Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,194
- 4,116
Wapo watu wengi wenye sifa za kupiga kura, lakini wamekuwa wakijiandikisha na baada ya hapo hawaendi kupiga kura kuwachagua viongozi wa kuwaongoza, na wengine hawajiandikishi kabisa licha ya kuwa na sifa stahiki na ni haki yao ya msingi ya kikatiba.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imempa haki kila raia wa Tanzania kupitia Ibara ya 5 (1), kila raia aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane kupiga kura. Lakini Watu wamekuwa wakishindwa kutumia haki hiyo kwa sababu mbalimbali wanazozijua wenyewe.
Kupitia sanduku la kura raia anapata fursa ya kufanya maamuzi ya kumchagua kiongozi anayeona ana sifa za kumuongoza.
Je, ni sababu zipi zimekuvunja moyo au kukufanya uache kupiga kura licha ya kuwa na sifa na unafahamu umuhimu wa zoezi hili?