Wanawake Wana drama hatari

Glenohumeral joint

JF-Expert Member
Oct 29, 2017
2,054
2,885
Salamu zenu jamani watu wa humu...habari za kazi zenu popote mlipo..mm ngoja niende moja kwa moja kwenye mada.

Kuna binti nimedumu nae ktk uhusiano kwa mwaka mmoja na Kama miezi miwili hvi,huyu binti ni mwanafunzi wa chuo,binti wa kinyaturu,mweupe ,mrefu na n mzuri hakika aisee...

Kipindi ninamtongoza huyu binti alkuwa first year chuo kimoja hapa dar enzi hzo mm pia nlkuwa chuo nasoma sema nlkuwa mbele yake kidogo,nakumbuka kipindi namtongoza aliniambia ametendwa Sana na mwanaume aliyekuwa naye tokea huko kwao singida,basi akawa anadai wanaume sio watu wazuri n.k..basi mm nikaendelea kukaza Uzi na kumsisitiza kuwa wanaume hatuko sawa,ikanichukua Kama wiki mbili hv ndio akanikubalia na mapenzi yakaanza...nakumbuka alinikubalia kuwa boyfriend wake na siku iliyofata alkuja getho kwangu kunitembelea na kwa vile ilkuwa weekend basi alikaa kuanzia ijumaa mpk jumapili humo ndani yakutokea yalitokea..wakat anaondoka nikampa nauli lkn alikataa na akasema yeye anayo nauli,bhc maisha yanaendelea huku nikijitahidi kwa dhati kabisa nisimuumize hata siku moja maana akilini mwangu nilijua mpenzi wangu anachuki na wanaume maana alishatendwa,basi mapenzi yakaendelea ikawa almost kila weekend mtoto lazma aje kwangu tuspend weekend Kama mnavojua Tena maisha ya chuo yalivyo kwa vijana wenye magetho mtaani.

Kiukweli tabia za huyu mnyaturu zilinipendeza Sana maana mtoto alionesha kunipenda kwa jinsi nilivyo,hakuwahi kuomba hela na nikimpa alikuwa anakataa na kusema "baby we pia unasoma so huna hela,muda ukifika utanipa tu baby"basi mm akili yote ikampenda nakuona wife material ndio huyu,hata alipokuwa akija getho kwangu aliniletea mboga Kama samaki,matunda n.k..kiukweli nikatokea kuzipenda tabia za binti kiasi Cha kuanza kumtambulisha kwa Kaka zangu na marafiki zangu wa karbu maana sikuona kinachoweza kufanya nisimuoe huyu binti.Nakumbuka Kuna kipindi mama yangu alkuwa mgonjwa na sikuwa na hela,huyu binti aliniomba namba ya mama amtumie hela ili aende hospital,n kweli alituma,Jambo hili likanifanya nimpende zaidi kupita kawaida.

Kwa vile nikimpa hela alkuwa anakataa basi nikabuni mbinu ya kumpa pesa kwa njia ya zawadi,nikawa nanunua vtu vidogo mfano viatu,nguo,n.k basi tu namm nionekane najali..na yy pia alinipa zawadi Kama tisheti,Mara aniletee mashuka mapya ,Mara mafuta ya alizeti tokea kwao singida yaan yote hayo yalinifanya nikambwagia moyo wangu wote huyu binti wa kinyaturu na sikujua yaliyokuwa nyuma ya pazia.

Tulipanga mipango mingi Sana ya maisha kiasi nikikumbuka Sasa roho inauma kabisa,bhc bhn ukapita mwaka wa mahusiano yetu na Sasa binti akapata likizo ya kwenda kwao singida Kama kawaida alilala kwangu namm ndio ninamsindikiza kwenda ubungo likizo zote,so nikafanya ilivyonipasa.

Alivyokuwa likizo huko kwao Mambo yalianza kubadilika kiasi nikagundua...mawasiliano yakapungua,ukimuuliza anakwambia Yuko bze Sana na shughuli za nyumbani maana kwao n Kijijini so mm sikuwa na Shaka Sana maana nilijua Yuko kwa mzazi sehemu salama.

Likizo ilipoisha ilkuwa mwezi wa kumi mwaka huu akaja dar namm nilikuwa getho Kama kawaida sema mm nikawa nishamaliza chuo,nipo tu napiga mishe kidogokidogo za mjini kujipatia riziki...nikaenda kumpokea ubungo na tukaja kwangu Ila nikagundua Kuna kitu kimechenji,huyu binti hakutaka niishike simu yake hata kidogo na alinikataza kuwa hapendi hayo Mambo,Jambo ambalo n tofauti na alivyokuwa zamani.

Basi mm nikaamua kuacha kumfatilia Sana ila alipoondoka kwenda chuo akabadilika kabisa,sms hajibu on time Kama zaman na sometimes hajibu kabisa,ukimuuliza anasema n ubize wa masomo bhc sikuwa na namna,nikamvumilia tu...

Kila nikimuomba aje kunitembelea alikataa na kusema Yuko bze na shule,ikapita miezi miwili bila yy kuja na hapa katikati mm nikaenda chuoni kwake Mara tatu kumuuliza shida n nn mbona amebadilika hvyo,lkn alisema hakuna shida na ananipe da Sana tu so nisijali Jambo vitendo vilionyesha Hali ya tofauti.

Basi siku moja Sina hili Wala lile nikaingia Facebook,nikashangaa kukuta Kuna mwanaume mmoja kashare kuwa Yuko in relationship ya huyu mwanamke wangu,nikashtuka Sana..baadae nikamuuliza nn kinaendelea Kati yao,akasema hamna bali huyo n x wake Yule aliyemuumiza moyo na huwa anamuomba msamaha Sana kuomba warudiane Ila yy amekataa...bhc mm sikurdhika ikabid nimzamie mchizi messenger anieleze vzuri about their relationship..ndio akafunguka kuwa Yule n mpenz wake na wameanza relationship kabla ya binti kuanza chuo na kashamtambumisha mpk kwa wazazi wake,kilichobaki niyeye binti kumaliza chuo na kuolewa na mchizi,daaaah niliishiwa nguvu ika sikuamini so nikadhani labda jamaa anajiproud tu maana nilimwambia huyu n mwanamke wangu na Nina mpango wa kumuoa,aisee akashangaa Sana..

Ndipo hapo akasema Kama simuamini kuwa binti ni wake na sio wangu ngoja ampigie simu aniunganishe namm ili niskie maongezi yao...kumbuka usiku wa siku hii ndio binti alilala kwangu na akaondoka jioni...jioni hii ndio huyu jamaa yake akaniunganisha kwenye simu ya maongezi yao,kiukweli ndipo niligundua kuwa wametoka mbali kweli na jamaa akamuuliza kuhusu habar zangu,sikuamini niliposkia binti huyu akisema mm ni x wake na tulishaachana muda mrefu wakati usiku wa siku hiyo amelala namm...

Niliumia Sana moyo,ndipo binti akaamua kuniambia kuwa alinidanganya aliposema Hana mpenzi Bali mpenz anaye na nyumbani wanamfahamu na kilichobaki n ndoa,so akasema mapenz namm hataki Tena na akamuomba msamaha huyo bwana wake kwa kitendo Cha kumsaliti kwa kulala namm kwa muda wa mwaka mzima wote aliokuwa akidate namm,jamaa amemsamehe na mapenz yanaendelea kama kawaida...mm ndio nmebaki solemba,kila nikiwaza najikuta naumia Sana yaan Sina hamu kabisa na wanawake tena.


Samahan Kama nmewachosha kwa kuandika maelezo marefu....kuna mengi sijayaandika ila kwa haya machache nmependa kuwashirikisha.

Muwe na wakati mwema sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
============
Mchango
Hapa kuna scenario mbili huenda kweli alikupenda kwa dhati lakini alikua tayari kasha saini mkataba kwa huyo jamaa na price ya kuuvunja huo mkataba (kumuacha jamaa ili aje kwako) hana. Kumbuka kua women wana time factor while sisi tuna financial a.k.a ndululu factor

Scenario nyingine ni huenda alikua anataka zima moto ile ya kupunguziana uzito unfortunately mkuu ukawa serious sana wakati yeye hakua hata na mawazo kama yako.

In every decision you make there is a price to pay, hii ni twisheni umeipitia kwa sababu ume fall in love kiboya. Next time kua makini, Never expect anything from any one especially wanawake kwa sababu they always think about shortcut au njia rahisi ya kutatua jambo itakayokuja kwa wakati huo ndio maana wanawake (asilimia kubwa) wapo radhi watembee hata na mizee (mfano vyuoni) ili tu wafaulu mitihani au wapate pesa za kujikimu.

Kwenye moja ya movie zake marehemu Kanumba aliwahi kusema
Never trust a woman or a disability dog.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu,
How I feel you.!!
Mtu unaweza dhani umeumizwa lakini ukiyaskia ya mwenzio unamshukuru Mungu, sababu wewe umeguswa tu hata hujaumizwa.!

Ni ngumu ila jifunze kuukubali ukweli kuwa it was never meant to be, jaribu ku move on and keep in your mind that this too shall pass!

Hakuna lenye mwanzo lisilokuwa na mwisho, hata hayo maumivu yana mwisho ipo siku hutoyasikia tena, I am talking from a very deadly experience, Just be strong, be passionate with yourself moreover focus on being in the best version of yourself.!!

Siku zote kumbuka kuwa no matter how hard the situation you're passing through Maisha ni lazima yaendelee, na Muda hautosimama kukusubiri kuwa Glenohumeral joint yuko kule anaumia hawezi fanya chochote!! Never.!!

the only revenge right now is 'SUCCESS'..!!
 
Hivi ulikuwa unamtafuna kwa kutumia ndomu au ulikuwa unaloweka tu kipindi chote hicho cha mwaka mzima?

With that being said,,pole sana..it's really hurts kuachwa na mwanamke uliyekuwa unampenda.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuhusu HIV Hana maana tulikuja kupima baadae ktk mahusiano yetu,tatzo likizo alizokuwa anaenda alkuwa analiwa na huyo bwana wake so Kama anavirusi bhc hii ya juzi ndio atakuwa kaniambukiza,maana nilikuwa namuamin Sana hasa baada ya kupima so sikuona umuhimu wa Kinga Tena...

Asante lkn mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Historia inataka kufanana na yangu, ila naamin Mungu alikuwa upande wangu na daima siku zote nitamtumain yy na hakika amenipa mke mwema sana katika maisha yangu nilimpoteza mwanamke niliyempenda ambaye alinifanyia drama kama ya huyo wako ila nikaja kupata mke mwema n siyo mwanamke wa drama

Sent using Jamii Forums mobile app
Ameen....ngoja nipige konde nisonge mbele....haikuwa ridhiki yangu hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom