Wanafunzi (watoto) kupakiwa mbele kwenye bodaboda wakati wa kwenda na kurudi shule ni hatari kwa afya. Mamlaka na wazazi hamuoni hili?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,883
2,765
Habari za alasiri hii ndugu wana JF, naandika kwa kughadhabika kinamna kutokana na upuuzi unaofanywa na baadhi ya wazazi huku mamlaka husika (Jeshi la Polisi) likiwa doro tu.

Kuna huu utaratibu wa kuwapeleka watoto wadogo shule kwa kutumia usafiri wa boda boda. Mzazi anamkabidhi mtoto kwa dereva asubuhi, na jioni kumrudisha. Mtoto mwenyewe ni miaka kuanzia minne hadi saba hivi na kuendelea.

Sasa hawa watoto huwekwa pale mbele kwa dereva. Ukichukulia ni asubuhi, huwa kunakuwa na baridi (hapa DSM). Sasa tunajua tena mwendo wa hawa bodaboda. Huwa naviona vitoto vinavyokunja sura huku vikipigwa upepo mkali mwilini na usoni.

Hivi wazazi husika huwa mnajifikiriaje? Huwa mnaonaje? Kama unaweza kumkabidhi bodaboda mwanao katika mazingira hayo, hushindwi kumtelekeza mtoto huyo katika majanga mengine. Huo ndio ukweli. Wala hao wazazi wasisingizie ubize au ugumu wa maisha, au urahisi wa usafiri. Mnawajeruhi watoto wenu kidogo kidogo. Mnawajeruhi kimwii na kihisia.

Miili ile haijaandaliwa kuhimili upepo na baridi la asubuhi na jioni, na mchana jua na vumbi. Basi mngekuwa na huruma mkawa mnawavika watoto wenu makoti, hata na barakoa kuwakinga na vumbi na upepo na baridi.

Polisi nao hili mnaliona kila siku. Hukai sehemu dakika tano bila kuona bodaboda kapita na mtoto akiwa kamweka mbele yake kama ngao. Mnasubiri nini enyi mamlaka? Tuwafundishe kazi?

Wizara ya Afya mnangoja nini? Ustawi wa jamii mnasubiri nini? Kupata vitoto vyenye changamoto za afya na pumu? Kupata wateja wa pneumonia kwenye hospitali zenu?

Mamlaka husika amkeni muwakemee hawa wazazi wapumbavu. Muwachukulie na hatua stahiki. Kamateni bodaboda moja kisha mtafuteni mzazi husika na mumuwajibishe ipasavyo, hata ikibidi kulala sero, na faini nzuri tu juu.

Naamini ujumbe huu utawafikia wahusika wote.
 
Kuna mambo mengi Serikali yetu haichukui hatua, sembuse hili. Wazazi wa hao watoto hawachelewi kusema usiwapangie namna ya kuishi hahahaaaa....
 
Naona MODS mmehariri kichwa cha habari. Bado nasisitiza. ENYI WAZAZI WAPUMBAVU NA MAMLAKA VIZIWI
. ENYI WAZAZI WAPUMBAVU NA MAMLAKA VIZIWI
. ENYI WAZAZI WAPUMBAVU NA MAMLAKA VIZIWI
. ENYI WAZAZI WAPUMBAVU NA MAMLAKA VIZIWI
. ENYI WAZAZI WAPUMBAVU NA MAMLAKA VIZIWI
. ENYI WAZAZI WAPUMBAVU NA MAMLAKA VIZIWI
 
Sasa tunajua tena mwendo wa hawa bodaboda. Huwa naviona vitoto vinavyokunja sura huku vikipigwa upepo mkali mwilini na usoni.

 
Back
Top Bottom