Wapi AshaDii?

Status
Not open for further replies.
Wataka tena zabiiibu , umekumbuka utamuuuuu ....halohalo hata kama umetubu kukupatena haramu........halooooooo nimeipenda hii

Abdallah Issa Leo tena! hii nyimbo alijibiwa na Bi malika enzi hizo

isikilize

 
Last edited by a moderator:
Boss and Kaizer

pata mashairi kwanza ....audio will be with you shortly

Rabi sinipe mapenzi, hakuna wakuamini
Wapendwa wenye ujuzi, ni wachache duniyani
Pendo la kisikuhizi, kuhadaana nyoyoni
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.

Niwingi udanganyifu, kweli hakuna nyoyoni
Ambao wathibitifu, ni tabu kuwabaini
Kitu nnacho khofu, kuja vunjiwa thamani
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.

Wanaopenda wapende, mimi siye asilani
Nimejitowa upande, singii mwao kundini
Moyo nimepiga konde, siwezi kutamani
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.

Nimefunga moyo wangu, usinitie taabuni
Kuteswa na walimwengu, wasojuwa pendo ni nini
Haiwi fakhari kwangu, kujinasa mtegoni
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.

Gaijin,

nimekukubali!!..................... siku zote nilikujua kama mwalimu hapa jamvini, ...................... ila sikujua kama uko deep kiasi hiki kwa mambo ya mwambao!!.................. big up saaaanaaaaaaaa...............................
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom