Toosweet
JF-Expert Member
- May 27, 2012
- 2,141
- 1,982
JF Kwenu,
Elimu humpa msomi kujiamini na kumfanya aheshimiwe na jamii. Kwa muda mrefu imekuwa tabia ya wanasiasa wetu kupenda kutajwa vyeo vyao vya kijeshi kabla ya majina yao, Luteni Yusufu Makamba, Kanali Jakaya Kikwete. Hupenda kuitwa hivyo hata kama wameachana na jeshi. Hii tabia naiona hapa Tanzania pekee.
Kagame na Kabila walikuwa majenerali, hawatumii tena vyeo hivyo baada ya kuingia kwenye siasa. Colin Powell, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani alikuwa jenerali wa jeshi. Hakutumia cheo hicho alipoingia kwenye siasa.
Kwa sasa vyeo vya kijeshi vimeanza kuachwa ingawa tuna wanajeshi kwenye nafasi za kisiasa, Meja Jenerali mstaafu Mustafa Kijuu(RC wa Kagera) ingawa bado anavaa gwanda.
Mtindo wa sasa ni kujipa au kupewa udaktari wa falsafa wa heshima(honorary PhD).Pamoja na kupewa kwa heshima, viongozi wa nchi nyingine hawatumii hizi titles. Hubaki kwenye kumbukumbu. Hapa kwetu mtu hufurahi kuitwa 'dakta' ili awakoge watu wakati hajaufanyia kazi. Dk. Jakaya Kikwete, Dr. Reginald Mengi(si mwanasiasa) Kwani kuna ulazima?
Kuna marais na viongozi wengine waandamizi duniani ambao wamesoma kwa viwango vya profesa lakini hawatumii tena titles za kisomi baada ya kuingia kwenye siasa. Hapa kuna Barack Obama, rais wa 44 wa Marekani(katika sheria),kulikuwa na Woodrow Wilson, rais wa 28 wa Marekani, Ricardo Lagos, rais wa zamani wa Chile, Bingu wa Mutharika aliyekuwa rais wa Malawi.
Wako PhD holders wengi pia, nimtaje tu waziri mkuu wa zamani wa Libya aliyekuwa na PhD ya electrical engineering.
Robert Mugabe ndiye rais msomi kuliko wote duniani. Ana shahada saba, mbili kati ya hizo ni masters. Mugabe ana shahada kumi na moja 11,za heshima, tatu zimekuwa revoked. Katika marais kumi wasomi Afrika, wa kwetu hayumo. Rais wa 7 wa Marekani, Andrew Jackson wa 18 Ulysses Grant, wa 28 Dwight Eisenhower ,walikuwa majenerali wa jeshi. Hawakutumia titles za kijeshi waljpokuwa wanasiasa.
Ikiwa kuna wasomi waliopiga shule hawatumii title za elimu au majenerali wa jeshi, kwa nini wale waliopewa kwa heshima wang'ang'anie u-'dakta' au wanasiasa wanajeshi nao wang'ang'anie u-luteni jenerali mstaafu?
Wale tuliojifunza kwao,ukishaingia kwenye siasa, wewe si academician tena, ni politician. Lengo ni kulinda taaluma zisichafuliwe na siasa. Watu wengi wa vijijini wanapata shida rais au waziri mkuu anapoitwa 'daktari'. Siwaonei wivu wasomi wanasiasa.Ni vizuri tujifunze kutoka kwa wengine. Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Ujerumani alipogundulika amekwiba andiko ili kupata PhD, aliachia ngazi.
Tujadili.
Sent using Jamii Forums mobile app