Wanaume naomba tuwapumzishe wanawake hapa Jukwaani, imekuwa kero na aibu sasa haya malalamiko yetu kila saa

Ivan Stepanov

JF-Expert Member
Apr 22, 2023
4,932
16,041
Kichwa cha uzi kinajieleza.

Guys, nafikiri hawa wanawake sasa tuwapumzishe, this is too much maana halipiti lisaa limoja uzi kuhusu mwanamke uko posted. Na kibaya zaidi ni wanaume ndio wanalia lia kuhusu hawa wanawake, mara wanawake hivi, mara wanawake vile, jamani ndio kusema wametushinda kiasi hiki mpaka kufikia hatua ya kutema nyongo every hour hapa JF??

Msome mwanamke wako, ukishamjua tulia kimya na jua namna ya kuenenda nae. Sio kisa manzi ako anapenda hela basi una kuja kulia lia hapa, tafuta hela mpe au piga chini tafuta unaye mmudu.

Kwanini uhangaike na vilivyo juu ya uwezo wako? Wanasema ukiona vyaelea ujue vimeundwa. Kama vimeundwa basi waundaji wapo pia. Mwanamke mzuri anagharamiwa. Sina maana kama na mimi pia nagharamia au nawapigia promo, hapana, nachofanya mimi naiba waliogharamiwa, namlaghai, nikishapata nachotaka kila mtu anaendelea na yake, I don't keep a woman that I can't afford, huo ni mzigo wa kujitakia. Halaf mwanamke ghali wala huhitaji degree kumjua kwamba hapo utatakiwa kuwekeza pesa ya kutosha, na mwanamke mjanja mjanja pia ni rahisi tu kumjua so tafuta unapopamudu pambana na hapo.

Sio unataka mambo mazuri halafu huna uwezo, ukipigwa na kitu kizito unakuja kuanza kulia lia hapa jukwaani.

Halaf mnapokesha kusema wanawake wa hapa ni ma jobless mara shapeless mara beautyless hizi ni tuhuma za kishamba sana sana kutolewa na mwanaume rijali aliyekamilika, yan ni vitoto pekee ndio vinakuja na hoja kama hizi. Wewe tafuta wa size yako uone kama utalalamika. Huwezi!!!

Ukitaka vizuri vilivyokuzidi uwezo na hutaki kugharamika basi jua tu kuwa unahitaji mbinu kuvipata. Hizi ni mbinu mshtukizo, yan manzi kabla hajajua nini kinaendelea au kabla hajaanza kukupa invoice ambazo ni halali yake, kwa kutumia hizo mbinu basi anajikuta ashaliwa zamani halafu huonekani.

Unaziua hizo mbinu?

Huwezi kuzijua wewe kama kila siku unakaa kulia lia hapa kuhusu wanawake badala ya kutafuta suluhisho.

Hebu tuwaache hawa wanawake. Sio kila dakika tu kuwaandama kana kwamba hamna kazi

za kufanya wanaume wazima.

Na ujue nini, wao badala ya kulalamika, wanakaa kimyaaaa kutusoma kisha wanakaza uzi kutunyoosha zaidi. Na kwa hali hii nachelea kufikiri kwamba hawa wanawake wametushika pabaya, maana haiwezekani kila siku ni wanaume tuu wanalalamika.

Ahsanteni.
 
๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘

๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ
 
Nina mashaka kama aliye andika huu uzi ni mwanaume, anyway unaweza weka hapa hizo nyuzi za malalamiko ili na wengine tuzione?
 
Back
Top Bottom