Wanawake, twawapenda sana, ila...!

Mtuvumilie jamani, sisi ndio maua ya ulimwengu. Tunataka usawa, kipaumbele na kipau nyuma kwa wakati mmoja, ili mradi vinilinde mimi na mslahi yangu kwanza.

Kumbe unaogopa eeee! umetoa avatar yako bisheshege! haya tuambie kisa cha kuweka picha ya mke mwenzako humu ni nini? hahahahahaaa. pole mamii
 
Da , inasikitisha sana pole wanaume wote mnaopitia hayo, na kwa asili mwanamme siyo mwepesi kuelezea matatizo ya ndani ya nyumba yake hadharani ukiona wanaume wanaeleza matatizo ya wake zao jf basi fahamu yamewafika shingoni.

Lakin baadhi ya mwanawake mwenye tabia hizo, unajisikiaje
usipoihudumia familia yako japo unawezeshwa na mumeo??
Unapowachukia ndugu wa mumeo hata kama wao wanakupenda??
Na kibaya zaidi unawachukia wazazi wa mumeo, waliomlea vizuri na kumpa elimu na mwelekeo mzuri wa maisha.
Hivi wazazi wako wakinyanyaswa na mumeo kama unavyowanyanyasa wewe wakwe zako utajisikiaje???

Mwanamke unapoolewa ondoa mtazamo kuwa ndugu wa mume ni wabaya siku zote,bali wachukulie kama hao ni sehemu ya familia yako. Hata wanapokukosea wasamehe kama wewe unavyosamehewa pindi unapokosea.lililo muhimu ni kufahamu kuwa unapoolewa unaenda kuungana na familia mpya,jaribu kuwasoma pia fahamu hao siyo malaika ni binadamu kama wewe wenye mapungufu na mazuri yao,tupendane na tuvumiliane.

Wanawake tukosoane,tusahihishane,tufundishane, pindi mwanamke mwenzetu anapoonesha tabia mbaya kwa mume,familia zao ,pia hata kwa familia ya mume, ili tuoneshe kwa vitendo kuwa sisi ni watu wenye hurumu na upendo.
Kabla haujamfanyia mtu mwingine kitendo kibaya jaribu kujiuliza je ukifanyiwa wewe hicho kitendo kibaya utajisikiaje??.

Ndoa kitu cha thamani sana ukijua na kufahamu thamani ya ndoa, pia fahamu siyo kila mtu anatimiza ndoto ya ndoa ,wewe uliyekifikia mtukuze /mshukuru mungu kwa kumtunza mumeo na familia yako kwa ujumla. Wengine mpaka mauti inawafikia pasipo kupata heshima ya ndoa japo sifa zoooote za kuolewa wanazo lakin wanapungukiwa na bahati ya kuolewa...mwanamke iombee ndoa yako kwa imani yako,iheshimu,ithamini,itunze,ilinde ili mumeo na familia yako wafurahi na kumshukuru mungu kwa kuwa na mama mwema.
 
Pole kaka kwa masaibu ya mke wa rafiki yako aliyekosa upendo hata kwa watoto wake. Ujue wanawake tumetofautiana na wengine huwa tunakosea na kufanya vitu tukidhani tunamkomoa mume kumbe tunabaki kuwaonea hata watu wasio kuwa na hatia. Mwambie huyo kaka asiishie kufanya tu shopping pia anatakiwa kuongea na mkewe na ajue shida iko wapi kufanyiwa vitu vyote hivyo na mume ni kushukuru, ulimwengu umeharibika kuna watu kwenye ndoa wanapangiana majukumu mpaka utashangaaa yote hiyo ni kwasababu ya mmoja kujikuta anafanya vyote lakini bado anakuwa kama anakomolewa!
 
Lol! Poleni sana waume zetu jamani, tuwekeni kwenye maombi hili ni pepo la ubinafsi, hivi kweli mtu aache 15,000 halafu usione hata haya umuwekee spinachi tu mezani na unaona poa tu! no, no, kama sio pepo basi ni kichaa, 15 mbona inatoa menu ya hatari jamani labda kama hiyo familia ni kubwa sana..
 
MIMI NAAMINI CHAKULA BORA ZAID ,SALAMA ZAID, CHENYE LADHA NZURI ZAID,CHENYE KUVUTIA ZAID, KINAPATIKANA NYUMBANI, NA SIYO HOTELINI WALA MGAHAWANI .SASA MWANAMKE UNAPOSHINDWA KUIANDALIA MENU BORA FAMILIA YAKO ,UNATAKA MUMEO / WATOTO WAKO WAKAIPATE WAPI HIYO MENU NZURI????!!!. NAOMBA NIELEWEKE VIZURI SINA MAANA KUWA HOTELINI,MGAHAWANI AU KWA MAMA NTILIE HAKUNA CHAKULA KIZURI,HATA HUKO KUNA CHAKULA KIZURI LAKIN PAMOJA NA UZURI WA HUKO, BADO HAKIWEZI KUZIDI UBORA WA CHAKULA KILICHOANDALIWA NA MAMA MAKINI, KSB HIKI CHA NYUMBANI KWA MFANO UNA UHAKIKA WA MAFUTA GANI UMEPIKIA?,VIUNGO GANI UMEUNGA,UMEPIKA SAA NGAPI, NA MENGINE MENGI MUHIMU....

KINA MAMA NAAMINI NA NAJUA MNA MAJUKUMU MENGI SANA (KIUCHUMI/KISIASA/KIJAMII) YANAYOWAKABILI LAKIN BADO NASISITIZA MJIBIDIISHE KUZITUNZA FAMILIA ZENU ILI MWANAUME AONE THAMANI NA UMUHIMU YA UWEPO WAKO. ASIWE NA MAWAZO MEEENGI YA KUKUMBUKA MSOSI WA MAMA YAKE MZAZI ALIOKUWA ANAUPATA KABLA HAJAOA...lol.
 
Wanawake wa aina hii huwa wanawavunja sana moyo waume zao, yaani hata watoto wake hawaonei huruma sababu ya tamaa zake tu zisizo na mbele wala nyuma
Blackbery , kuna thread mtu kakufungulia anasema kakuzimia,umeiona? mbona hujamfungulia moyo wako?
 
Hata watoto wake wakuwazaa mwenyewe?
Mmmmh, tumbo halimuumi, akiona wanavyokua vibaya, hawana afya ya kutosha.
Yani waishi wakila vibaya na kuvaa vibaya kikiwa hakipo, sio umeficha sijui wapi.
Khaaaaaaaaaaaaa, watoto wake wakiwa wakubwa wakisikia atakoma, vile watakavyo mchukia.
 
Back
Top Bottom