Wananchi wamvamia mwekezaji mgodini

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Mgodi wa Dirif wasitishwa kutoa huduma baada ya wananchi kumvamia mwekezaji aliyeletwa na kikundi cha Kagera wakishinikiza aondoke kwa kuwa ni mali ya wananchi.

Katavi. Mgodi wa Kijiji cha Dirif uliopo Manispaa ya Mpanda umesitishwa kutoa huduma na Serikali kutokana na taharuki iliyotokea baina ya wananchi na wasimamizi wa mgodi huo kikundi cha Kagera wanaolalamikiwa kuleta mwekezaji kinyemela pasipo kuwashirikisha kwa lengo la kujinufaisha wenyewe tofauti na taratibu walizojiwekea huku Tundu Lisu akilaumiwa kwa kutetea wawekezaji zaidi badala wananchi.

Taharuki hiyo imedumu zaidi ya masaa 11 kuanzia asubuhi hadi jioni Mei 5, 2023 baada ya wananchi wa Kijiji cha Dirif kuuvamia mgodi huo wakimtaka Mwekezaji Kamtoni, kusitisha shughuli za uchimbaji dhahabu kwa kuwa eneo hilo lina mgogoro muda mrefu na linamilikiwa na wananchi.

Wakazi hao walisikika wakipaza sauti zao “tunataka mlima wetu” wakidai hawana imani na uongozi wa kikundi cha Kagera waliowapa dhamana ya kusimamia mgodi huo kisha kutafuta leseni ya umiliki wao binafsi.

Mussa Keta mkazi wa kijiji hicho amesema mgogoro baina yao na kikundi hicho ulianza 2022 hadi sasa na kwamba walishatoa taarifa ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mpanda lakini imeshindwa kuutatua.

“Tunashangaa ofisi imeshindwa kutoa maamuzi kwasababu leseni inayotumiwa na kikundi cha Kagera ni ya wananchi wote, viongozi walikuwa wanapeleka dhahabu soko la madini tumewachoka kwa ufisadi wao,” amesema.

“Hadi sasa tunawadai zaidi ya Sh45 milioni, tunachoshangaa wanaleta mwekezaji bila wananchi kujua, tumeona grenda linakwangua ndo maana vurugu zimetokea, kwa mwezi wanakusanya Sh4 milioni zinakwenda wapi?” amesema.

Amesema matarajio yao fedha hizo zitumike kuboresha miundombinu ya shule na miingineyo lakini hadi sasa shule yao haina choo cha walimu na huduma ya maji hali iliyopelekea mradi ujenzi wa zahanati kukwama.

“Kuna watu wengi wakiwamo wazee na vijana wanategemea kunufaika na mgodi huu lakini hawanufaiki na chochote wanaonufaika ni watu nane pekee hatuwataki tuliwachagua sisi sasa wametosha kutuibia,” amesema.

“Unaona risasi hizi zimepigwa baada ya wananchi kumfuata mwekezaji kumushusha pale, askari aliyeletwa kuwalinda akafyatua, anapiga wachimbaji wanaotafuta ridhiki, hizi zinatakiwa kupigia majambazi, watu walipata hasira wakarusha mawe,” amesema Keta.

Kilio cha wananchi hao wanahitaji ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi kuingilia sakata hilo kwa madai kuwa, hawamtaki mkuu wa wilaya kwasababu anauchochea mgogoro huo na kupelekea kukosa haki yao ya kupata mahitaji na kusomesha watoto.

Imedaiwa kuwa baada ya mgogoro huo kuwasilishwa Ofisi ya Mkuu Wilaya ya Mpanda alikwenda Kaimu Mkuu Wilaya, Onesmo Buswelu akaelezwa changamoto hiyo na wananchi kupitia mkutano wa hadhara.

“Aliuliza huu mgodi ni wa kikundi cha Kagera au wananchi? mmoja wa kiongozi kutoka kikundi hicho alijibu ni wa wananchi, akauliza mnataka nini tukajibu uongozi uliopo utoke tuchague wapya na mwekezaji Kamtoni hatumtaki,” amesema.

“Wakakubali wakasema hatuwezi kutoa majibu sasa hivi tutaenda kukaa kikao tujadili tulete mwafaka, kabla ya pasaka tulitakiwa kupewa taarifa lakini hatujapata na kazi zinaendelea,”amesema Lwiza Nkomedi.

Aidha amesema majibu wanayopata kutoka kwenye kikundi cha Kagera ni kwamba wameidhinishwa na ofisi ya mkuu wilaya, mgodi ni mali yao bila maandishi au kuitisha mkutano wowote kama walivyoahidiwa.

Mkazi mwingine wa kijiji hicho Hamisa Masebu amesema baada ya eneo hilo kugundulika kuwa lina madini aina ya dhahabu wananchi walitozwa fedha kulingana na uwezo wao.

“Mimi nina mgahawa nilitozwa sh5000 wengine Sh100,000 na kuendelea, tukawachagua viongozi wasimamie lakini wanajinufaisha wenyewe tunamuomba Rais (Samia Suluhu Hassan) atusaidie, eneo hili halina mashamba tunategemea mgodi huu,”Hamisa.
 
Aisee, Washikilie papo hapo mpaka kieleweke. Tunachoshwa na kusikia masuala ya Unyonyaji na dhuluma zinazofanywa na wawekezaji uchwara. Wananchi waamke kudai haki yao stahiki pale jambo kama hili likitokea.
 
Back
Top Bottom