Wananchi: Maridhiano ni Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote

Salaam ,shalom!!

Ni Kweli homa ya Uchaguzi imepanda, wengine wameanza kuacha kuongoza vyama na kukimbilia kuanza maandalizi ya kugombea ubunge nk nk.

Wananchi hatufurahii urafiki kati ya chama tawala na vyama vya upinzani, maslah ya Wananchi yapo katika kutofautiana Kwa HOJA kuongeza Kasi ya maendeleo.

Tunasikia habari ya nusu mkate, kugawana vyeo, hiyo nusu mkate kugawana vyeo itasaidia vp

1. Kuondoa tatizo la mgao wa umeme nchini?

2. Nusu mkate, Itaondoa vp mfumuko wa bidhaa nchini?,

3. Nusu mkate, Itaondoa vp RUSHWA?,

4. Nusu mkate, Itaondoa vp urasimu kupata huduma mahospitalini?

5. Nusu mkate itasaidia vipi kulinda raslimali za nchi yetu?

6. Nusu mkate itasaidia vp kupatikana Kwa pesa kulipa mikopo na riba?

7. Nusu mkate itapunguza vipi pengo kubwa kati ya maskini na matajiri nchini?

8. Nusu mkate itasaidia vipi kupunguza ukubwa wa Serikali Kwa kupunguza gharama za uendeshaji serikalini, kupunguza idadi ya wabunge na baraza la mawaziri?

9. Nusu mkate, itasaidia Kwa kiasi Gani kuondoa watoto wanaorandaranda mitaani bila uangalizi wowote?

10. Kugawana majimbo kati ya CCM na upinzani kutachangia vipi kupunguza lindi la Umaskini Kwa wananchi maskini?

Wanasiasa jitahidini kuongea lugha ya wananchi tutaelewana.

ANGALIZO: Maridhiano ni kupata Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote.

Kheri ya mwaka mpya 2024, yajayo yanafikirisha.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA

Karibuni.
Rubbish! Tumehuru ingiza kwenye Ilani ya tundulissu 2025 pamoja na serkali za Majimbo (ukabila) na ndoa za mashoga. Mkishinda ndiyo mtuletee tumehuru na mashoga, hamtopata kwa maridhiano mlango wa nyuma.
 
Katiba mpya ni muhimu kwa mustakabali mwema wa taifa.
Wapinzanzani kukosa katiba mpya siyo nusu mkate bali kuukosa kabisa.
Twende kwenye ufafanuzi wa kugawana majimbo (labda hapo ndipo nusu mkate yaweza kupata kueleweka).
Je kuna namna yoyote wanasiasa wamekubaliana kugawana majimbo? (haya ni matusi kwa wapiga kura na wananchi kwa ujumla).
Kutopatikana Kwa Tume HURU ya UCHAGUZI itokanayo na Katiba mpya kunaondoa sauti ya Mwananchi kuchagua kiongozi amtakaye!!

Hujaona wameanza kupita na kugawa Mutungi ya gesi Kwa maskini?

Huoni wanagawana majimbo hapo?

Ubunge na uongozi wanaamini unanunuliwa Kwa pesa!!

Ikiwa Sanduku la kura haliheshimiwi, uchaguzi bila Tume HURU ya UCHAGUZI na KATIBA mpya wakazi Gani?
 
Rubbish! Tumehuru ingiza kwenye Ilani ya tundulissu 2025 pamoja na serkali za Majimbo (ukabila) na ndoa za mashoga. Mkishinda ndiyo mtuletee tumehuru na mashoga, hamtopata kwa maridhiano mlango wa nyuma.
Ninyi ni akina nani kudhani mnayo hati milki ya Tanzania yetu?

Hujui kuwa yupo Mungu atawalaye duniani, na anapenda KWELI na HAKI?

Thamani ya kura ni Bei Gani?
 
Kutopatikana Kwa Tume HURU ya UCHAGUZI itokanayo na Katiba mpya kunaondoa sauti ya Mwananchi kuchagua kiongozi amtakaye!!

Hujaona wameanza kupita na kugawa Mutungi ya gesi Kwa maskini?

Huoni wanagawana majimbo hapo?

Ubunge na uongozi wanaamini unanunuliwa Kwa pesa!!

Ikiwa Sanduku la kura haliheshimiwi, uchaguzi bila Tume HURU ya UCHAGUZI na KATIBA mpya wakazi Gani?
Tume huru ya uchaguzi, katiba mpya na mifumo mizuri ya utawala italetwa na wananchi wanaojielewa wanaoweza kupambana kuinua hali zao kwa kuwadhibiti wanasiasa.
Ubunge kununuliwa kwa fedha ni kwa sababu ya umasikini wa mali na fikra wa wananchi.
Kinachohitajika ni kuelimisha na kuwajenga kifikra wananchi wasikate tamaa, wajue kuwa nguvu na kura yao inaweza kudhibiti na kuwashughulikia wanasiasa (kama kura haiwezi kwa sababu ya mizengwe, nguvu inaweza). Elimu hiyo ilifika pia kwa wanasiasa (ambao ni sehemu ya wananchi), mambo yote yatakuwa sawa.
Kama sehemu kubwa ya wananchi ni majuha, wanasiasa hufanya watakalo.
Hata huko kwenye nchi zilizoendelea wananchi waliwashughulikia viongozi na wanasiasa ipasavyo, na ndiyo sababu leo kuna ustaarabu na maendeleo.
 
Betina wa pale mjengoni anatakiwa aendelee kuwa mbunge Kwa kuvunja jimbo la Mbeya mjini kuwa mawili. Huu ni wizi wa pesa za walipa Kodi.
 
Wakati wananchi tunadai Katiba mpya Ili kupunguza idadi ya majimbo yawe machache kupunguza Mzigo wa wananchi kugharamia Serikali,

Pale Mbeya na maeneo mengine wanapanga kugawanya majimbo Ili Kila Mmoja apate cake yake!!

Kugawanya majimbo, kunapunguza Umaskini wa Watanzania Kwa kiasi Gani zaidi ya kuiongeza?

Unakubaliana na mambo hayo?
Sikubaliani.
Tunatakiwa kupunguza walaji na tuongeze wazalishaji ili tuendelee.
 
Hivi hii kitu ni halisia ama uzushi? Naona hivi Sasa inaandikwa sana humu jukwaani. Na JF huwa haikosei.

Kweli chadema wamekubali kuachiwa baadhi ya majimbo ndiyo wakayaita maridhiano??I Ikiwa hili litatokea basi chadema kwisha habari yake
 
Hivi hii kitu ni halisia ama uzushi? Naona hivi Sasa inaandikwa sana humu jukwaani. Na JF huwa haikosei.

Kweli chadema wamekubali kuachiwa baadhi ya majimbo ndiyo wakayaita maridhiano??I Ikiwa hili litatokea basi chadema kwisha habari yake
Mara ya mwisho umemsikia Lema ni Lini?
 
Inawezekana Bi Tozo anayo dhamira ya dhati ya kuitaka katiba Mpya lakini anazongwa na wahafidhina ya Chama Twawala
Angekuwa na Nia ya dhati kutupatia Katiba mpya,

Asingetangaza kutaka Urais akiwa na mwaka mmoja tu baada ya kuokota dodo.
 
Back
Top Bottom