Wanajeshi wastaafu wataka kushirikishwa mji mpya Kigamboni

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
bot_tabimg.gif

Wanajeshi wastaafu wataka kushirikishwa mji mpya Kigamboni
Send to a friend
Saturday, 14 January 2012 08:55
0digg

Shakila Nyerere
UMOJA wa wastaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) wanaoishi Kigamboni jijini Dar es Salaam, wamesema hawana tatizo na uanzishwaji wa Mji mpya na wa kisasa wa Kigamboni lakini, kwa sasa hawajakubaliana na mpango huo hadi hapo madai yao ya msingi yatakaposikilizwa.

Akizungumza na vyombo vya habari jana , Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Thadei Mgoso alisema , kutokana na kukiukwa kwa utaratibu uliowekwa , hawako tayari kukubaliana na mpango huo wa mradi wa kuendeleza kigamboni kuwe jiji la kisasa.

Mgoso alisema serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imekataa kushiriki kwenye midahalo mbalimbali pamoja na kupelekewa mialiko na hata kujibu tuhuma zinazotolewa na wakazi wa kigamboni, kupitia barua na vyombo vya habari.

“Sisi hatujaukataa mradi ni mzuri, lakini wamekosa kutushirikisha katika kila jambo lililokuwa likituhusu wakazi wa eneo hili na badala yake huwaita wadau wengine kushiriki vikao hivyo huu ni ukiukwaji wa sheria tuliokuwa tumekubaliana,” alisema

Alisema kutokushirikishwa kwa wamiliki wa ardhi katika eneo la mradi tangu hatua za kutangazwa kwa mradi, mpango wa jumla, mpango kamili, na kuundwa kwa Mamlaka ya Uendelezaji wa Jiji la kisasa (Kigamboni Develoment Authority-KDA), wakazi wamekosa imani kutokana na usiri unaofanywa kuhusu uendelezaji mji huo.

Alifafanua kwamba, pamoja na hayo kumekuwa na ukiukwaji wa sheria na udanganyifu unaofanywa na viongozi mbalimbali hivyo kufanya wananchi kupoteza imani na serikali.

Alisema hofu ni pamoja na ziara aliyoifanya Rais mstaafu wa Marekani, George Bush, na baada ya kuondoka wizara iliwatembelea wakazi hao.

Alisema miongoni mwa ziara za mara kwa mara zinazofanywa na wageni na matajiri kwenda katika mji huo zimekuwa zikiwatia hofu.

Alisema baadhi ya maeneo yatahitajika kwa ajili ya miundombinu na shughuli mbalimbali za umma na hivyo, serikali italazimika kutoa fidia kwa wahusika na kuzingatia fidia itakayotolewa kwa thamani ya soko

“Sisi tunaoondolewa bila ridhaa yetu ,fidia ya ardhi ni vema izingatie thamani halisi ya ardhi ili mwenye ardhi aweze kurudisha jengo litakalobomolewa, ni jambo la busara fidia imuwezeshe kujenga jengo kama hilo la mwanzo,” alisema.
 
Back
Top Bottom