Wanavijiji Waendelea Kushirikiana na Serikali Kujenga Maabara za Masomo ya Sayansi Kwenye Sekondari zao za Kata

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

WANAVIJIJI WAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZAO ZA KATA

Wanavijiji wa Jimbo la Musoma Vijijini wamedhamiria kujenga MAABARA TATU za masomo ya sayansi kwenye Sekondari zao za Kata. Maabara hizo ni za masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia.

Jimbo letu lenye Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374 lina jumla ya Sekondari 25 za Kata, na 2 za Binafsi (Katoliki & SDA).

Vyanzo vya MICHANGO ya ujenzi wa Maabara hizo ni:
*Michango ya fedha taslimu kutoka kwa Wanavijiji na Mbunge wao wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo
*Nguvukazi za Wanavijiji - kusomba mawe, kokoto, mchanga, maji na kuchimba misingi ya majengo
*Fedha za Mfuko wa Jimbo
*Fedha kutoka Serikali Kuu, yaani TAMISEMI na Wizara ya Elimu
*Wadau wa Maendeleo zikiwemo Benki za NMB, CRDB, NBC na POSTA
*Baadhi ya Wazaliwa wa Musoma Vijijini

Sekondari zenye Maabara 3 za Masomo ya Sayansi zilizokamilika na zinazotumika ni:
(1) Mugango, Kata ya Mugango, (2) Bugwema, Kata ya Bugwema, (3) Kiriba, Kata ya Kiriba, (4) Nyakatende, Kata ya Nyakatende, na (5) Ifulifu, Kata ya Ifulifu.

(6) Makojo Sekondari ya Kata ya Makojo, itakamilisha maabara ya tatu kabla ya tarehe 30.7.2023

Sekondari nyingine 19 za Kata zinaendelea na ujenzi wa Maabara 3, na lengo ni kukamilisha ujenzi huo mwakani, kabla ya Julai 2024.

Sekondari 4 mpya zinazojengwa (Nyasaungu, Muhoji, Wanyere na Rukuba Kisiwani) lazima majengo ya maabara 3 za masomo ya sayansi yawe sehemu ya ujenzi wa sekondari hizo.

Halmashauri yetu (Musoma DC) inaendelea kushawishiwa na kuombwa nayo ianze kuchangia, kwa kutumia mapato yake ya ndani, ujenzi wa Maabara na Maktaba kwenye shule zetu!

Musoma Vijijini inaomba ipewe "High Schools" za Masomo ya Sayansi:
*Sekondari 6 zilizotajwa hapo juu ziko tayari kuanza kupokea Wanafunzi wa Form V (Kidato cha V) mwakani, Julai 2024

Masomo ya Hisabati na Sayansi kwa ngazi ya awali ya shule za msingi na sekondari ndiyo msingi imara wa taaluma mbalimbali za kiufundi zinazotoa, kwa uharaka, ajira ndani na nje ya nchi.

SHUKRANI
Wanafunzi wa Sekondari za Kata za Musoma Vijijini, Wazazi na Viongozi wao wa ngazi zote, wanaishukuru Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuchangia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu Jimboni mwetu - Ahsante sana.

Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
*Wanafunzi wa Kiriba Sekondari wakiwa wanafanya mazoezi kwenye Maabara yao ya Kemia (Chemistry practical class)

*Maabara 2 (Chemistry & Biology laboratories) za Makojo Sekondari zilizokamilishwa ujenzi hivi karibuni. Ujenzi wa Maabara ya tatu (Physics laboratory) ya Sekondari hii utakamilishwa kabla ya tarehe 30.7.2023

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumapili, 2.7.2023
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-07-02 at 10.26.05.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-02 at 10.26.05.jpeg
    78.3 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-07-02 at 10.26.05(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-02 at 10.26.05(1).jpeg
    74.8 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-07-02 at 10.26.06.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-02 at 10.26.06.jpeg
    74.5 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-07-02 at 10.26.06(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-02 at 10.26.06(1).jpeg
    68 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-07-02 at 10.26.06(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-02 at 10.26.06(2).jpeg
    101.3 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-07-02 at 10.26.06(3).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-02 at 10.26.06(3).jpeg
    33.4 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-07-02 at 10.26.07.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-02 at 10.26.07.jpeg
    95.1 KB · Views: 5
Back
Top Bottom