wapangaji kuanza kulipa VAT

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,907
3,261
kuna tetesi kuwa wapangaji wote wa jijini dar wataanza kulipia VAT katika pango la nyumba, wadau hii ikoje?
 
Ni wazo zuri. Serikali huendeshwa kwa kodi. Lakini kwa uhakika pesa zitapotea kwa makarani wakusanyaji. Sijui modality gani gani itatumika kukusanya mapato haya. SSN hamna, sijui watatumia wajumbe wa nyumba 10 10?
Ni mzigo mwingine kwa walalahoi wa nchi hii. Wataopitisha sheria hii wao wanakaa kwenye majumba ya serikali, nani atalipa kodi yao?
 
Kuna maeneo meengi sana ambayo serikali inatakiwa kupata pesa (hilo ni mojawapo na huko nyuma i.e. bcs nilishalizungumzia).......tatizo ni kuwa hizo pesa zinatumikaje.........kweli inaudhi sana
 
Huku uswahilini kwetu hizo gharama za umeme+maji+kufagia=VAT,sasa hiyo VAT wakiileta itakuwaje?2oneeni huruma jamani,tunakubali tumekuja mjini kimakosa,tuvumilieni karibu tutarudi kwetu jamani!!!!
 
kuna tetesi kuwa wapangaji wote wa jijini dar wataanza kulipia VAT katika pango la nyumba, wadau hii ikoje?

Kwanini wapangaji ni si wapangishaji? Waanze kwanza wao wenyewe wenye majumba ya kupangisha zaidi ya tano sehemu nzuri nzuri Dar. Kuwapiga VAT wapangaji ni uonevu mtupu!!
 
Kwa sababu ni tetesi yaweza kuwa si kweli. Nevertheless, is stupid to introduce VAT tax to renters. I would agree if they introduce council tax. However, council tax has to reflect the social economic services they provide to the community for instance provision of sufficient gabbage collection equipments and vehicles, timely collection of gabbages to each household, provison and maintanance of sustainable seawage systems, etc. As longer as the council is doing nothing to the community it ought to serve, the proposed tax is nonesense.

I submit
 
Hii kodi ndo ya kumlipia Sita 10m kodi ya Pango kwa mwezi?

Mkuu sasa ukiwa na misukule yako unaifanyaje? Unainyonya tu hata ikibidi kukauka kama ukuni wa mpingo!

Ni wazo zuri sana na labda litasaidia watu kujua kwamba wanalipa kodi kwani hizi zinazopitia kwenye bidhaa wengi hawana habari kama wanazilipa. Ila serikali ingefanya jambo la maana kama ingerudisha na ile kodi ya kichwa. Serikali inakosa pesa wakati watu wanasumbua mtaani, lazima ibuni mbinu za kuongeza mapato. Hapo viongozi wetu watakuwa wabunifu kweli!:rolleyes::confused:
 
Ni wazo zuri lakini waanzie kwenye makazi ya 'High Class' labda huko watapata kodi ya maana.

Kwetu uswazi masuala ya pango ni 'informal sector' na TRA mkitufuata mtapigwa mawe!
 
Ni wazo zuri kama tu kutakuwepo na udhibiti maalumu wa zoezi zima pamoja na bei za nyumba zenyewe.Kwa maana mpaka sasa kila mwenye nyumba ana sheria yake mwenyewe kuhusu nyumba yake.Hata akilala akiota kuongeza bei basi keshoye asubuhi kodi inapanda.Na hata hao Madalali ndo hawafai kabisa(wengi matapeli).Labda nao wangekuwa wanatambulika kisheria na wabanwe vilevile.Vinginevyo ni Disaster nyingine kwa Wananchi wengi hasa Mijini kama Dar es salaam.
 
Wanatafuta vita na kuvugika amani nchini kwa kuwa wao wameshakata tamaa na mambo waliyoifanyia nchi hii. Huwezi kumlipa mtu mshahara wa 18m kwa mwezi na kisha mtu huyo asiseme piga kodi wapangaji. Kwa kuwa hata hivyo kula kunywa hadi kunya analipiwa na serikali kwa payee zetu na vat zetu na kodi mshenzi zetu. I mean huu ni ufedhuli. Tanzania na pawepo na vita dhidi ya mafisadi. Amina.
 
Kodi gani tena hiyo?. Ukisoma vizuri Bajeti ya 2009/2010. hakuna jipya zaidi ya ile withhold Tax na ile 20% VAT ambayo sasa imekuwa 18% VAT.
 
Jamani mimi naona waweke kodi kwa wenye nyumba sio wapangaji.....kama kodi 1.8m akatwe 18 percent awape serikali maana wanapandisha tuu kodiiiiii hawaulizwi wala hawalipi kodi....
 
usijali mkuu,hizo pesa tutatumia kukujengea barabara na mashule,tunaomba ujitahidi kulipa usikwepe hiyo kodi kwa sababu tutakufunga
 
Back
Top Bottom