MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 295
- 679
Nimesikiliza kipande kifupi cha Narration ya Filamu Tanzania the Royal Tour amesikika Mwongozaji wa Filamu hiyo kuwa Magufuli alifariki kutokana na matatizo ya Moyo lakini walio wengi wanaamini kuwa kifo chake kimetokana na COVID-19.
Walio wengi ni akina nani?
Walio wengi ni wapinzani wa Serikali akiwemo Lissu, Mbowe, Lema na wengineo wenye haiba kama hizo. Pia wanaharakati ni Maria Sarungi, Fatma Karume na wengineo ambao walionesha haiba hiyo.
Wote hawa kwa ujumla walishubaza shingo zao katika mitandao ya kijamii kuchapisha taarifa za kudai kuwa kifo cha Magufuli kimetokana na COVID-19 licha ya Serikali kuweka wazi kuwa kifo chake kilitokana matatizo ya moyo.
Hivyo, kauli ya Peter siyo jambo geni na wala haipaswi kuonekana ni jambo kushangaza kwani ametukumbusha yale yaliyozushwa na wapinzani wa serikali na wanaharakati hao wakati wa kifo cha Magufuli.
Cha ajabu ni kwamba, leo katika mitandao ya kijamii hao wanaharakati na wapinzani wa serikali5ue wanachapisha taarifa za kuona kauli ya Peter kama ni kauli ngeni, wakati wao ndio waliokuwa wa kwanza kufanya hivyo, na kupitia wao, Peter akaeleza kuwa walio wengi wanaamini hivyo licha ya Serikali kueleza ukweli.
Tumuogope Mungu na teknolojia.
Na;
Msema ukweli
23.04.2022