Wananchi Kwimba waigomea Tume ya kutoa Maoni

Nyakwec's Bro

JF-Expert Member
Apr 27, 2012
820
174
Wananchi wa wilaya ya kwimba mkoani,wamegoma kutoa maoni katika tume ya kukusanya maoni baada ya mkuu wa wilaya hyo kutoa wito kwa wananchi kujitokeza.

Wananchi hao wamesema kwamba hawawezi kutoa maoni ya katiba mpya wakati hiyo katiba ya zamani hawaijui inavyofanana toka iundwe hivyo hawawezi kutoa maoni katika jambo wasilolijua,hivyo wameitaka serikali wawapatie elimu juu ya katiba hiyo ya zamani hapo wataweza kuchangia maoni yao katika katiba mpya.

Chanzo: Matukio RFA

Tumeshuhudia serikali ikizuia taasisi za kiraia,vyama vya siasa kutoa elimu hiyo kwa madai ya uchochezi,swali langu ni hivi kweli serikali kwa kutaka maoni kwa watu juu ya kitu wasichokijua kutatuletea katiba tunayoita?!..
 
Tatizo tume na yenyewe ni kikwazo,wananchi wanapotoa maoni yao wanaambiwa wamepewa na vyama vya siasa hasa upinzani. Sasa tume inategemea wananchi watoe maoni gani wakati wengine hata maana ya katiba hawajui? Hapo warioba nae ni sehemu ya propaganda za kukwamisha upatikanaji wa maoni mazuri
 
Leo nipo NGUDU makao makuu ya wilaya ya kwimba! Nipo hapa uwanja wa mpira ambapo wajumbe wa watu kumi wa tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya ipo hapa ikiongozwa na mzee butiku. Watu ni wengi na kadri muda inavyozidi kwenda ndio jinsi watu wanavyozidi kuja. Mkutano umeanza kuanzia saa 2 asb leo. Wana kwimba wamehamasika kuja kutoa maoni yao.
Source: mimi mwenyewe CPA nikiwa NGUDU kwimba kwenye eneo la tukio.
 
Mkutano ndio umeisha mzee butiku ndio anafunga. Jumla ya wachangajia 36 kwa maneno na 320 kwa maandishi. Watu wametia maoni yao kwa ustaarabu bila woga. Kuondolewa kwa mbio za mwenge, sherehe za kumbukumbu za karume, nyerer, ukomo wa ubunge, usawa wa kidemokrasia,ukumo wa madaraka la urais n.k
 
Back
Top Bottom