Wananchi wangapi walikataliwa Kupiga Kura Igunga?

kamanda mtema mnatutisha kidogo jamani chama makini hakitakiwi kutoa majawabu kama haya yasiyojitisheleza. wewe ni mbunge tunategemea
kuwa huko jikoni sasa inakuwaje makamanda wengine wanakwenda na info. frontline bila kuwa brief nyie wenyewe kwa wenyewe kwanza ili nyie
wote muwe na coherent message. basi tunategemea utawasiliana na wahusika ili tupate majawabu ya uhakika.

Usimlaumu sana kakiri mapungufu, Mheshimiwa Mbunge kafanya kazi kubwa sana Igunga na katuletea report ya huko mpaka wana JF tufaidike nayo, bofya hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-rostam-aziz-hutasameheka-13.html#post2601004
 
ndioi maana nafuatilia kwa kuuliza swali sasa nisingeuliza ningekuwa sifuatilii. Au ningeweza kufuatilia bila japo kuuliza?

Kazi njema. Labda utakuta waliokataliwa kupiga kura ni wengi kuliko waliokubaliwa na waliokataliwa wote walikuwa waipigie CHADEMA, vipi CCJ ndio imekufa kabla ya kutambaa?
 
Si vizuri kwenda kwa kuamini tu; ni vizuri kuwa na japo ushahidi wa awali. Maana isije kuwa hakuna mtu aliyekataliwa kupigwa kura kama alienda kupiga kura. Sijali sana wale ambao hawakwenda kabisa kupiga kura; I'm more concerned na wale ambao walienda kupiga kura lakini hawakupiga kura. This number interests me much.

Tumetazama kweli madhara yanayoendana na hili jambo yaani kitu kama multiplier effect?mtu mmoja anakataliwa anamwambia mke au mme au rafiki au jirani au coleague au yeyote yule kuwa haiwezekani halafu hao nao hawaendi kwakuwa wanajua hawatapiga kura. kwenye forum ni vyema kuviangalia vitu tofauti na namna vinavyotazamwa kwenye mahakama.
 
Kazi njema. Labda utakuta waliokataliwa kupiga kura ni wengi kuliko waliokubaliwa na waliokataliwa wote walikuwa waipigie CHADEMA, vipi CCJ ndio imekufa kabla ya kutambaa?

Wanasema ukiona kobe kainama.... CCJ mbona ilishatangazwa kufa na msajili na kufutiwa usajili? Sikilizia CCK au something like that.. utajua siyo vita vyote vinapigwa angani!
 
Kuna madai ambayo tulianza kuyasikia siku ya J'pili wakati waupigaji kura kuwa watu walikuwa wanakataliwa kupiga kura kwa sababu mbalimbali. Na baadaye madai haya yametolewa na pande zote mbili hasimu (Katibu Mkuu Mukama kwa upande wa CCM, na Mwenyekiti Mbowe kwa upande wa CDM).

Natumaini wote hawa wana ushahidi wa madai haya; binafsi ningependa kujua tu je vyama hivi vilifanya utaratibu wa kufuatilia na kujua wale waliokataliwa kupiga kura ni kina nani na sababu za kukataliwa ni zipi na kwa kufanya hivyo kuweza kujua kwa kiasi fulani idadi ya watu waliokataliwa kupiga kura kwenye jimbo hilo.

Kuna mtu ana namba isije kuwa ni idadi ambayo ni negligible - isingeweza kubadilisha matokeo. Kwa mfano (kama ni watu 100 kwenye jimbo zima hata kama wote wangeruhusiwa kupiga kura na wote wangeipigia CDM bado matokeo yasingebadilika).

Sidhani kama kwenda baada ya uchaguzi kuuliza watu kama walikataliwa yaweza kuwa njia sahihi ya kujua kilichotokea siku ya uchaguzi. Ni matumaini yangu CDM walifanya utaratibu wa kuorodhesha watu waliokataliwa kupiga kura kwenye vituo mbalimbali siku ya Jumapili mbili ya Oktoba.

Well;ni kweli kwamba kuna tatizo hilo lilitokea,na inasemekana,japo bado sijapata namba kamili ni watu zaidi ya 1000...Lakini nimeshangaa kwenye hii post yako mkuu MM umeipa kazi CDM kusema watu waliokatazwa kupiga kura,kwanini ukuuliza kwa upande wa CCM pia,CUF,UDPD,CHAUSTA,DP nk..maana wote hawa waliathirika na kitendo cha watu hawa kutokupiga kura...sidhani kama ni haki kuibebesha mzigo CDM juu la hili,ni tatizo la kitaifa kabisa...Lakini nasikitika sana kwa baadhi ya watu kuibebesha CDM mizigo isiyo yake,nadhani hili swali sehemu sahihi ilikuwa TUME YA UCHAGUZI au kwa msimamizi wa kituo cha uchaguzi Igunga...otherwise tuchambue mambo kwa undani kabla ya kusema chochote....
 
Kazi njema. Labda utakuta waliokataliwa kupiga kura ni wengi kuliko waliokubaliwa na waliokataliwa wote walikuwa waipigie CHADEMA, vipi CCJ ndio imekufa kabla ya kutambaa?

Kama huna cha kuongea si ukae kimya tu jamani? du mwanWAr maROPE bwana?
 
Ambao hawakupiga kura wako 2000 wale wageni walioletwa na Chadema kutoka mikoani kwenda Igunga
 
GY.... hapa nidpo tunahitaji sana SVO and CSOs kufanya kazi yao... alas' bado wana hangover ya alawansez za uchaguzi na ubwabwa wa wapiga kampeni
 
Wanasema ukiona kobe kainama.... CCJ mbona ilishatangazwa kufa na msajili na kufutiwa usajili? Sikilizia CCK au something like that.. utajua siyo vita vyote vinapigwa angani!

Mwanakijiji,

Achana na huyo Fox. Wengi hawakuielewa CCJ hata mimi niliwemo. Kweli kwa mwenendo wa huu ni rahisi sana mtu kuamua kupita njia ya CCJ(toa nape sijaelewa ni kwa nini alikuwemo kwa kweli).

Pamoja na mapenzi yangu makubwa kwa Chadema lakini naona nazidi kuwa frustrated siku hadi siku. Kushindwa uchaguzi hasa na chama tawala ni jambo la kawaida hasa eneo letu hili la sub sahara. Lakini kurudia makosa yale yale kila wakati inaanza kuchosa sana.

Uchaguzi uliopita pamoja na kusema kuwa nchi yetu haina udini lakini ni ukweli kuwa watu wengi ambao walifutwa majina yao au kuamishwa kituo kimoja kwenda kingine walikuwa ni wakristo wenye majina ambayo unaweza kuyaona toka mbali, John, David, Irene, Joshua and Emanuel. Na kwa kweli ilifanya kazi sana na unaona turn out iliyotokea.

Igunga yakarudia bali wakaenda hatua nyingine, yaani futa majina ya wagalatia, nunua ID za wagalatia halafu energise the base kwa mtandio. Lakini good news ni kwamba yote haya yanapangwa na wakristo wenyewe! what a shame!!!!111
 
Amekiri makosa ya kibinadamu kuhusu takwimu sioni umuhimu wa kumkomalia namna hii. Huyu dada kaonyesha political maturity.

Hata mimi sioni sababu ya kumkomalia mbunge Regia. Tume ya uchaguzi inafanya kazi kama vile ni mradi kazi ipite na ndio maana hawajui wanakosea wapi ili wajirekebishe katika uchaguzi unaofuata ili kuondio lawama kila uchaguzi. Wao wakisha tangaza matokeo wanaondoka badala ya kurudi kwa wananchi waone kasoro zilizojitokeza na kurekebisha. Haya mambo ya kuwahamisha watu kwenye vituo bila taarifa inaudhi sana. Mtu anazunguka zaidi ya vituo vinne haoni jina lake atahangaika kutafuta siku ngapi?

Hapo kwenye tume panatakiwa pakae watu wanaojituma kufanya kazi na kutekelaza haki kwa kila mtanzania. Mfano katika uchaguzi wa mwaka jana nimekuta jina la mtu ambaye amefariki 2006 badi lipo kwenye list sasa hapo kunautendeji kweli au ni ili mradi uchaguzi upite. Tume ya uchaguzi inatakiwa iwe karibu na wananchi kuwaelimisha jinsi ya kutumia haki yao wanapo piga kura. Na ndio maana ile siku ya kupiga kura ni siku yao sio nafasi ya vyama wao wanakuwa wameshafunga mikutano. Vyama vya siasa wanafanya kazi yao ya kutoa sera zao lakini tatizo la kupigakura lipo hapo tume ya uchaguzi.

Tume ya uchaguzi isiwe inasubiri kipindi cha uchaguzi ndio wanajifanya wako busy. Kuwe na adhabu katika sehemu husika endapo matukio yatakuwa yanajirudia ya kuwasumbua wananchi wanapotumia haki yao. Hii tume ya uchaguzi ikiwezekana ivunjwe iundwa yenye mwelekeo wa haki na wanaopenda kufanya kazi.

Lakini hapa ninapata shida kujua uchaguzi ukiisha watu wote wanarudi makao makuu au bado wanabaki wilayani? Hawa maafsa wa wilaya kazi yao ni kupiga umbea huko ofisini kutwa nzima hakuna wanchokifanya kila siku vikao vya utendaji utendaji gani mbovu kabisa.

Haya ni yangu machache.
 
Mh Regia kasema kama yeye. Kumbuka makamanda waliokuwa front line walikuwa wengi, yawezekana hizo data yupo mmoja anazo, tena kwa usahihi na usishangae baadhi ya wale waliokosa kupiga kura kwa sababu kama hizo wame sign mbele ya majina yao. CDM nawaamini.

Pengine hawaoni (hata MH Regia) haja ya ku disclose idadi na majina kwa wakati huu kwa hofu ya kuchakachuliwa. This is politics and you know this. As far as i can predict CDM wana kila kitu. Namwomba Mzee Mwanakijiji awe na subira hadi kesi itakapounguruma mahakamani. Vitu hivi mahala pake sahihi kutolewa ni mahakamani tu.

Let us wait and see, is when you will get back to me saying "Oh you was right". Hii ndiyo CHADEMA hayupo aliye mvivu wa kufikiri bana.!!
 
Mwanakijiji sijaelewa lengo lako hasa katik sredi hii ni nini?nikijua nitaweza kucomment zaidi

QUOTE=Mzee Mwanakijiji;2600564]Kuna madai ambayo tulianza kuyasikia siku ya J'pili wakati waupigaji kura kuwa watu walikuwa wanakataliwa kupiga kura kwa sababu mbalimbali. Na baadaye madai haya yametolewa na pande zote mbili hasimu (Katibu Mkuu Mukama kwa upande wa CCM, na Mwenyekiti Mbowe kwa upande wa CDM).

Natumaini wote hawa wana ushahidi wa madai haya; binafsi ningependa kujua tu je vyama hivi vilifanya utaratibu wa kufuatilia na kujua wale waliokataliwa kupiga kura ni kina nani na sababu za kukataliwa ni zipi na kwa kufanya hivyo kuweza kujua kwa kiasi fulani idadi ya watu waliokataliwa kupiga kura kwenye jimbo hilo.

Kuna mtu ana namba isije kuwa ni idadi ambayo ni negligible - isingeweza kubadilisha matokeo. Kwa mfano (kama ni watu 100 kwenye jimbo zima hata kama wote wangeruhusiwa kupiga kura na wote wangeipigia CDM bado matokeo yasingebadilika).

Sidhani kama kwenda baada ya uchaguzi kuuliza watu kama walikataliwa yaweza kuwa njia sahihi ya kujua kilichotokea siku ya uchaguzi. Ni matumaini yangu CDM walifanya utaratibu wa kuorodhesha watu waliokataliwa kupiga kura kwenye vituo mbalimbali siku ya Jumapili mbili ya Oktoba.
[/QUOTE]

Ww dada ww hujaelewa nn sasa hapo km kitu simple umeshindwa kuelewa je uwakilishi bungeni kweli unaweza ww ?. Watu wote tumemuelewa kasoro ww tu, hivi huoni aibu ww dada ? kila siku nakuambia acha kujiabisha
 
Mh Regia kasema kama yeye. Kumbuka makamanda waliokuwa front line walikuwa wengi, yawezekana hizo data yupo mmoja anazo, tena kwa usahihi na usishangae baadhi ya wale waliokosa kupiga kura kwa sababu kama hizo wame sign mbele ya majina yao. CDM nawaamini.

Pengine hawaoni (hata MH Regia) haja ya ku disclose idadi na majina kwa wakati huu kwa hofu ya kuchakachuliwa. This is politics and you know this. As far as i can predict CDM wana kila kitu. Namwomba Mzee Mwanakijiji awe na subira hadi kesi itakapounguruma mahakamani. Vitu hivi mahala pake sahihi kutolewa ni mahakamani tu.

Let us wait and see, is when you will get back to me saying "Oh you was right". Hii ndiyo CHADEMA hayupo aliye mvivu wa kufikiri bana.!!

Ndio mnajifariji ? mmeshindwa tu jipangeni upya !
 
Ni kweli kabisa kuna watu walikataliwa kupiga kura ila kwa takwimu sidhani sisi kama CHADEMA tunazo kwakuwa kwa bahati mbaya hatukuweka rekodi.Wale tuliokuwa tunazunguka kwenye vituo vya kupitia kura na kukuta changamoto hii tulichokuwa tunafanya ni kutoa tu taarifa kwa waratibu wa Kampeni nawao sina hakika kama watakuwa na takwimu.We were not smart kukumbuka kuweka takwimu..

Kwa majibu kama haya unadhani ni vipi watu watawaamini wa wape kuongoza nchi? Ile kauli mbiu yenu ya cdm chama makini iwapi hapa, sioni umakini wenu. Mnaanzisha mambo mengi halafu baadaye mnayaacha hivi hivi tu. Ziko wapi juhudi za kudai katiba mpya, yale maandamano ya nchi nzima yameishia wapi? suala la kupinga posho li wapi? and the list goes on. Mnatakiwa mbadilike bwana, mlingia vipi kwenye uchaguzi wa Igunga wakati mazingira ni yaleyale, baada ya kushindwa tuhuma ni zile zile, hamjifunzi jamani unajua sometimes mnakera basi tu, hatuoni mbadala hapa TZ.

Hapo kwenye red tuite jina gani huo kama sio uzembe, na anayejibu hivyo ni kiongozi tena mbunge kwenye bunge la JMT.
 
Kuna madai ambayo tulianza kuyasikia siku ya J'pili wakati waupigaji kura kuwa watu walikuwa wanakataliwa kupiga kura kwa sababu mbalimbali. Na baadaye madai haya yametolewa na pande zote mbili hasimu (Katibu Mkuu Mukama kwa upande wa CCM, na Mwenyekiti Mbowe kwa upande wa CDM).

Natumaini wote hawa wana ushahidi wa madai haya; binafsi ningependa kujua tu je vyama hivi vilifanya utaratibu wa kufuatilia na kujua wale waliokataliwa kupiga kura ni kina nani na sababu za kukataliwa ni zipi na kwa kufanya hivyo kuweza kujua kwa kiasi fulani idadi ya watu waliokataliwa kupiga kura kwenye jimbo hilo.

Kuna mtu ana namba isije kuwa ni idadi ambayo ni negligible - isingeweza kubadilisha matokeo. Kwa mfano (kama ni watu 100 kwenye jimbo zima hata kama wote wangeruhusiwa kupiga kura na wote wangeipigia CDM bado matokeo yasingebadilika).

Sidhani kama kwenda baada ya uchaguzi kuuliza watu kama walikataliwa yaweza kuwa njia sahihi ya kujua kilichotokea siku ya uchaguzi. Ni matumaini yangu CDM walifanya utaratibu wa kuorodhesha watu waliokataliwa kupiga kura kwenye vituo mbalimbali siku ya Jumapili mbili ya Oktoba.

Haijalishi idadi ya watu na hata akiwa mmoja kama amekataliwa kupiga kura (wakati anastahili) kwa jamii zilizostaarabika hilo ni kosa kubwa sana.
 
Well;ni kweli kwamba kuna tatizo hilo lilitokea,na inasemekana,japo bado sijapata namba kamili ni watu zaidi ya 1000...Lakini nimeshangaa kwenye hii post yako mkuu MM umeipa kazi CDM kusema watu waliokatazwa kupiga kura,kwanini ukuuliza kwa upande wa CCM pia,CUF,UDPD,CHAUSTA,DP nk..maana wote hawa waliathirika na kitendo cha watu hawa kutokupiga kura...sidhani kama ni haki kuibebesha mzigo CDM juu la hili,ni tatizo la kitaifa kabisa...Lakini nasikitika sana kwa baadhi ya watu kuibebesha CDM mizigo isiyo yake,nadhani hili swali sehemu sahihi ilikuwa TUME YA UCHAGUZI au kwa msimamizi wa kituo cha uchaguzi Igunga...otherwise tuchambue mambo kwa undani kabla ya kusema chochote....
Kwa kuongezea tu ni kwamba katika muda huo wa kupiga kura endapo CDM wangeanza kuandikisha majini ya hao waliodhulumiwa haki yao ya kupiga kura, wangeambiwa waneanzisha vituo hewa vya kupigia kura au hata kusingiziwa kwamba wanagawa rushwa.
 
Back
Top Bottom