NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,853
Hakuna anaejua siku yake ya kesho itakuwa vipi, lolote laweza kutokea uwe muhalifu ama sio mhalifu waweza kujikuta umeingia rasmi 18 za kwenda gerezani.
Wiki iliyopita nilienda mtembelea rafiki gerezani, yupo kwa takribani mwezi sasa kosa likiwa kununua simu kwenye magroup haya ya whatsapp, iliyoibiwa, simu aliyonunua kumbe ilikuwa ya wizi, kapewa kesi ya unyang'anyi kwa kutumia silaha, nilivyomkuta machozi yalinilenga. Ni mwezi kakaa lakini hali niliyomkuta nayo inasikitisha.
Mlo mmoja kwa siku tena ugal mkubwa ila mboga sasa unakuta majan yakunde yalokomaa maharage manne mchuzi pipa
Kuoga kwa folen
Kujisaidia kwa folen tena waziwazi kabsa wenzio wanakuona
Kulala sa kumi jioni,
Godoro kuu kuu zimeoza kwa jasho
Chumba kimoja wafungwa 50 mpk 60
Hakuna simu wala mawasliano ya aina yoyote
Kazi ni amri ni lazima kufanya
Ukiugua dawa za shida yan
Kwa upande wa mahabusu wanapoingizwa pale kwa mara ya kwanza huamini kuwa watatoka soon ila siku huwa wiki, wiki huwa mwezi, mwezi huwa miaka, wapo mahabusu kibao tangu 2020 kesi hazijasikilizwa
Epuka sana mambo ya madawa ya kulevya , wizi (ikiwemo kununua vya wizi), ujangili, kutembea na wanafunzi wa shule kike, n.k, hizi kesi ndio zina sotesha sana watu gerezani
Kama unadhani jela ni shule mpeleke mwanao, sio kuzuri hata kidogo