natokea Sanza vatikani. nipande magari ya wapi na nishukie wapi? maana naenda kwenye interwiew j3

Jirani unaniangusha bhana.. Ni Sinza vatican.. Kifupi panda gari za ubungo, ukifika ubungo panda gari za mbagala shuka uhasibu.. ukifika hapo chukua boda boda elfu 1 mpaka elfu 1 na mia tano..
 
hiyo avatar yako tu imeshakukosesha kazi. huwezi kuwa mpenda kunyonya damu za watu halafu upate kazi ya kuifanyia kanisa. bora usiende tu umeshaliwa wewe labda ubadili avatar yako

Siyo Avatar tu aliyoikosea hata hiyo Sanza Vatican mi alishanipoteza nikadhani anatokea Vatican City.Tuwe makini jamani tukiandika k2 tusome kwanza kabla ya Public.
 
Back
Top Bottom