Wapenzi wa ndondi, kipindi bondia Tyson bingwa wa dunia kulikuwa na mapambano ya utangulizi kabla ya pambano lake!!?

HOPEfull

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,732
2,082
Tunapomalizia weekend jamani salamu🙁

Kichwa cha habari kinajieza.Huyu jamaa au mbabe wa ndondi enzi hizo ilikuwa akiingia tu basi anatoa klebu moja tu kwa mpinzani wake tena dakika ya kwanza tu na pambano linakuwa limeisha.

Sasa mi naona watu au mashabiki walikuwa wanaliwa tu hela ya bure maana walikuwa hawapati burudani..

Sasa je kulikuwa na mapambano ya utangulizi kabla ya pambano lake?? Huyu jamaa alikuwa hataki masihara na mtu.

One klebu one down.

Bondia Bingwa mwingine kabla ya Tyson anaitwa Mohamed Ali.Huyu alikuwa anawapeleka taratibu wapinzani wake hadi roundi ya nane huko wakichoka tu anaanza kuwapelea Moto mpaka wanaona dunia chungu na kuamua kusalimu amri😁.Huyu mbabe Ali angalaau mtu ulikuwa unapata burudani kidogo ya ndondi.Lakini sio Tyson,
Sijui alikuwa na misuli gani Huyu jamaa.😶

Usiku mwema.
 
Ndio yalikuwepo, pambano la utangulizi lililokuwa linanivutia zaidi ni la mwanadada Laila Ali bint wa Mo Ali
 
Back
Top Bottom