Wananchi Mtwara Mjini wafanya maandamano makubwa kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar!

Hivi hiyo gesi ikibaki mtwara bila kupelekwa Dar ndo itawafaidia nini? Rasilimali ni vizuri ikajulikana ni za nchi wala siyo mkoa, wilaya au kanda. Kama Mtwara ungekuwa jiji lenye watu wengi na matumizi makubwa na fursa ya kutumia gesi ikapelekwa Dar na kuacha Mtwara hapo kungekuwa na tatizo.
Unaelewa ulichokiandika lakini au na wewe ndio wale wale wazee buku 2 per day kupost ujinga JF? Jifunze kwanza Niger Delta wanadai nini halafu ndio utajuwa madai ya wamakonde ni ya msingi na sasa kimbilio la CCM ni kwa Wazaramo na Wakwele tu ambao raslimali zao ni mihogo na kisamvu tu labda na mafenesi.
 
Ni haki yao kikatiba kutoa mawazo yao hatahivyo hawapaswi kupongezwa kwa kufuata sera za kikanda badala ya kinchi
Samahani kama nitakuwa nimekuelewa vibaya. Sisi wana Mtwara tunatambua kwamba mkoa wetu ni sehemu ya nchi ya Tanzania. Tunapinga kuhamishwa gesi toka Mtwara kwa kuwa tunaamini kwamba mandhari ya Mtwara ina kila kitu ambacho kipo huko gesi inapo pelekwa, na kama ni hivyo kwa nini gesi ihamishiwe huko badala ya kuruhusu fursa zinazo jitokeza kutokana na kuwepo na gesi kuifuata gesi Mtwara? Kilichofanyika katika mchakato mzima wa kutaka kuhamisha gesi toka Mtwara ni ubinafsi wa raisi wetu. Lengo kubwa la raisi ni kuhamisha fursa hizi zitokanazo na gesi kwenda kwao Bagamoyo. Sisi hatulitaki hili, na tunauhakika tutashinda kwa sababu tunajua kwamba uwezo wa kushindana na ukandamizaji wa aina hii ni umoja wetu.
 
Komaeni hivyohivyo mpaka mpate maelezo ya kutosha kuwa mtafaidika vip na hiyo gas kama ilienda kuuzwa dar na kwingineko.
 
Jamani tuwekane sawa,Hakuna mwana Mtwara yeyote asiyetaka Gas kuondoka ,tatizo ni namna ya kuondoka .Kwa nini iondoke kwa njia ya Pipe na production ikafanyike Kinyelezi-Dar badala ya Mtwara?,Kila mtu anafahamu kule inakofanyika final production ndiko kutakako pata mafanikio.Tunataka production ifanyike Mtwara tupate Mrahaba wetu .
Alafu ,kwa nini wanataka kuiondoa Gas Mtwara bila kusema kwa kila kiwango cha Gas itakayo ondoka Halmashauri au Mkoa utapata Mgao kiasi fulani?,wao wanasema inaondoka tu.Hatukubari,
Ieleweke bayana hakuna anayetaka kugombea Rasilimali za eneo husika zisitumime kwa Maslahi ya Wote HAPANA.
Tatizo ni namna ya kuzitumia hizo rasilimali,kwa nini kila kitu kiwe Dar ?,kwani Nchi hii ni Dar tuuu?.
 
Ndugu zangu wa Mtwara nyie ni watu makini, msiponzwe na CHADEMA, maandamano si njia bora ya kudai haki zenu, tumieni wawakilishi wenu kuanzia madiwani hadi wabunge watafanyia kazi kupitia serikali yetu sikivu

Wasiponzwe na CHADEMA ila wawakubalie MAGAMBA kuchukua gas....!!!!!
 
mkoa wangu upo nyuma sana, hizo tetesi za kukataliwa hawa wa ghasia zilianza kama mzaha sasa zinajitokeza. gas inapelekwa dar wenyewe hatufaidiki wapi na wapi?

Na mapato yatokanayo na mbuga, madini na raslimali zingine zibaki kwa wenyeji? sidhani kama ni sahihi kwa walichokifanya.
 
Urusi ndiyo nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa gesi duniani na wamejenga bomba la kusafirishia gesi hiyo hadi Bahari Nyeusi (Black Sea) ili waweze kuisafirisha kwenda Ulaya ambako ndiko kuliko na soko!

Itakuwa ajabu kwa gesi ya Mtwara kubaki huko ambako hakuna watumiaji wala soko!

Nadhani kuna upotoshaji mkubwa umefanywa, jitihada zifanyike kutoa elimu sahihi kuhusu gesi na hasa matumizi yake!

Ni kweli kuwa mitambo ya kuzalisha umeme na viwanda vya mbolea vitakavyotumia mali ghafi ya gesi vijengwe Mtwara na Lindi lakini pia bomba la kusafirisha gesi hadi Dar es Salaam, Tanga, Morogoro nk kwa matumizi ya nyumbani na kuendesha magari nk linapaswa kujengwa!
 
Ndugu zangu wa Mtwara nyie ni watu makini, msiponzwe na CHADEMA, maandamano si njia bora ya kudai haki zenu, tumieni wawakilishi wenu kuanzia madiwani hadi wabunge watafanyia kazi kupitia serikali yetu sikivu

maandamano ni haki yao kikatiba na katiba sio mali ya chadema bali ni ya watanzania wote.
hao wawakilishi unaosema ndo kina hawa ghasia ambao wamewafanya wana mtwara kuwa misukule wa ccm.
ccm imewanyanyasa watu wa mtwara na sasa wamechoka.
 
Ndugu zangu wa Mtwara nyie ni watu makini, msiponzwe na CHADEMA, maandamano si njia bora ya kudai haki zenu, tumieni wawakilishi wenu kuanzia madiwani hadi wabunge watafanyia kazi kupitia serikali yetu sikivu

Unaogopa eh? Usijali Tararibu tu kila mtu ataelewa
 
Ndugu zangu wa Mtwara nyie ni watu makini, msiponzwe na CHADEMA, maandamano si njia bora ya kudai haki zenu, tumieni wawakilishi wenu kuanzia madiwani hadi wabunge watafanyia kazi kupitia serikali yetu sikivu

hawa wawakilishi walishashindwa siku nyingi maana wote wanaishi DSM; ukweli wa hii gas serikali haijatoa elimu ya uraia kwa wananchi kwa hiyo wananchi wanaonekana kama vile wametelekezwa tuu kwa kuambiwa gas inaelekea DSM na huko Bagamoyo pili vidia kwa hilo bomba la gas imewaudhi zaidi maana vikiria shina la muhogo wamelipwa 100 kama sijakosea sasa kweli hapo wametendewa haki bila kupewa elemu yoyote au mkataba wa hiyo gas unasemaji kwa manufaa ya wenyeji na watz kwa ujumla
lazima elimu itolewe kwa maslahi ya wananchi wote sio tu Mtwara na kwingineko kuhusu hizi riziki za watanzania wote maana ilikuwa hivihivi madini yote wakapewa watu

so serikali iweke na mikata yote wasi kwa wananchi wote tujui tunafaidika vipi ya hiyo gas
 
Unaelewa ulichokiandika lakini au na wewe ndio wale wale wazee buku 2 per day kupost ujinga JF? Jifunze kwanza Niger Delta wanadai nini halafu ndio utajuwa madai ya wamakonde ni ya msingi na sasa kimbilio la CCM ni kwa Wazaramo na Wakwele tu ambao raslimali zao ni mihogo na kisamvu tu labda na mafenesi.

Hivi maandamano hayo yana uhusiano gani na itikadi za vyama? inawezekana kuna watu wanaandamana hawaelewi kwa nini wanaandamana. Sidhani kama madai ya watu wa Niger Delta yanaweza kufananishwa na hiki kinachoendelea huku Mtwara.
 
Nipo hapa pande za Bima watu ni wengi mno, foleni ni kubwa sijawahi ona, waandamanaji/wapigananji..wanazunguka barabara kuu huku jeshi la posilisi likiwa nyuma yao lengo kubwa ni kupinga utoaji wa gas ielekee daslam...nyimbo nyiingi wanazoimba ni kwamba hawamtaki hasa ghasia wala mkuchika na gas isiwafate bali wao waifate ilipo....

NB: Kwa hali hii naona watu wa mtwara tumeanza/wameanza kujitambua!! Impact yake gas ikihamishwa itakuwa kubwa kuliko maelezo...we still keep in watching...GAS KWANZA, VYAMA BAADAE!!
More photos to come soon!!Stay tuned!!

VIJANA WA MUJINI HUA WANASEMAGA OOOOI OOOOOI OOIII

WATU WANGU WA SOUTH SIDE WOTE NA WATANZANIA WENZANGU WOTE WANAOUCHIKIA CCM NA MAFISADI MAKE SOME NOOOOOOOOISYYYYYYY....!!!

CCM WAMETAKA CHAI SASA WANALALAMIKA YA KWAMBA INAWAUNGUZA SASA SSI TUWASAIDIEJE??

HAWAKAWII KUSEMA CDM WANAYACHOCHEA HAYAAA,,

MKUCHIKA NA HAWA GHASIA MFIKISHIENI JEIKEI UJUMBE YA KWAMBA CHAMAKI NCHANGA HALIKI TENAAAAA

:poa:horn:
 
hawa wawakilishi walishashindwa siku nyingi maana wote wanaishi DSM; ukweli wa hii gas serikali haijatoa elim ya uraia kwa wananchi kwa hiyo wananchi wanaonekana kama vile wametelekezwa tuu kwa kuambiwa gas inaelekea DSM na huko Bagamoyo pili vidia kwa hilo bombo imewaudhi zaidi maana vikiria shina la muhogo wamelipwa 100 kama sijakosea sasa kweli hapo wametendewa haki?
lazime elimu itolewe kwa maslahi ya wananchi wote sio tu mtwara na kwingineko kuhusu hizi riziki za watanzania wote maana ilikuwa hivihivi madini yote wakapewa watu

so serikali iweke na mikata yote wasi

Naona kama umechoka sana na hangover za sikukuu.
 
Hizi NGOs na vyama vinavyoshabikia maandamano ya watu wachache wa Mtwara watueleze yafuatayo:-

1. Uzalishaji wa gesi unaofanyika Mtwara
2. Watumiaji wa gesi mkoani Mtwara

Wananchi wasikubali kutumiwa na watu wanaotaka kupata maslahi yao kupitia maandamano

Kazi yenu ya kuitetea ccm inazidi kuwa ngumu. Huwa nakuambia mara kwa mara hapa, hali halisi ya maisha inawaamsha hadi wajinga wa mwisho toka usingizini. Kazi ya kuwarudisha usingizini tena ni ngumu kuliko maelezo. Subirini 2015 mkione cha mtema kuni!
 
Ndugu zangu wa Mtwara nyie ni watu makini, msiponzwe na CHADEMA, maandamano si njia bora ya kudai haki zenu, tumieni wawakilishi wenu kuanzia madiwani hadi wabunge watafanyia kazi kupitia serikali yetu sikivu
Usitudanganye..! Kama huna hoja kaa kimya. Maandamano haya hayajahamasishwa CHADEMA, nI maandamano ya wananchi wa Mtwara na hayana msukumo wa kisiasa. Tupo kwenye maandamano watu wa itikadi mbalimbali, na hatutofautiani katika lengo letu. Lengo letu ni kushinda madai yetu bila kujali tofauti za kihitikadi.
 
Urusi ndiyo nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa gesi duniani na wamejenga bomba la kusafirishia gesi hiyo hadi Bahari Nyeusi (Black Sea) ili waweze kuisafirisha kwenda Ulaya ambako ndiko kuliko na soko!

Itakuwa ajabu kwa gesi ya Mtwara kubaki huko ambako hakuna watumiaji wala soko!

Nadhani kuna upotoshaji mkubwa umefanywa, jitihada zifanyike kutoa elimu sahihi kuhusu gesi na hasa matumizi yake!

Ni kweli kuwa mitambo ya kuzalisha umeme na viwanda vya mbolea vitakavyotumia mali ghafi ya gesi vijengwe Mtwara na Lindi lakini pia bomba la kusafirisha gesi hadi Dar es Salaam, Tanga, Morogoro nk kwa matumizi ya nyumbani na kuendesha magari nk linapaswa kujengwa!

tatizo ndg yangu hiyo mikataba umeiona????? maana wananchi wana wasiwasi isije kuwa kama ya madini yetu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom