Wananchi Monduli wasogezewa huduma za afya

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
[h=2][/h] Jumamosi, Agosti 18, 2012 09:40 Na Eliya Mbonea, Monduli

TATIZO la upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi 5,996 wa Kijiji cha Esilalei wilayani Monduli, hatimaye limepatiwa ufumbuzi.

Wananchi hao kwa miaka mingi walilazimika kutembea umbali wa kilomita 16 kwa ajili ya kufuata huduma za afya katika Mji wa Mto wa Mbu.

Akizungumza wakati mbio za Mwenge wilayani humo, Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Jowika Kasunga, alisema kukamilika kwa ujenzi wa zahanati kijijini hapo kutawanufaisha wananchi wengi.

Alisema zahanati hiyo imegharimu Sh milioni 97 ambapo umejumuisha jengo la zahanati na nyumba moja ya watumishi.

“Ujenzi huu ulianza Mei, mwaka huu na umefanyika kwa makubaliano mazuri kati ya uongozi wa Kijiji na mdau Martha,” alisema Kasunga.

Alisema mdau huyo aliyeingia ushirikiano na uongozi wa kijiji hicho, hujishughulisha na masuala ya uwindaji na uhifadhi wa wanyamapori.

Aliueleza ujumbe wa Mbio za Mwenge Kitaifa ulioongozwa na Kapteni Honest Mwanossa kwamba tatizo hilo la upatikanaji wa huduma za afya ulisababisha akina mama wengi kushindwa kufikia huduma hizo muhimu kwao, ikiwamo afya ya uzazi.

“Akina mama wengi walishindwa kuhudhuria kliniki wakati wa ujauzito na matokeo yake waliendelea kujifungulia nyumbani na kukosa chanjo kwa watoto, hatua iliyosababisha watu wengi ugonjwa wa surua.

Katika uzinduzi wa zahanati hiyo, alizitaja huduma za afya zitakazopatikana hapo kuwa ni huduma za kitabibu kwa wagonjwa wote, huduma kwa wajawazito.

Huduma nyingine alizozielezea ni kwa wanawake wanaojifungua, huduma za kliniki kwa watoto chini ya miaka mitano, uzazi wa mpango kwa kina mama na wenzi wao, ushauri nasaha na upimaji wa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU).

Katika hatua nyingine, Kapteni Mwanossa aliwakabidhi wananchi wa Kata ya Leporko na Sepeko ng’ombe 44 kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete.

Wananchi hao walipoteza mifugo yao mwaka 2008/2009, baada ya kukumbwa na ukame mkali uliosababisha malisho na majani kukauka na ng’ombe wengi kufa.

Mbio za Mwenge kwa mwaka huu zinakwenda na ujumbe unaohamasisha watu kujitokeza na kuhesabiwa katika mchakato wa Sensa ya Watu na Makazi, itakayofanyika Agosti 26, Upimaji wa Ukimwi na Ushauri nasaha na vita dhidi ya dawa za kulevya.

[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
Tatizo la huduma za afya si majengo pekee, ni pamoja na upatikanaji wa dawa,vifaa tiba na wataalam. Hata hivyo tunawapongeza kwa mwanzo mzuri.
 
Back
Top Bottom