Wanasheria Mnatungusha Watanzania

Tatizo hapa ni zaidi ya Wanasheria.

Si lazima kuwa mwanasheria ili kufungua kesi, si lazima kuwa mwanasheria kumshitaki mtu, si lazima kuwa mwanasheria kuanzisha "grassroot organization", si lazima kuwa mwanasheria kumbana mbunge, speaking of that, sio lazima kuwa mwanasheria ili kuwa mbunge na kwenda kutunga sheria.

Sasa huku kulia lia kuhusu Wanasheria, kunaweza kueleweka kwa upande mmoja, lakini upande wa pili tunarudi pale pale, tumezoea mtu fulani atufanyie kazi, tunatafuta mtu wa kumlaumu na kumtwika matatizo yetu.

Mwanasiasa, Mwanasheria, Fisadi, Msomi, mtu yeyote, mtu yeyote kasoro sisi wenyewe.

Wewe unayewalaumu wanasheria umefanya nini kwanza?
 
nafikiri tunachoongelea hapa ni zaidi ya sheria kwani tatizo ni mfumo dume wa serikali na ccm ndio imeoza mwanasheria ata uwe safi uwezi kupingana nao wanapotaka ufanye kazi zao
 
Mwanasheria aliyemakini na safi ana opportunity nyingi tu ya kulisaidia Taifa lake mifano tumeiona kwa Dr. Slaa na Tundu Lisu what if wangekuwa na backing ya chama chao cha wanasheria hii nchi ingefika hapa ilipo? Kumbuka Mafisadi bila wanasheria wazuri ambao wameua moral conscious zao hawawezi furukuta kwani ingekua rahisi kuwa kamata; why now hawawezi kamatika? Nikwasababu behind them there are very intelligent wanasheria ambao wanaweza kuwawezesha kufanya ufisadi salama!
 
nafikiri tunachoongelea hapa ni zaidi ya sheria kwani tatizo ni mfumo dume wa serikali na ccm ndio imeoza mwanasheria ata uwe safi uwezi kupingana nao wanapotaka ufanye kazi zao

Sawa mfumodume wa CCM.

Hii ishakuwa chorus hapa, and you are singing the chorus to the choir, we hardly need to hear that.

What we need to hear is how can each one of us, starting with you, topple that "Mfumodume"
 
Mwanasheria aliyemakini na safi ana opportunity nyingi tu ya kulisaidia Taifa lake mifano tumeiona kwa Dr. Slaa na Tundu Lisu what if wangekuwa na backing ya chama chao cha wanasheria hii nchi ingefika hapa ilipo? Kumbuka Mafisadi bila wanasheria wazuri ambao wameua moral conscious zao hawawezi furukuta kwani ingekua rahisi kuwa kamata; why now hawawezi kamatika? Nikwasababu behind them there are very intelligent wanasheria ambao wanaweza kuwawezesha kufanya ufisadi salama!

Sawa mwanasheria makini ana opportunities nyingi tu.

Lakini hata raia yeyote aliye makini ana opportunities nyingi tu, kabla hatujaanza kuona kibanzi kilicho jichoni mwa mwanasheria, je tumeona boriti iliyo jichoni kwetu?

Tushawahi kujiuliza kwamba wanasheria pia wanahitaji msukumo wa jamii? Na kama jamii haiwapi msukumo wanakosa energy ya kufuatilia mambo ipasavyo?

Ni lazima tukubali responsibility kama jamii nzima, kuanzia jeshi, walimu, madereva, wakulima, wafanyabiashara, makasisi, masheikh you name it, wote wana sehemu sawa katika hili.

Si haki kuwapa lawama wanasheria kama wao ni miungu watu wenye macho matatu na mikono sita.
 
Najaribu kufuatilia threads zako, uliyoyauliza ndio yameibuka, labda Kabudi na wenzake watawarudisha heshima ya wanasheria wetu kwenye mstari, mwanzoni swala sidhani kama lilikuwa ni ujuzi, ilikuwa ni kufanya kazi kwa mazoea, ubinafsi, rushwa na tamaa..
 
Back
Top Bottom