Wanawake, ni zipi changamoto za kuishi na mwanaume aliyesimamishwa kazi?

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,513
Husika na kichwa cha habari ..

Ninavyoandika hapa kuna mwanamke anapitia changamoto baada ya mumewe kusimamishwa kazi...

Anadai mumewe amekuwa mkali sana yaani kidogo tu anakasirika...

Amekuwa na wivu sio wa nji hii yaani hataki mkewe atoke na rafiki zake...

Amekuwa mlevi Ile hatari yaani ni mitungi yeye na mitungi mtu...

Mkewe anadai kuwa mumewe alikuwa hataki afanya kazi hapo nyuma...

Yaani alimuachisha kazi akawa mama wa nyumbani yaani goli kipa...

Sasa kimeumana, mumewe hana kazi na Wala hawana chanzo chochote cha pesa...

Imefika mwaka Sasa hamna kazi wamekopa na kukopa...

Sasa tumshauri huyu bidada, maana naona kama anadata...

Najua Kuna waliopitia haya wapo hapa watamshauri bidada.
 
Changamoto zipo tu kila siku na kukosa pesa au ajira ni sehemu ya changamoto na unapokutana na hali usiyoitarajia ichikulie kama fursa tu.

Mshauri huyo Bi Dada atafute ushauri na msaada wa Kisaikolojia. Maana anachokifanya Mume wake sio ufumbuzi au utatuzi wa hiyo changamoto
 
Husika na kichwa cha habari ..

Ninavyoandika hapa kuna mwanamke anapitia changamoto baada ya mumewe kusimamishwa kazi...

Anadai mumewe amekuwa mkali sana yaani kidogo tu anakasirika...
Pole Sana Kwa hizo changamoto Kwa ufupi katika kitu ambacho wanaume tunakutana nacho tukiwa hatuna kazi ni kupoteza ile uhakika au tumanini ndani ya MTU

Kama ana ndugu au Jamaa atafute WA kumsaidia Ila kama anaweza kuongea na marafiki wa Mume wake angalau wawe wanamtembelea na kumtia Moyo kutokana na hizo changamoto

Kwa mwanaume kupoteza kazi ni Sawa na kupoteza uanaume hivyo , kunaitaji Sana msaada wa Mungu katika ilo, pia usisahau kufanya na maombi pia

Kingine mshauri rafiki yako kutokuwa mbali na mumewe maana kuna kuwa na hisia labda anataka kumtelekeza au kuwa na mahusiano mengine, Mungu awatete katika hicho kipindi kigumu
 
Wewe ni me unazijua...

Weka hapa...
Nadhani umeanzisha mada ambayo umeomba majibu hivyo kama yeye naye ana dukuduku lake basi anaweza kuanzisha thread yake.

Back to the topic: ni kweli sisi wanaume tunapokuwa na changamoto ya kipato huwa hatujiamini na tunadhani kuwa wake zetu wanatudharau hata kwa jambo ambalo siyo. Njia sahihi ya mwanamke ku deal na hilo ni kumuonyesha upendo mumewe.

Aepuke kujibizana naye na kuwa jeuri na kama anamshauri jambo lolote atumie kauli laini na yenye upendo. Aepuke dharau au majibu ya dharau. Jambo jingine la muhimu sana ni kutopenda kutoka mara kwa mara na rafiki zake.
 
Kisiraniii....nyie nyie....au basi.
Mana mtu ananuna bila sababu, self esteem inashuka to zero. Yani hata ukimwambia naomba glass ya maji anakwambia kwahiyo umeanza kunidharau kwakua sina kazi, wakati mwanzo alikua hadi kupika na kufua anafanya.

Asikwambie mtu, mwanaume akikosa hela anachanganyikiwa had unamuonea huruma. Wanaume tafuteni hela ili matatizo ya afya ya akili yapungue mtaani.

Ni miaka miwili migumu kuwah kupitia maishan but namshukuru tulitoka salama life linasonga japo haikuwa rahisi kumrudisha kwenye normal state.
 
Hawezi kuanzisha mada, kifupi huyo bidada sio mtu wa mitandao...

Sasa amenyong'onyea mno...

Mi nikamdadisi ndo akawa analia huku anaongea...
Kuhusu kuanzisha mada: Nilikuwa namjibu yule member Father of All aliyeuliza ''Zipi changamoto za kuishi na mwanamke aliyeachishwa kazi?''. Nikamshauri aanzishe thread yake ili hii watu wachangie ulichouliza wewe.
 
Back
Top Bottom