wanaume wa fesibuku wanapenda kweli?

Nov 11, 2011
49
10
Naombeni mnisaidie kidogo ili nipate kufahamu maana naona hii social network haina faida kabisa,
Mara ya kwanza tulionana fesibuku nililike picha yake hapo sasa ndo kosa baada ya hapo nikatumiwa namba mi sikuona hatari kwani nilichukulia kama social networking tukawa tunawasiliana alinialika nyumbani kwake sikwenda basi akanialika ofisini kwake.

Sikua na wasiwasi kwani nilijua ofisi ni sehemu yenye watu wengi hivyo hakuna baya linaloweza kutokea baada ya story za hapa na pale niliomba kuondoka akaomba anikumbatie bila hiyana nikakubali kumbe hilo ndo kosa langu hapo hapo mara akaanza na mabusu mara antaka na romance sikuweza kumkubalia ilibi nimng'ate kumbe ndo kama nilikua nampandisha hisia zaidi hakunielewa mara ulimi sikioni na kutaka kunichania blouse lakini sikukubali matokeo yake aliniumiza shingoni nikaondoka na alama.

Sio siri nilijuta sana ile siku na dakika hiyo hiyo nikadeactivate account yangu ili kujipa break kwanza,
Baadae alintumia message na kuniambia 'I love you' nikabaki najiuliza huko kunipenda ghafla kumetokea wapi au ndo love at first sight inavyokuwa?au alikua na kiu zake akataka kuzimalizia kwangu?
mimi sina hisia zozote juu yake zaid namuona kama rafiki embu nisaidieni mapenzi ndo huwa yanakua hivi?
wanaume wa fesibuku wanapenda kweli au wanataka kutimiza tu kiu zao?na ni sahihi kweli kupata mchumba fesibuku au mi sielewi
 
hahahahaahahahahahahah si uende huko huko ukawaulize..................hapa ni swa na kutuuuliza maswal ya kindergaten sisi wanafunzi wa secondari
 
unajibu hata kama wewe ni sekondari,jibu kisekondari kwani unafikiri wote mliomo humu mna miaka 30 wengine tuna miaka 20,kwahiyo bado hatujawahi kukumbana na hayo we unachotakiwa kufanya ni kutoa ushauri kama unaona swali la kindergaten basi liache
 
Malizia kufanya hiyo kazi ya tuition uliyopewa jana...
 
Huyo ni limbukeni. Ulitakiwa umripoti polisi kwa 'shambulio la aibu'. Pili uwe makini na kujificha na stranger kwene sehemu ambazo sio public, next time utabakwa na kuachiwa magonjwa yasiyo na tiba.
 
Kuna waliopata wachumba kutokana na Facebook
Kuna walioolewa kutokana na Facebook
Kuna walioumizwa kutokana na Facebook
Kuna waliochana kutokana na Facebook
Kuna waliosaliti ndoa zao kutokana na Facebook
Kuna waliokutwa na mauti kutokana na Facebook

Hitimisho: Facebook kama Facebook ilivyo sio mtandao mbaya watumiaji ambao ndio sisi wenyewe ndio tunaufanya mtandao wa Facebook uonekane kama vile kichaka cha maovu, same applies to Jamii Forums kuna viroja vya hapa na pale lakini hauwezi kulaumu mtandao wenyewe maana watumiaji ndio wanakuwa wana misuse privacy na uhuru wa kutumia internet.
 
Swahiba kumbe usipoamkia kaunta unakuwaga na mapointi hivi?...

Utanidai azam juice moja..
 
Hizi social network hizi watu wanasoshaliziana kweli kwel na wengi tulivyo vichwa panzi.....hivi unakutanaje kwa siri na mtu usiyemfahamu?
 
Asanteni nimewaelew vizuri..
Kupitia hii post nimejifunza humu ndani kuna wengine akili zao hazifikirii sawasaw,Eti jamii forum imevamiwa na watoto eti kwa mkasa huu jifunze kutokua mtu wa kutoa hukumu WHO ARE YOU TO JUDGE ukiona post ya kipuuzi/ya kitoto achana nayo kuliko kupoteza muda
Nimepena sana The finest alivyotoa maneno yake na wengine baadhi ambao ni watu wazima wanaelewa wameona ili nikue ni lazima wanishauri ili nipate kujifunza kwamba maisha ndivyo yalivyo.
 
kila mtu ana njia yake ya kutongoza , na inaonyesha ulikuwa unamkaribusha kila kitu ndo maana hakuchelewa kuvuka mipaka ... hukujiwekea mipaka kwake na akautumia udhaifu wako ..
 
Ulimwamini sana mtu usiyemjua. Na ukampatia fursa nyingi (namba ya simu, kumtembelea ukiwa peke yako, kukumbatiwa n.k) pia ambazo yeye kwa akili yake alitaka azitumie ipasavyo. Feisi buku ni zaidi ya uijuavyo, kama alivyoainisha The Finest, yapo mengi mazuri yanaweza kufanyika kupitia FB.. Lakini kwa sisi binadamu tulivyo % kubwa wanaitumia kwa yale yasiyo mazuri.
 
Kuna waliopata wachumba kutokana na Facebook
Kuna walioolewa kutokana na Facebook
Kuna walioumizwa kutokana na Facebook
Kuna waliochana kutokana na Facebook
Kuna waliosaliti ndoa zao kutokana na Facebook
Kuna waliokutwa na mauti kutokana na Facebook

Hitimisho: Facebook kama Facebook ilivyo sio mtandao mbaya watumiaji ambao ndio sisi wenyewe ndio tunaufanya mtandao wa Facebook uonekane kama vile kichaka cha maovu, same applies to Jamii Forums kuna viroja vya hapa na pale lakini hauwezi kulaumu mtandao wenyewe maana watumiaji ndio wanakuwa wana misuse privacy na uhuru wa kutumia internet.

So so true...na hakuna mahali palipoandikwa kuwa mwanaume unaekutana nae facebook ni muongo kuliko mwanaume unaekutana nae JF.... Ila kwa jinsi hiyo stori ilivyoenda,sina uhakika kama huyo mwanaume ana mapenz ya dhati.. anataka tu kamchezo,akishakulamba kwisha habari yako mamaa....
 
Back
Top Bottom