H1N1
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 4,217
- 1,579
Assume wewe ni muislam na una wake watatu na watoto 5:4:3 yaani 12 jumla kwa wake watatu..umefariki
Kwa sheria za ndoa ya 1971; ugawaji wa urithi huo hauwezekani japo muislam huyu aliruhusiwa kuoa kiislam
Kwanini mali yake isigawanywe kiislam?? tunataka kadhi wawasaidie hao wanawake, watoto kuhusu mgawanyiko wa mali ya muumini huyu.. siyo voluntarily iwe sheria kabisa na hukumu itolewe na mahakama..ok
Ndio maana tunataka mahakama ya Kadhi..
NB: Naomba wale wenye hasira na uislam na waislamu watuache kwanza tuseme kwanini tunataka mahakama ya kadhi ili mtuelewe
Hakuna swala la kuassume hapa,ni ukweli ulio wazi katika ndoa ya Kiislam wake ni wengi ni ruksa kisheria.
mahakama za serikali na mirathi hizo hua ni halali,tatizo ni kukosekana mfumo maalum ambao umeamliwa ka QURAN yao kuhusu Kadhi,bado kama waislam wanayo namna ya kuanzisha kufuata taratibu zao kama zilivyoamliwa na kitabu chao.
Lakini kwa namna ambaywaislam wamesimama kutaka mahakama za kadhi zianzishwe sambamba na mahakama zingine kisheria,lazima kuna ajenda nyingine iliyojificha nyuma ya madai hayo. Sioni sababu ya Waislam kushindwa kuanzisha hizo mahakama ndani ya UISLAM wao wakiwa na haki ya kikatiba ya UHURU WAO WA KUABUDU huku wakiendelea kulalamika na kutaka kuanzisha fujo wakati jambo lenyewe lipo ndani ya uwezo wao kisheria.
Labda nikuulize wewe uliye uliza swali, wake zako wote ni WAISLAM,Ndugu zako waislam,hata watoto pia,NINI KINAWAPELEKA MAHAKAMA za kawaida kugawa mirathi na mshindwe kutumia taasisi zenu za kidini kugawa mirathi hiyo ?ambapo ugawaji ungezikatia maamrisho ya Quran yenu ?
Sheria ya ndoa hiyo ya 1971 inatambua uwepo wa NDOA ya Kiislam,sasa kama sheria hiyo inatambua uwepo wa ndoa hiyo maana yake inatambua hata namna ya ugawaji wa mirathi Kiislam,japo inajua pia kuwa huwezi kumshurutisha mtu kutumia sheria za Kiislam kama hataki.