Wanafunzi wanateseka sana kuhusu usafiri wa daladala

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
8,868
27,597
Ni majira ya asubuh niko kituoni nasubiri daladala(mwana JF pekee nisie na gari) nielekee kwenye mizunguko yangu ya kutafuta riziki.

Mara likafika daladala la kuelekea makumbusho, konda kasema sipakii baada ya kuona wanafunzi wengi pale kituoni. Kaenda mbele kapakia watu wazima kasepa.

Hali ni hiyo hiyo kwa wanafunzi hasa mida ya asubuhi na jioni. Ndio kusema kwamba serikali na jamii imeshindwa kuja na njia mbadala ya namna ya kusaidia wadogo zetu wawezi kupata namna nzuri ya kwenda na kurudi toka shule zetu pendwa za uuma?

Nadhani watu wana mawazo mazuri tu namna ya kuwasaidia wanafunzi kupata usafiri wa kwenda na kurudi shule, kama una wazo lililo bora au maoni tuweke wadau, najua kwenye wengi hapaharibiki kitu.

Shkuran sana wakuu
 
Back
Top Bottom