Wapalestina Gaza wagaragazwa wenzao wanaangalia tu. Huu ni unyama

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,183
10,921
Inashangaza sana kuwa binadamu sasa wamekuwa na roho za kinyama sana kwa sababu wanyama ndio ambao mwenzao akiliwa wanakuwa na msaada mdogo sana japokuwa kwa umoja wao wangeamua wangeweza kumuokoa.

Kinachotokea Gaza kinalingana sana na unyama.Kiwango cha vifo vya wapalestina na kujeruhiwa ni kikubwa sana na huenda haijawahi kutokea katika dunia tangu kuumbwa kwake.Kule Hiroshima na Nagasaki wajapani walikufa wengi kwa mpigo lakini kutokana na aina ya silaha iliyotumika hata watu hawakuona mateso yale kiasi kwamba wangelaumiwa kwa kutokutoa msaada kwa wenzao.

Pale Gaza hali ni tofauti sana kwani Israel ni taifa lenye silaha nyingi za kisasa ikipigana na Hamas ambao ni wanamgambo silaha yao kubwa ikiwa ni RPG na makombora yanayoruka hewani kwa mfumo wa kizamani.Silaha nyengine inayowasaidia na kuwasukuma mbele Hamas ni kujua madhila yaliyowakuta wazazi wao na wenyewe ambayo wameona hakuna njia nyengine isipokuwa ni kufa huku wakijitetea badala ya kufa kitandani.

Muhimu tunachokizungumzia hapa ni vile ambavyo Israel inapiga na kuua na kujeruhi wanawake na watoto mpaka wagonjwa na kuvunja majumba yao waliyojenga kwa shida.

Wengine waliobaki hai mwanzoni walitakiwa wahamie kusini,maskini wengi wakatiii amri hiyo,lakini hii ilikuwa kama kuwacheleweshea adhabu zao au kuwapunguzia kwa wakati huo kwani hawakuwachwa huru moja kwa moja kutokana na mashambulizi hayo.

Baada ya muda sasa Israel imekuja kusini na kuwataka hata wale walio katikati nao wazidi kuelekea kusini mpakani na Misri.Maskini wapalestina wa rika zote wametii japo haikuwasaidia chochote kwani makombora yanaendelea kupigwa na kuuliwa kwa idadi kubwa kila siku.

Watu waliokuwa na utajiri na familia zao mara wanajikuta wamebaki wapweke na hata mikoba ya akiba zao imewapotea na wanajikuta omba omba na waokotaji kwenye magofu ili wapate cha kula bila kuchagua ubora.
Katika hali hiyo ya kusongamana kwenye kambi za wakimbizi au kwa ndugu waliobaki na majumba bado wapalesina hao wanatakiwa hapo walipo waende mashariki au magharibi ili itoe nafasi ya kuvurugwa muda mfupi ujao.kwa kisingizio kuwa hapo walipo kuna Hamas.Maskini wote wanatii na kukimbia bila kutaka kufanya mjadala kuwa hawajawaona hao Hamas.Wanafanya hivyo kwa kujua kuwa ikisemwa hivyo kinachofuata ni makombora ya kusambaratisha kila kitu.

Wakipata amri kama hizo ama kwa vipeperushi au namna nyengineyo wapalestina hukimbizana kwa miguu au kwa gari za punda ambazo wachache wamebaki nazo. Hata hivyo wale wanaochelewa kidogo hupatikana viungo vyao tu vilivyotapakaa baada ya kufa kwa mabomu.

Muhimu zaidi tunachotaka kukieleza ni kuwa huo ukatili unaofanyika unafanywa mbele ya macho ya walimwengu wote wa makabila na dini zote. Ukiondoa hisia za kidini basi kiubinadamu tu basi isingepaswa kufanyika mbele ya binadamu wengine.

Kama ni lawama basi tukisema tulaumu hizo lawama zitaanza kwa watu wenye imani moja na wapalestina ambayo ni uislamu na ambayo ni dini karibu ya raia wote wanaoizunguka Palestina na Israel kwa ujumla.Hiyo ndiyo dini ya viongozi wa nchi hizo.

Matendo ya kuuliwa na kuchomewa majumba waislamu wala hayapo na hayajaanza Palestina na Gaza yake pekee.Hayo yamefanyika sana India,Myamar na China.Japo kuna mengi yangeweza kufanyika kuokoa hali zile lalini kule yawezekana ikasemwa ni mbali na hata hayakuwa yakioneshwa wazi wazi.

Haya yanayofanyika Gaza katikati ya ndugu zao na bila kuchukua hatua yoyote ile hakuna namna ya kuyaelezea isipokuwa ni unyama ambao umeingia ndani ya mioyo ya binadamu.

Kuna wenye nyoyo za kinyama ambao wanaweza wakaleta maneno ya kejeli kwa kisingizio kuwa piga Hamas haoo! eti kwa vile walishambulia oktoba 7.Ukiondoa hisia za kinyama na mtuj akabaki na ubindadamu wake basi kwa kuangalia historia hakuna sababu ya kuilaumu Hamas kwa kushambulia na wala haipasi kuwalaumu kwa kutokuwa tayari kusalimu amri.

Lawama kubwa itabaki kwa unyama ulioingia ndani ya nyoyo za binadamu wa karne hizi zinazokariibiana na kiama.Kwa hali hiyo kama litatokea la kutokea kwa unyama wa binadamu basi asilaumu hali ya tabia nchi wala nini isipokuwa abaki kujutia na kulaumu nafisi yake aliyoibadilisha na kuwa ya kinyama.

1701753261405.png
1701753282825.png
1701753300840.png
1701753314977.png
1701753395118.png
1701753418810.png
1701753445570.png
1701753462615.png
 
Attachments

  • 1701753300840.png
    1701753300840.png
    18 KB · Views: 3
Inashangaza sana kuwa binadamu sasa wamekuwa na roho za kinyama sana kwa sababu wanyama ndio ambao mwenzao akiliwa wanakuwa na msaada mdogo sana japokuwa kwa umoja wao wangeamua wangeweza kumuokoa.

Kinachotokea Gaza kinalingana sana na unyama.Kiwango cha vifo vya wapalestina na kujeruhiwa ni kikubwa sana na huenda haijawahi kutokea katika dunia tangu kuumbwa kwake.Kule Hiroshima na Nagasaki wajapani walikufa wengi kwa mpigo lakini kutokana na aina ya silaha iliyotumika hata watu hawakuona mateso yale kiasi kwamba wangelaumiwa kwa kutokutoa msaada kwa wenzao.

Pale Gaza hali ni tofauti sana kwani Israel ni taifa lenye silaha nyingi za kisasa ikipigana na Hamas ambao ni wanamgambo silaha yao kubwa ikiwa ni RPG na makombora yanayoruka hewani kwa mfumo wa kizamani.Silaha nyengine inayowasaidia na kuwasukuma mbele Hamas ni kujua madhila yaliyowakuta wazazi wao na wenyewe ambayo wameona hakuna njia nyengine isipokuwa ni kufa huku wakijitetea badala ya kufa kitandani.

Muhimu tunachokizungumzia hapa ni vile ambavyo Israel inapiga na kuua na kujeruhi wanawake na watoto mpaka wagonjwa na kuvunja majumba yao waliyojenga kwa shida.

Wengine waliobaki hai mwanzoni walitakiwa wahamie kusini,maskini wengi wakatiii amri hiyo,lakini hii ilikuwa kama kuwacheleweshea adhabu zao au kuwapunguzia kwa wakati huo kwani hawakuwachwa huru moja kwa moja kutokana na mashambulizi hayo.

Baada ya muda sasa Israel imekuja kusini na kuwataka hata wale walio katikati nao wazidi kuelekea kusini mpakani na Misri.Maskini wapalestina wa rika zote wametii japo haikuwasaidia chochote kwani makombora yanaendelea kupigwa na kuuliwa kwa idadi kubwa kila siku.

Watu waliokuwa na utajiri na familia zao mara wanajikuta wamebaki wapweke na hata mikoba ya akiba zao imewapotea na wanajikuta omba omba na waokotaji kwenye magofu ili wapate cha kula bila kuchagua ubora.
Katika hali hiyo ya kusongamana kwenye kambi za wakimbizi au kwa ndugu waliobaki na majumba bado wapalesina hao wanatakiwa hapo walipo waende mashariki au magharibi ili itoe nafasi ya kuvurugwa muda mfupi ujao.kwa kisingizio kuwa hapo walipo kuna Hamas.Maskini wote wanatii na kukimbia bila kutaka kufanya mjadala kuwa hawajawaona hao Hamas.Wanafanya hivyo kwa kujua kuwa ikisemwa hivyo kinachofuata ni makombora ya kusambaratisha kila kitu.

Wakipata amri kama hizo ama kwa vipeperushi au namna nyengineyo wapalestina hukimbizana kwa miguu au kwa gari za punda ambazo wachache wamebaki nazo. Hata hivyo wale wanaochelewa kidogo hupatikana viungo vyao tu vilivyotapakaa baada ya kufa kwa mabomu.

Muhimu zaidi tunachotaka kukieleza ni kuwa huo ukatili unaofanyika unafanywa mbele ya macho ya walimwengu wote wa makabila na dini zote.Ukiondoa hisia za kidini basi kiubinadamu tu basi isingepaswa kufanyika mbele ya binadamu wengine.

Kama ni lawama basi tukisema tulaumu hizo lawama zitaanza kwa watu wenye imani moja na wapalestina ambayo ni uislamu na ambayo ni dini karibu ya raia wote wanaoizunguka Palestina na Israel kwa ujumla.Hiyo ndiyo dini ya viongozi wa nchi hizo.

Matendo ya kuuliwa na kuchomewa majumba waislamu wala hayapo na hayajaanza Palestina na Gaza yake pekee.Hayo yamefanyika sana India,Myamar na China.Japo kuna mengi yangeweza kufanyika kuokoa hali zile lalini kule yawezekana ikasemwa ni mbali na hata hayakuwa yakioneshwa wazi wazi.

Haya yanayofanyika Gaza katikati ya ndugu zao na bila kuchukua hatua yoyote ile hakuna namna ya kuyaelezea isipokuwa ni unyama ambao umeingia ndani ya mioyo ya binadamu.

Kuna wenye nyoyo za kinyama ambao wanaweza wakaleta maneno ya kejeli kwa kisingizio kuwa piga Hamas haoo! eti kwa vile walishambulia oktoba 7.Ukiondoa hisia za kinyama na kuangalia historia hakuna sababu ya kuilaumu Hamas kwa kushambuli na wala kwa kutokuwa tayari kusalimu amri.

Lawama kubwa itabaki kwa unyama ulioingia ndani ya nyoyo za binadamu wa karne hizi zinazokariibiana na kiama.Kwa hli hiyo kama litatokea la kutokea kwa unyama wa binadamu basi asilaumu hali ya tabia nchi wa la nini isipokuwa abaki kujutia na kulaumu nafisi yake aliyoibadilisha na kuwa ya kinyama.

View attachment 2833477 View attachment 2833479 View attachment 2833489 View attachment 2833481 View attachment 2833485 View attachment 2833487 View attachment 2833488 View attachment 2833491
ulisema Idf inapata kipigo huko Gaza , imekuwaje tena useme wao ndo wanaonea hamas?
 
Juzi tu tuliwaambia kuwa mtaanza kulialia tena. Israeli akisitisha mapigano mara mnasema ameshindwa vita. Aise ninyi hamna jema kabisa.
Unashindwa kupata mantiki ya maandiko kama haya.Hatupo kwa ajili ya kulia lia kama unavyodhani.
Hii habari unahusu ubinadamu na unyama
Tukishindwa kuonesha ubinadamu wetu basi tunaweza kugeuzwa wanyama kabisa na si sisi tu bali na nyinyi pia mtaumia au tuseme tutadhurika sote kwa pamoja.
 
Mnatuchanganya Sasa kwanini mnabadilisha taarifa mnazotupa, msema majeshi ya Israel yanaisha huko Gaza halafu hapohapo mnatuambia wapalestina "wanagaragazwa" tushike lipi?
Tunakupa ushahidi uone kinachotokea sasa na kinatisha uje ung'amue kwa nini kitakachotokea huko mbele ya safari itakuwa ni machumo ya hiki tunachokishuhudia sasa.
Ingekuwa IDF tunaona wakiwagaragaza Hamas basi tusingekuwa na maneno mengi.Lakini kugaragaza raia na watoto lazima itasemwa na athari itatokea,
 
Inashangaza sana kuwa binadamu sasa wamekuwa na roho za kinyama sana kwa sababu wanyama ndio ambao mwenzao akiliwa wanakuwa na msaada mdogo sana japokuwa kwa umoja wao wangeamua wangeweza kumuokoa.

Kinachotokea Gaza kinalingana sana na unyama.Kiwango cha vifo vya wapalestina na kujeruhiwa ni kikubwa sana na huenda haijawahi kutokea katika dunia tangu kuumbwa kwake.Kule Hiroshima na Nagasaki wajapani walikufa wengi kwa mpigo lakini kutokana na aina ya silaha iliyotumika hata watu hawakuona mateso yale kiasi kwamba wangelaumiwa kwa kutokutoa msaada kwa wenzao.

Pale Gaza hali ni tofauti sana kwani Israel ni taifa lenye silaha nyingi za kisasa ikipigana na Hamas ambao ni wanamgambo silaha yao kubwa ikiwa ni RPG na makombora yanayoruka hewani kwa mfumo wa kizamani.Silaha nyengine inayowasaidia na kuwasukuma mbele Hamas ni kujua madhila yaliyowakuta wazazi wao na wenyewe ambayo wameona hakuna njia nyengine isipokuwa ni kufa huku wakijitetea badala ya kufa kitandani.

Muhimu tunachokizungumzia hapa ni vile ambavyo Israel inapiga na kuua na kujeruhi wanawake na watoto mpaka wagonjwa na kuvunja majumba yao waliyojenga kwa shida.

Wengine waliobaki hai mwanzoni walitakiwa wahamie kusini,maskini wengi wakatiii amri hiyo,lakini hii ilikuwa kama kuwacheleweshea adhabu zao au kuwapunguzia kwa wakati huo kwani hawakuwachwa huru moja kwa moja kutokana na mashambulizi hayo.

Baada ya muda sasa Israel imekuja kusini na kuwataka hata wale walio katikati nao wazidi kuelekea kusini mpakani na Misri.Maskini wapalestina wa rika zote wametii japo haikuwasaidia chochote kwani makombora yanaendelea kupigwa na kuuliwa kwa idadi kubwa kila siku.

Watu waliokuwa na utajiri na familia zao mara wanajikuta wamebaki wapweke na hata mikoba ya akiba zao imewapotea na wanajikuta omba omba na waokotaji kwenye magofu ili wapate cha kula bila kuchagua ubora.
Katika hali hiyo ya kusongamana kwenye kambi za wakimbizi au kwa ndugu waliobaki na majumba bado wapalesina hao wanatakiwa hapo walipo waende mashariki au magharibi ili itoe nafasi ya kuvurugwa muda mfupi ujao.kwa kisingizio kuwa hapo walipo kuna Hamas.Maskini wote wanatii na kukimbia bila kutaka kufanya mjadala kuwa hawajawaona hao Hamas.Wanafanya hivyo kwa kujua kuwa ikisemwa hivyo kinachofuata ni makombora ya kusambaratisha kila kitu.

Wakipata amri kama hizo ama kwa vipeperushi au namna nyengineyo wapalestina hukimbizana kwa miguu au kwa gari za punda ambazo wachache wamebaki nazo. Hata hivyo wale wanaochelewa kidogo hupatikana viungo vyao tu vilivyotapakaa baada ya kufa kwa mabomu.

Muhimu zaidi tunachotaka kukieleza ni kuwa huo ukatili unaofanyika unafanywa mbele ya macho ya walimwengu wote wa makabila na dini zote.Ukiondoa hisia za kidini basi kiubinadamu tu basi isingepaswa kufanyika mbele ya binadamu wengine.

Kama ni lawama basi tukisema tulaumu hizo lawama zitaanza kwa watu wenye imani moja na wapalestina ambayo ni uislamu na ambayo ni dini karibu ya raia wote wanaoizunguka Palestina na Israel kwa ujumla.Hiyo ndiyo dini ya viongozi wa nchi hizo.

Matendo ya kuuliwa na kuchomewa majumba waislamu wala hayapo na hayajaanza Palestina na Gaza yake pekee.Hayo yamefanyika sana India,Myamar na China.Japo kuna mengi yangeweza kufanyika kuokoa hali zile lalini kule yawezekana ikasemwa ni mbali na hata hayakuwa yakioneshwa wazi wazi.

Haya yanayofanyika Gaza katikati ya ndugu zao na bila kuchukua hatua yoyote ile hakuna namna ya kuyaelezea isipokuwa ni unyama ambao umeingia ndani ya mioyo ya binadamu.

Kuna wenye nyoyo za kinyama ambao wanaweza wakaleta maneno ya kejeli kwa kisingizio kuwa piga Hamas haoo! eti kwa vile walishambulia oktoba 7.Ukiondoa hisia za kinyama na kuangalia historia hakuna sababu ya kuilaumu Hamas kwa kushambuli na wala kwa kutokuwa tayari kusalimu amri.

Lawama kubwa itabaki kwa unyama ulioingia ndani ya nyoyo za binadamu wa karne hizi zinazokariibiana na kiama.Kwa hli hiyo kama litatokea la kutokea kwa unyama wa binadamu basi asilaumu hali ya tabia nchi wa la nini isipokuwa abaki kujutia na kulaumu nafisi yake aliyoibadilisha na kuwa ya kinyama.

View attachment 2833477 View attachment 2833479 View attachment 2833489 View attachment 2833481 View attachment 2833485 View attachment 2833487 View attachment 2833488 View attachment 2833491
UNATUCHANGANYA SANA ALWAZ. HATUELEWI TUSHIKE LIPI TUACHE LIPI. JUZI TU ULISEMA ISRAEL IMESHINDWA IMEPATA KIPIGO CHA KUFA MTU. TUKASHANGILIA SANA NA MIMI NIKAFURAHI. LEO TENA UNASEMA WAPALESTINA WANAGARAGAZWA.... AU ULITAKA SEMA WAISRAEL WANAGARAGAZWA HUKO PALESTINE /GAZA?
 
Tunakupa ushahidi uone kinachotokea sasa na kinatisha uje ung'amue kwa nini kitakachotokea huko mbele ya safari itakuwa ni machumo ya hiki tunachokishuhudia sasa.
Ingekuwa IDF tunaona wakiwagaragaza Hamas basi tusingekuwa na maneno mengi.Lakini kugaragaza raia na watoto lazima itasemwa na athari itatokea,
Hao wanaogaragazwa Ni Hamas, mamlaka ya Palestine hawawatenganishi hamas na raia wengine wa kawaida Kama Ni vifo wote wanatangazwa Kama raia wa Palestine. Na ndio maana Hata siku moja hatasikia mpiganaji yeyote wa hamas akiuawa anatagazwa isipokuwa kwa viongozi pekee.
 
Hamas ilishambulia Israel na kuteka Raia na mpaka sasa kuna raia wa Israel ambao wamebakia kama mateka mikononi kwa Hamas/Palestina na sioni ukilaani hilo.

Niseme tu, mpaka sasa Israel hana hatia yeyote juu ya damu ya wapalestina inayomwagika, na hata kama wapalestina wote watateketea hiyo damu itakuwa juu ya Hamas.

Uwezi ukashikilia raiya wa nchi fulani afu ukachekewa tu.

Wapalestina walitakiwa walitakiwa wajitenge na Hamas pamoja na kulaani kitendo cha Hamasi kuuwa na kuteka raiya wa Israel. Sasa kwa Kukaa kimya tafasiri yake ni moja tu HAMAS NA PALESTINA WANASHIRIKIANA
 
UNATUCHANGANYA SANA ALWAZ. HATUELEWI TUSHIKE LIPI TUACHE LIPI. JUZI TU ULISEMA ISRAEL IMESHINDWA IMEPATA KIPIGO CHA KUFA MTU. TUKASHANGILIA SANA NA MIMI NIKAFURAHI. LEO TENA UNASEMA WAPALESTINA WANAGARAGAZWA.... AU ULITAKA SEMA WAISRAEL WANAGARAGAZWA HUKO PALESTINE /GAZA?
Mwenye akili ya kibinadamu wala hachanganyikiwi.Kwa sasa tunazungumza habari ya hisia za kinyama.
Kama ni kipigo basi Israel haiwezi kukiepuka na kama hakikutolewa na binadamu na majirani zake basi kitatoka kwa yule ambaye pigo lake ni la ajabu na sio la ukatili kama ule wa Gaza.
 
Hii habari unahusu ubinadamu na unyama
Tukishindwa kuonesha ubinadamu wetu basi tunaweza kugeuzwa wanyama kabisa na si sisi tu bali na nyinyi pia mtaumia au tuseme tutadhurika sote kwa pamoja.
Mbona unyama wa kutisha ulianzishwa na hao hao Hamas 7/October ?

1701760292099.png

A teenage Israeli girl caught by HAMAS while trying to escape from the Nova music festival on October 7, hands tied, after being raped.

This is just one of the women who were raped and burned alive while their hands were tied.
 
Lawama kubwa itabaki kwa unyama ulioingia ndani ya nyoyo za binadamu wa karne hizi zinazokariibiana na kiama.Kwa hali hiyo kama litatokea la kutokea kwa unyama wa binadamu basi asilaumu hali ya tabia nchi wala nini isipokuwa abaki kujutia na kulaumu nafisi yake aliyoibadilisha na kuwa ya kinyama.
Halafu pata ufafanuzi hapa kuhusu kinachofanyika Gaza kwa sasa na umuhimu wake...
👇👇
 
Hamas ilishambulia Israel na kuteka Raia na mpaka sasa kuna raia wa Israel ambao wamebakia kama mateka mikononi kwa Hamas/Palestina na sioni ukilaani hilo.

Niseme tu, mpaka sasa Israel hana hatia yeyote juu ya damu ya wapalestina inayomwagika, na hata kama wapalestina wote watateketea hiyo damu itakuwa juu ya Hamas.

Uwezi ukashikilia raiya wa nchi fulani afu ukachekewa tu.

Wapalestina walitakiwa walitakiwa wajitenge na Hamas pamoja na kulaani kitendo cha Hamasi kuuwa na kuteka raiya wa Israel. Sasa kwa Kukaa kimya tafasiri yake ni moja tu HAMAS NA PALESTINA WANASHIRIKIANA
Kwa vile wapalestina wanaiona Hamas ndio mtetezi wao hakuna anayewalaumu hata akiona wanawe wamekufa,Kule ukanda wa mashariki ndio kwanza wameamini kuwa Hamas ndio wakombozi wao,Watu karibu 300 wangefia magerezani kama wenzao kama si Hamas kushikilia mateka wa Israel.
Hao mateka waliobaki Gaza ama watakufa nao au vyenginevyo lakini hawawezi kuwaachilia hivi hivi.Hawawezi kufaidika na chochote kwa kuwaachia kwao na masharti mepesi.Uzuri Hamas wanawajuwa mayahudi vizuri kwamba ni watu madhalimu,waliolaaniwa na wasioheshimu mikataba.
 
Tunakupa ushahidi uone kinachotokea sasa na kinatisha uje ung'amue kwa nini kitakachotokea huko mbele ya safari itakuwa ni machumo ya hiki tunachokishuhudia sasa.
Ingekuwa IDF tunaona wakiwagaragaza Hamas basi tusingekuwa na maneno mengi.Lakini kugaragaza raia na watoto lazima itasemwa na athari itatokea,

Juzi maustazi uchwara walikua wanashangilia wanajeshi zaidi ya elfu 3 wameangamia hapo Gaza. Shida nini sasa?
 
Vita vya so called Ugaidi haviwezi kushindwa kwa Mabavu kinachohitajika na Knowledge na kuonyesha kwamba Haki inatendeka....

Kinachoendelea sasa ni kuzalisha HAMAS wengine at an exponential level; KInachofanyika sasa its for detriment to the future world peace

Mbona JW ilifanikiwa kufukuza magaidi kule kibiti?!
 
Back
Top Bottom