Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 118,321
- 219,633
Mara zote tumeandika humu na kwingineko kwamba Shetani hajawahi kuwa na Rafiki , nadhani sasa mmeanza kuelewa tulichomaanisha .
Ukitetea Wananchi hata kama wewe ni Mwanaccm , ni lazima utashughulikiwa tu , hii ni kwa sababu ccm haipo kwa ajili ya Wananchi .
---
Leo Jumatano Agosti 23, 2023 mawakili wa mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Ole Shangai anayeshikiliwa na polisi tangu juzi, wamefungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuomba mteja wao afikishwe mahakamani pamoja na wananchi wengine 30.
Ole Shangai alikamatwa juzi wilayani Karatu akiwa njiani kwenda polisi baada ya kupata maelekezo kutoka kwa mkuu wa upelelezi Mkoa wa Arusha.
Wakizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kupeleka maombi ya kufungua kesi hiyo, mawakili hao wamesema tangu mbunge huyo alipokamatwa, hawajui alipo.
Wakili Joseph Ole Shangai amesema wameamua kwenda mahakamani kusaka haki kwa maelezo kuwa makosa wanayotuhumiwa nayo yanadhamana kisheria.
Amesema juzi baada ya mbunge kukamatwa alikua naye polisi ambao walimuahidi wangempa dhamana mteja wake jambo ambalo limekuwa kinyume chake.
Wakili mwingine, Alayce Melau amesema, ‘’Tumepeleka maombi ya kesi kwa msajili tuna imani kesi itapangiwa hakimu wa kusikilizwa haraka uwezekavyo ili haki utendeke.
Baadhi ya wananchi wanaoshikiliwa hali zao ni mbaya maana baadhi ni wagonjwa kutokana na kipigo.’’
Hata hivyo, Polisi Mkoa wa Arusha hawajatoa taarifa yoyote ya kushikiliwa kwa mbunge huyo wa CCM. Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo kuzungumzia suala hilo zinaendelea.