Wanaharakati waandamane kumshinikiza Kikwete

Tuongozeni kishinikiza serikali kutekeleza maazimio ya bunge na sio kuandamana kulipinga bunge.

I couldn't have said it better.. hivi hata leoukiuliza Kikwete kafanya nini kuhusu Richmond kuna mtu anaweza kutuelekeza alichofanya JK zaidi ya kutake credit for other people's labor?
 
Nakubaliana na wewe Mwanakijiji for sure kazi ihamie kwa Rais,ila mimi siungi mkono utaifishwaji wa Dowans hayo mengine nayakubali kwa moyo wote.
 
yaani "hawezi".. then sababu lazima iwe nzito.. tusaidie mkuu..
JK hawezi kufanya hivyo kwa sababu naye ni moja katika Baraza la Mawaziri ambaye tena yeye Ndiye Mwenyekiti wake, Hivyo kufanya hivyo ni kujihukumu mwenyewe, Watu na Watanzania tunashindwa kujua kuwa Rais ana sehemu katika mambo haya na ndio maana nasema kuwa katiba yetu ina matatizo makubwa sana, maana rais anahusika moja kwa moja kwenye mambo ya msingi kama haya je anaweza kujichukulia hatua yeye mwenyewe
 
Kikwete anaogopa maandamano dhidi yake kuliko kitu kingine chochote. Yakianza maandamano dhidi yake au kumshinikiza ataharakisha kufanya maamuzi kwa haraka kwa sababu hataki wawekezaji waogope kuja nchini.
 
Nafikiri kinachotakiwa ni dereva tu maana mabasi na wananchi wapo tayari wamesikia mengi ya Ufisadi wanasubiri tu huyo dreva, sijui yuko wapi? Je, tutumie twitter au face book?
 
Back
Top Bottom