Wanasema tujiajiri wao mbona hawajiajiri?

.......Unajua mda mwingine sijui tuseme vituko

unakuta profesa. Waziri. Katibu mkuu. Dr. Mkurugenzi... Anasema graduates acheni mawazo potofu ya kuajiriwa.. Jiajiriri Ajira ni chache.... Dahhhh kauli inauma hii

cha kushangaza..

Wao hawajawahi kufikiria kujiajiri

watoto wao hawajawahi kuwahimiza wajiajiri japo wana mitaji ya uhakika kabisaaa

kwamba ni ngumu kukuta mtoto wa kigogo kakosa kazi.. Kumbe ajira zipo asehhhh....

Kwamba ikitokea ajira zimetangazwa ndo kwanza anatafutwa mtoto wa mjomba wa shangaz wa kaka.. Abandikwe ili mradi tu mtoto wa mkulima akose kazi.. Rejea sakata la uhamiaji

JAMANI... WANATANGAZA AMANI HUKU NYUMA WAMESHIKA MAPANGA HII SYO FAIR KABISAA

KWAMBA ajira ni chache wanatuhimiza vijana wa wakulima tujiajiri ilihali wanajua fika kuwa hatuna mitaji wakati watoto wao ambao wana uhakika wa mtaji hawawez kujiajiri..

kana kwmba haitoshi ht kile kidogo kinachotengwa kuwawezesha vijana wajiajiri watu wanagawana

inauma sana.. Lengo si uchochezi ila ni kueleza hali halisi. Au nimeongopa?????

Mkuu apo ndoo nashangaa mimi
 
Yaan wewe maneno unayotupiwa yangekuwa mishale, basi ni mvua, huponi hata kwa uchawi..... huna pointi!!!!! la maana ulilotoa na unalotakiwa kutoa siku zote za maisha yako ni USHAURI. Ondoka. Sio "mimi napingana na... mwa mwa mwa........ wewe fikiria mwa mwa mwa......" zaa wanao wasomeshe ndio uje uwaambie hayo mapingo yako!!!! Biashara wa kuijua wewe?????aliye kuhamasa je..... na yuko wapi tangu kaanza hadi leo??????? OLEWANYACHUUMLUTUNYE!
 
Hapa ni vigumu sana watu kuelewa ila ukweli utabakia ukweli Daima. kama viongozi hawajajiajiri na wanakuambia ujiajiri si sababu ya kukataa kisa wao wameajiriwa. Katika Dunia hii uko peke yako that is why hata ukifa utazikwa mwenyewe.

Tumekuwa tukitumia Ukosefu wa Mitaji kama Ngao. ni kweli kuna tatizo la mitaji but sio kwamba ndo iwe sababu kuu. Wengi wetu wana lilia wamekosa mitaj8 ikiwaambia waje na Idea zao watakuja na Idea za ajabu mpaka ushangae.

ili uweze kujiajiri unatakiwa kuwa Commitment. huo ndo mataji mkubwa kabisa. ukiamua utaweza ukiamua.

Wengi wetu tunaona Aibu na hii ni kwa sababu ya matarajio makubwa tuliokuwa nayo tukiwa vyuoni.
.Tukikaa kusubiria sijui mifumo inadilike tutasubili sana tena mno, kilichopo wewe ni kuanza na ulicho nacho na hakuna mtaji maalumu wa kuanzisha biashara. ila kama huna dhamira utabakia kusema mtaji hakuna.

mkuu,idea yoyote ukisha ifanyia practise ndo utajua matokeo yake kama nzuri au mbaya.unaposema watu watakuja na idea za ajabu sijui una manisha nini au unataka kila mtu afuge nguruwe ama?.
 
Mimi binafsi naamini katika kujiajiri! Nilipo maliza chuo niliona kuajiriwa ndio njia rahisi ya kupata maisha niliyokuwa najiwazia. Lakini nilipokuwa nimeajiriwa nilijikuta natumia muda wangu mwingi kuineemesha taasisi niliyokuwa naifanyia kazi huku kipato kikiwa kidogo! Lakini nilipofanya uwekezaji mdogo tu Kariakoo na pale Temeke, hela ninayotengeneza kwa siku ningesubiri mishahara ya miezi miwili kuipata kama ningeng'ang'ania kubaki kule kwenye ajira!
sijajua sana mazingira uliyopo lakini kwangu mimi kujiajiri naona kunaelekea kunipeleka kule ninako taka kwenda muda mchache ujao!

dili gani unafanya mkuu?
 
Mimi binafsi naamini katika kujiajiri! Nilipo maliza chuo niliona kuajiriwa ndio njia rahisi ya kupata maisha niliyokuwa najiwazia. Lakini nilipokuwa nimeajiriwa nilijikuta natumia muda wangu mwingi kuineemesha taasisi niliyokuwa naifanyia kazi huku kipato kikiwa kidogo! Lakini nilipofanya uwekezaji mdogo tu Kariakoo na pale Temeke, hela ninayotengeneza kwa siku ningesubiri mishahara ya miezi miwili kuipata kama ningeng'ang'ania kubaki kule kwenye ajira!
sijajua sana mazingira uliyopo lakini kwangu mimi kujiajiri naona kunaelekea kunipeleka kule ninako taka kwenda muda mchache ujao!
ok, mdau.kumbe uliajiriwa kwanza,kwa hiyo tunarudi kwenye point ile ile.hakuna asiyependa kujiajiri,but atleast wengi hutaka kuajiriwa ili apate muda wa kujipanga as well as the starting capital.kwanini hukumaliza chuo na kuanza kujiajiri moja kwa moja,kwa nini kwanza ulingoja upate kazi ya kuajiriwa? what was your logic behind/
 
Back
Top Bottom