Wanawake na mauongo yao ya saluni haya hapa….!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
wedd9.jpg


hair-salon.jpg


Kwenye Saluni nyingi za wanawake, mazungumzo mengi yanahusu maisha ya watu na hasa kuhusu mapenzi na kipato, kashfa na saikolojia zisizo rasmi kuhusu ndoa na uhusiano. Kuna mazungumzao ya kukatishana tamaa na kuumizana zaidi, kwa sababu kila mmoja anajaribu kuonyesha kwamba ana nafuu fulani.

Lakini mbaya zaidi ni kwamba, saluni za wanawake hutumiwa na wanawake hao kama maeneo ya kusemea hisia zao chungu na kutoa jumuisho kuhusu wanaume na uhusiano. Huko saluni hakuna wataalamu, bali kuna wazungumzaji ambao wanaamini wao ni wataalamu, na wengine kwa sababu ya kuzidiwa na mzigo wa matatizo hasa ya uhusiano na pengine ya kipato, huwaaamini hao wataalamu wasio rasmi.

Huko saluni ndiko ambako wanawake wanaambiana`kwamba, mwanaume akiacha kufanya tendo la ndoa kwa wiki moja na mpenzi wake, ni lazima mwanaume huyo atakuwa na ‘nyumba ndogo.' Ndiko ambako wanafundishana kwamba, ukipata Mganga wa nguvu unaweza kumshika mwanaume. Ndiko huko ambako hutajwa orodha ya wanawake ambao wamewashika waume zao kupitia kwa waganga. Ndiko huko ambako majina ya waganga maarufu hutajwa.

Lakini ndiko huko saluni ambako, wanawake hutaja orodha ya wanawake wenzao waliopata mali kupitia ‘mabuzi,' ambao huwapa mitaji ya biashara inayowawezesha kusafiri hadi Uchina. Pia hutajwa majina ya wanaume wanaohonga sana. Ni saluni ambako wataalamu wasio rasmi hutoa suluhu ya matatizo ya ndoa. Ndiko ambako wataalamu hao huwaambia wanawake wenzao kwamba, ukimuonyesha mwanaume kwamba unampenda sana, atakudharau na kukuacha.

Kwa hiyo mwanamke akitoka saluni anakuwa ametoka shule anayoiamini . ambapo huacha kumwonesha mumewe kwamba, anampenda. Ni wazi shule hii ya saluni haijui kwamba, unapoonesha kutokupenda, nawe utaoneshwa kutokupendwa. Kwani unachopanda ndicho unachovuna. Wakati mwingine shule hii inajua jambo hilo, isipokuwa inataka waliopotea na kuharibikiwa wawe wengi.

Ni huko saluni ambako utasikia wanawake wakifundishana namna ya kuwadanganya wanaume zao. Hufundishana namna ya kujenga nyumba bila kunaswa na mume, kwani wanaume hawaaminiki, huwezi kuacha kujiandaa. Lakini shule hii haijui kuwa, hiyo ni sumu kubwa kuliko sumu nyingine kwenye ndoa, kutafuta mali na kujenga msingi wa kipato kwa siri.

Ni hukohuko saluni ambako wanawake huambiana uongo kuhusu wakwe, watoto wa kambo, na mawifi. Hufundishana kwamba, kumpenda mama mkwe au wifi ama mtoto wa kambo ni kutafuta muhali. Haiishia hapo huendelea kufundishana hata namna ya kuwachukia watu hao.

Mwanaume, kama ukiona mwenzi wako anakwenda saluni na akitoka huko amekuwa mtu mwingine kabisa, unapaswa kujua kwamba, huenda amepata ‘dozi' ya wataalamu hao.

Wanawake, nawashauri jihadharini sana na maneno ya saluni. Kwani katika kila maneno mia moja, ni moja tu linalokaribia ukweli. Kumbuka, linalokaribia ukweli . siyo kuwa ni la kweli……
 
Kaka ni kweli kuwa kwenye saluni za kike kuna mambo sana.
Kuna kina dada wamefanya hivyo ndio vijiwe vyao vya kupiga soga zote za mambo mabaya.
 
Hapo naona Mtambuzi unachukia tu mwanamke kwenda saluni maana hata maofisini watu huyafanya hayo uliyoyataja.
 
Last edited by a moderator:
Umenena kabisa ndugu Mtambuzi! Salun zimejeruh na kusambaratisha ndoa na mahusiano mengi directly au in directly! Nlipokuwa nasoma post hii nimepata wazo la ghafla, je mtu kwa mfano akafungua kitengo cha kushughulikia maswala ya ndoa (marriage counseling) karibu na salun, ukawa unatoa ushauri wa kitaalam itakuwaje? Au humo humo ndani ya salun unakuwa na kachemba kako ka kutolea ushauri km zile za massage inaweza kulipa? Huwa nahurumia wanandoa wanaopotea just kwa kusikiliza watu walioshindwa ktk ndoa...!
 
Last edited by a moderator:
Kiukweli mimi ni mmama lakini sipendi kabisa kwenda saluni......
Najitahidi nakuwa na kila kitu changu nyumbani kwa ajili ya kuhudumia nywele zangu. naosha, steaming, nk mwenyewe. Nikitaka kusuka huwa nina mtu anakuja kunisuka nyumbani kwangu. Saluni naenda tu kama nina dharura.
 
Heshima yako mkuu kwa mada yenye ukweli 100% ijapokuwa siku hizi huonekani katika zile kesi za kusisimua kulikoni?
 
saluni ninayoenda mimi wahudumu wote ni wanaume... ni kazi tu hakuna umbea.

Umeona hizo eyebrows... ....nani hapo Mpwapwa anaweza kunifanyia threading......nataka arch shape.......zangu ukiziona utadhani brush lililoisha.......nipo njiani nakuja huko.....
 
Kiukweli mimi ni mmama lakini sipendi kabisa kwenda saluni......
Najitahidi nakuwa na kila kitu changu nyumbani kwa ajili ya kuhudumia nywele zangu. naosha, steaming, nk mwenyewe. Nikitaka kusuka huwa nina mtu anakuja kunisuka nyumbani kwangu. Saluni naenda tu kama nina dharura.

aahhh binamu hapo umenena huo ni mfano wa kuigwa, hizi saluni siku hizi kwa asilimia kubwa zimekuwa kama magulio hasa za Sinza... bora wangekuwa wanapiga umbea tu... afadhali lakini ukijua ya nyuma ya pazia lol.... chichemi
 
Back
Top Bottom