Wanafunzi wengi vyuoni wanafaulu mitihani kwa kutazamia/kuibia nini hatma ya tanzania?

mlimbwa1977

Member
Feb 7, 2011
24
0
Imebainika kuwa wanafunzi wengi katka vyuo vyetu nchini wanajihusisha na ghiliba/ujanjaujanja wakati wa mitihani mbalimbali au kazi wanazopewa na walimu wao,wapo wasiojihusisha kabisa na kazi zinazotolewa(assignments) lakini mwisho wa siku mtu anafaulu kwa kupata alama a,ndani ya vyumba vya mitihani ni aibu watu wanatengeneza kitu kinaitwa 'network' ili wapeane majibu kwa kila swali lililopo kwenye mtihani (hawana muda wa kuchemsha akili zao,mambo kwa shortcut).

Hiyo ni mipango mkakati inayomwezesha mtu kupata/kufikia malengo aliyoyakusudia(starategic objectives) lakini je hii ni njia sahihi itakayoliwezesha taifa letu kupata/kuwa na wataalamu weledi/waliobobea kuweza kulivusha taifa hili katika matatizo lukuki yanayoelekea kutushinda?

wapenda maendeleo,nini kifanyike kutokomeza hali hii kwa ustawi wa taifa letu?
 
Mbona ni kazi rahisi kuwadhibiti hao wanafunzi? Tatizo ni walimu na wasimamizi wa mitihani kotofanya kazi yao ipasavyo na wengine ni corrupt. La kufanya kutumia wasimamizi wa nje makini na ambao sio 'corrupt'.
 
Kikubwa usimamizi. Walimu hawazidi hata watano wasimamie wanafunzi elf 1 unafikiri wataweza.
 
sijuhi kama kitafanyika japo cha kufanywa kipo.,UDSM kwanza warudishe 'marticulation',2..wajenge vyumba vya kutosha kuweka nafasi kati ya mtu wakati wa mitihani,..3 suruhu ianzie chini kwenye primary vingnevyo huku juu ni matokeo ya ubovu toka chini
 
Back
Top Bottom