Wapenzi wa Yanga na Simba acheni kuvaa fulana za timu zetu wiki nzima

Mars 12

JF-Expert Member
Feb 25, 2021
221
349
Wapenzi wa Yanga na Simba, Jezi zenu huwa zinavaliwa angalau siku moja kabla ya mechi,hadi siku ya mechi na baada ya mechi unaweza ukavaa kwa nusu siku hata kama umeshinda au umefungwa.Ushamba wenyewe unakuwa hivi aliyeshinda anavaa jezi wiki nzima asubuhi hadi wengine wanalala nazo,wakati aliyeshindwa havai kabisa.

Hata akienda kazini jezi anayo,akienda kwenye starehe hivo hivo wengine mpaka sehemu za sehemu za ibada.Ningeomba akina Alli Mayai angalau wawafahamishe hawa wapenzi wa hizi timu kubwa kiushabiki lakini mbumbumbu kwenye mapato.Ni aibu hata timu moja kushindwa kujiendesha hadi waje akina rostam,manji,GSM,dewji na wengineo.

USHINDANI WA JADI UPO MISRI ALAHLY NA ZAMALEK,upo South africa Orlando Pirayes na Kaizer Chief,upo Ghana Asante kotoko na Hearts of Oak,Upo Tunisia Esperance na Alafricana,upo Sudan Almerreikh na Alahly Khartoum n.k lakini wote hawa wana viwanja vyao na vyanzo vya mapato.Pia wanauza wachezaji wengi tu Ulaya na China.Simba na Yanga acheni ushamba.mnatutia aibu nje ya nchi.
 
Kwanini unalazimisha Simba na Yanga ziwe kama wao?

Yaani unapangia watu namna ya kuishi wafanye wao uaibike wew?

Kila nafsi ifanye jambo kwaajili ya kujipa furaha yenyewe sio kwa ajili ya kuifanya nafsi nyingine ifurahi jambo la msingi usivunje sheria.

Kunywa maji ya kutosha huo muda unaotumia kufwatilia watu wamevaaje uutumie kwenda kukojoa mara kwa mara.
 
Back
Top Bottom