Wanafunzi wa kike au mabinti wenye umri kati ya miaka kumi na tano mpaka miaka kumi na nane wanaopewa ujauzito au kufanya ngono na wanafunzi wenzao au vijana wenye umri unaoendana na wao wapewe adhabu ya muda mfupi kisha warudishwe masomoni chini ya uangalizi wa wazazi.
Imezoeleka kwamba watoto wa kike walio chini ya miaka kumi na nane wakipata ujauzito basi huachwa tu mtaani kwa maelezo ya kuwa wao hurubuniwa hivyo aliyerubuni ambaye ni kijana wa umri wake hukutana na rungu la miaka thelathini jela au zaidi. Lakini ukitazama kwa namna nyingine mabinti hao wanaozungumziwa huwa na miaka kuanzia kumi na tano na kuendelea hii si sawa hasa kwa dunia ya sasa ambayo wanaharakati wanapambania haki sawa kwa jinsia zote mbili. Sharia ya ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 13 na 17 kinaruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 kwa kibali cha Mahakama na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi na sharia ya makosa ya jinai Tanzania ya mwaka 2002 kifungu cha 130 (2)mtu mwanamume atafanya uhalifu waubakaji kama ataingiliana kingono na msichana au mwanamke katika mazingira yafuatayo; imeelezwa kwa vifungu (a) mpaka(d) mambo kadhaa lakini kifungu (e) kinasema kwa ridhaa ya mwanamke ambapo msichana au mwanamke huyo ana umri chini ya miaka kumi na nane, isipokuwa tu kama msichana huyo ana umri wa miaka kumi na tano kwenda juu na wameoana kihalali na hawajaachana sheria hizi mbili zinaonesha wazi binti wa miaka 14 na kuendelea ana utambuzi wa ndoa ni kitu gani kwa maana hiyo tu ile dhana ya kurubuniwa inafifia yenyewe. Hata hivyo kumekuwa na mambo yafuatayo yanayohitaji tafakari;
Usingiziaji, watoto wa kike wamejua wazi kwamba akishaongea tu yeye ataachwa huru hivyo anaropoka tu bila kujali athari za matokeo ya uongo wake lakini nay eye akijua ana kibano pia akili zao zitawakaa sawa. (rejea kesi ya Maria Sanga na Tumaini Mfinanga ya mwaka 2017 binti huyoalikiri wazi alimsingizia kijana kwa shinikizo kutoka kwa wazazi hali ya kuwa akijua si kweli, gazeti la mwananchi la tarehe 31-1-2021) na pia (rejea kikao cha katibu mkuu wa wizara ya katiba na sheria Profesa Sifuni Mchome mkoani kigoma aliwakumbusha wananchi kwamba ni kosa la jinai kwa mtu yeyote kumsingizia mtu mwingine tuhuma za ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia kwa madhumuni ya kujipatia fedha, issamichuzi.blogspot.com, alhamisi oktoba 14 2021) .
Kukiri hawakubakwa bali walikubaliana, ni jambo la kushangaza kwamba binti anaondoka kwao wakati mwingine kwa njia za kificho na kuenda geto la kijana na kuingia kwa kificho asionekane na wazazi wa kijana husika halafu mwisho wa siku ionekane alirubuniwa na bado kwenye ushahidi wa mahakamani anathibitisha ya kwamba mtuhumiwa ni boifrendi wake wa muda mrefu na wameshafanya tendo mara kadhaa na mara zote wamekuwa wakisapoti “songi” la maua sama “mwagia ndani” lakini bado binti huyo anaachwa tu bila kufanyiwa kitu kitakacho mfanya ajutie matendo yake.
Wamefundishwa njia za kijikinga na ujauzito, asilimia kubwa wa wahanga wa jambo hili huwa bado wapo mashuleni kwa levo ya sekondari na shule za msingi huko mashuleni elimu ya kijinsia hutolewa kwa mapana kwa lengo la kuwakinga na mimba za mapema kwa vile kati ya vitu vigumu ni kuzuia kwa watoto wasijihusishe na matendo ya ngono kabisa hilo limethibitika wazi haliwezekani kwani viongozi wa dini wamepiga kelele sana na kuendesha semina ambazo kwazo zimegeuka kuwa koneksheni ya vijana kupata mawasiliano na kuanzisha walichotoka kukatazwa imekuwa sawa na kumshauri mbwa juu ya uzazi wa mpango basi elimu hii ya kujikinga itumike kama njia moja wapo ya kuwafanya wao waepuke balaa hilo.
Tafsiri ya haki sawa na usawa wa kijinsia itakuwa imetimia, kumekuwa na kampeni za kutosha kuhusu usawa wa kijinsia na kwamba kwa sasa ni vema kila kitu iwe hamsini kwa hamsini kwa jinsia ya kiume na jinsia ya kike basi jambo hili pia linahitajika kwenda kwa usawa kama ni adhabu itolewe kwa wote na wazazi wao watakuwa na jukumu la kulea hao watoto watapozaliwa mpaka pale adhabu itakapoisha.
Itapunguza mrundikano wa kesi zilizotokana na starehe za vijana wenye akili zao timamu, mahakama zetu zimekuwa bize kupambana na kesi ambazo zimetokana na makubaliano ya vijana wawili wenye akili na utashi wao na kwa kuridhiana kwao kunabadilika kuwa mzigo mkubwa kwa serikali na kutumia pesa nyingi kushughulikia jambo ambalo liltakiwa liishie nyumbani kwa balozi wa nyumba kumi.
Fursa ya kurudi shule kwa watoto wa kike waliopata ujauzito wakiwa shule, mwaka huu 2022 serikali kwa kushirikiana na benki ya dunia pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) limeanzisha elimu maalumu ya mfumo wa elimu ya watu wazima (BBC Swahili 21 juni 2021, wanafunzi waliopata mimba Tanzania kurejea masomoni kupitia vyuo vya maendeleo ya wananchi) lakini taarifa hiyo haijaweka wazi kuhusu wa kiume ikiwa ni wanafuzi wenzao wamerudishwa kupata fursa ya elimu au la, kama tunakubaliana kwamba mtoto wa kike kupata ujauzito ni ajali na anatakiwa ajiulize lakini “dogo” wa kiume umri wake aliyempa huo ujauzito wa atajiuliza mbele ya “nyapara” nyuma ya nondo (jela) .
Taswira ya kesi ya mtoa rushwa na mpokea rushwa kuwa hatiani itumike, kama sheria ingekuwa inamhukumu mpokeaji pekee basi kuchomeana kungekuwa kwa kutosha lakini kitendo cha wote wawili kuwa hatiani ni vigumu mtoaji wa rushwa kujiachia na hivyo kwa namna fulani imesaidia kupunguza unafiki wa mtoaji au mpokeaji ya kwamba alishawishiwa (kurubuniwa) kama ilivyozoeleka katika kesi za ngono kwa vijana.
Mwisho nomba nieleweke vyema hapa sizungumzii wale walibakwa au kujaamiana na watu wazima bali wale walioridhia wenyewe na kufanaya tendo na vijana wenzao wa umri kama wao (15-18), itakuawa ni jambo la kushangaza kusikitisha kama tuna mabinti wa miaka kimi na tano au zaidi lakini hawezi kupambanua nikifanya ngono matokeo yake ni mimba.