Wanaojua watufundishe kuhusu 'Cortex digital Marketing' je, ni matapeli?

The Next MP

Member
Nov 15, 2023
37
43
Tufaidishane pengine tukaokoa watu wengi kutotapeliwa au kuingiza faida.

Kuna namba ilinitumia message telegram wakidai wao ni kampuni ya marketing za online ambapo wanafanya media buy wakishirikiana na makampuni mbalimbali. Wanachofanya ni ku-recruit watu kufanya kazi ya ziada binafsi walinipa link nikawa na access ya kuona kinachoendelea kwenye group la telegram lenye wafuasi zaidi ya elfu 8. Kila baada ya dakika 20 wanaweka link unaenda ku-like na ku- subscribe, unascreenshot unamtumia alokuunganisha. kila action moja ya hivo unapata elfu moja.

Wiki iliyopita sikuwa biz kwahiyo kila link nilifanikiwa kufanya hivyo na nikatumiwa 27,000. nikafanya kwa siku 5 kila siku nikawa napata hicho kiasi. Hiyo kazi inabidi uwe na bando na muda wa kutosha kuchungulia kila mara kama kwenye group kuna link. Hizi link ni za makampuni na taasisi mbalimbali pamoja na wasanii wakubwa.

Kwenye group naona kinachoendelea na link zilikuwa zinatumwa mle lakini sina access ya ku-comment. Sasa kilichonishtua ni kwamba kuna wakati wanatoa orodha ya viwango vya pesa vya ku-invest yaani mtu anatuma pesa ndani ya dakika 30 anarudishiwa na kamisheni ya 9% mfano ukituma 30,000 anarudishiwa 39,000. wanajaribu kunishawishi lakini hii binafsi naona wazi wanataka kunipiga kwasababu kwa upande wangu mtu akishaingia hatua ya mimi kutuma pesa huwa naamini tayari huu ni utapeli. So naomba yeyote anayejua haya mambo tujuzane mimi huwa napenda kujifunza JF kabla ya kufanya kitu maana ni moja ya kuchunguza haya mambo. Karibuni wadau.
WhatsApp Image 2024-01-11 at 3.12.43 PM.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-11 at 3.12.00 PM.jpeg
 
Yaani mimi fursa yoyote ya kutumiwa meseji, tena na namba ngeni, fursa ambayo sijaitafuta huwa naipita kushoto.
 
Mkuu hao ntmn niingie kwa gia nyingne nile hela zao mana n tam kupata buku 10 ya chap n tam sana hzo invest wanazo weka wawatafute watu wa vijijni huko ndy watawatapeli.
 
Interested kujua mleta mada aliishia wapi. Atujuze maana hata mimi wamenicontact. Alifanikiwa kuinvest?
 
Tufaidishane pengine tukaokoa watu wengi kutotapeliwa au kuingiza faida.

Kuna namba ilinitumia message telegram wakidai wao ni kampuni ya marketing za online ambapo wanafanya media buy wakishirikiana na makampuni mbalimbali. Wanachofanya ni ku-recruit watu kufanya kazi ya ziada binafsi walinipa link nikawa na access ya kuona kinachoendelea kwenye group la telegram lenye wafuasi zaidi ya elfu 8. Kila baada ya dakika 20 wanaweka link unaenda ku-like na ku- subscribe, unascreenshot unamtumia alokuunganisha. kila action moja ya hivo unapata elfu moja.

Wiki iliyopita sikuwa biz kwahiyo kila link nilifanikiwa kufanya hivyo na nikatumiwa 27,000. nikafanya kwa siku 5 kila siku nikawa napata hicho kiasi. Hiyo kazi inabidi uwe na bando na muda wa kutosha kuchungulia kila mara kama kwenye group kuna link. Hizi link ni za makampuni na taasisi mbalimbali pamoja na wasanii wakubwa.

Kwenye group naona kinachoendelea na link zilikuwa zinatumwa mle lakini sina access ya ku-comment. Sasa kilichonishtua ni kwamba kuna wakati wanatoa orodha ya viwango vya pesa vya ku-invest yaani mtu anatuma pesa ndani ya dakika 30 anarudishiwa na kamisheni ya 9% mfano ukituma 30,000 anarudishiwa 39,000. wanajaribu kunishawishi lakini hii binafsi naona wazi wanataka kunipiga kwasababu kwa upande wangu mtu akishaingia hatua ya mimi kutuma pesa huwa naamini tayari huu ni utapeli. So naomba yeyote anayejua haya mambo tujuzane mimi huwa napenda kujifunza JF kabla ya kufanya kitu maana ni moja ya kuchunguza haya mambo. Karibuni wadau.
View attachment 2868351View attachment 2868352
Kaka naomba nisaidie namba zao hao jamaa niangalie nakconnect nao vipi niwapige.
Maana wanajikuta wanajua sana
 
Back
Top Bottom