Exaud J. Makyao
JF-Expert Member
- Nov 30, 2008
- 1,518
- 22
1. Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni,
na ajira bora kwa wageni pia.
2. Katika nchi yetu wenyewe,
tumekuwa kama yatima wasio na baba,
mama zetu wamekuwa kama wajane.
3. Tumebaki kuitwa WANANCHI,
Lakini wapo WALANCHI.
4. Ni lazima kununua maji tunayohitaji,
Raslimali zetu zapatikana kwa kuzinunua.
5. Haki zetu, sasa zapatikana sokoni,
Wenye nacho ndiyo wamiliki wa haki zetu.
6. Wenye nacho hawashindwi kesi,
Katika zetu mahakama.
7. Wale ambao wanafuatilia maisha yetu,
wapo kwenye njia zetu,
Tumechoka na hakuna pumziko.
8. Tumejitolea kuwatumikia wageni,
ili tupate chakula chetu cha siku kwa siku.
9. Je, ni Baba zetu walitenda mabaya,
na sisi tunachukua adhabu yao?.
Au twateseka kwa makosa yetu wenyewe?
10. Wageni wanatutawala, vitega uchumi wajitwalia,
nani ajitolee kutuweka huru kutoka katika mateso?
na ajira bora kwa wageni pia.
2. Katika nchi yetu wenyewe,
tumekuwa kama yatima wasio na baba,
mama zetu wamekuwa kama wajane.
3. Tumebaki kuitwa WANANCHI,
Lakini wapo WALANCHI.
4. Ni lazima kununua maji tunayohitaji,
Raslimali zetu zapatikana kwa kuzinunua.
5. Haki zetu, sasa zapatikana sokoni,
Wenye nacho ndiyo wamiliki wa haki zetu.
6. Wenye nacho hawashindwi kesi,
Katika zetu mahakama.
7. Wale ambao wanafuatilia maisha yetu,
wapo kwenye njia zetu,
Tumechoka na hakuna pumziko.
8. Tumejitolea kuwatumikia wageni,
ili tupate chakula chetu cha siku kwa siku.
9. Je, ni Baba zetu walitenda mabaya,
na sisi tunachukua adhabu yao?.
Au twateseka kwa makosa yetu wenyewe?
10. Wageni wanatutawala, vitega uchumi wajitwalia,
nani ajitolee kutuweka huru kutoka katika mateso?