Tarehe 22, Juni, wanafunzi wa shule za upili wa Taasisi ya Confucious katika chuo kikuu cha Dar es Salaam Tanzania (UDSM) wametembelea kijiji cha kale cha Siping na jumba la maonyesho la mji wa Jinhua.
Kijiji cha Siping kilichoko katika mlima Jiufeng mjini Jinhua, kilijengwa mwanzoni mwa enzi ya Ming, ambacho ukubwa wake ni mita za mraba 6,000. Ukuta wa majengo kijijini umechongwa picha mbalimbali za ndege, wanyama, maua na kadhalika, ambao una thamani kubwa ya kihistoria na kiutamaduni. Kijiji hicho kimewekwa kwenye orodha ya vijiji maarufu vyenye historia na utamaduni vya China mwaka 2010.
Wanafunzi hao walitembea katika kijiji hicho, kujionea mandhari nzuri ya kijiji na kuzungumza na wanakijiji.
Wanafunzi na walimu wanapiga picha kwa pamoja nje ya lango la kijiji cha Siping
Wanafunzi wanatazama samaki wa rangi aina ya “Koi Fish”.
Wanafunzi wanatembea kwenye vichochoro kijijini Siping
Wanafunzi wanapiga picha pamoja na wanakijiji
Wanafunzi wanatazama vinyago vya kichina
Wanafunzi wanajifunza chesi ya Go
Wanafunzi wanajaribu mchezo wa Touhu
Wanafunzi wanatazama kisima
Wanafunzi wakikaa ndani ya shule ya Chongde
Siku hiyo mchana, wanafunzi hao walikwenda jumba la maonyesho la mji wa Jinhua. Jumba hilo linaonyesha historia ya maendeleo ya mji wa Jinhua na mpango wa maendeleo ya mji huo kwa kutumia teknolojia ya VR, modeli ya kidijitali, 3D na teknolojia nyingine za kisasa. Wanafunzi hao walishangaa kuona kasi ya maendeleo ya mji wa Jinhua.