Elections 2010 Wanafunzi Vyuo Vikuu epukeni aibu hii

Sio Thobias Mwasiga pekee mwenye fikra mgando kuhusu tukio lile la kihistoria lililofanywa na CHADEMA Bungeni. Wapo wengi wakiwapo viongozi wa hata vyama vya upinzani ambao kwa njaa zao wanasahau kazi yao ya kutetea haki za wananchi na kufanya kazi za kujipendekeza kwa CCM, shame on them.
Jana nimemsikia Kyara akibwabwaja kulaani kutoka kwa wabunge siku ile,wasichokijua ni kuwa kitendo kile hata kama kimemwaibisha huyo Rais,zile ni salaam toka kwa Watanzania wote ambao hawakutendewa haki kwa kuibiwa kitu muhimu katika maisha yao,KURA.
Kwa vile sheria yetu ni kandamizi hivyo NEC wakituchagulia Rais wao hakuna wa kuwapinga, lazima itumike njia ambayo haina fujo kuonyesha kupinga jambo hilo nayo ni ya Waheshimiwa ku toka nje ya Bunge wakati akihutubia huyo aliyewekwa na NEC. Hizo ni salaam za uchungu kwa pande zote.
 
Mimi hawa vijana wa udom nawashangaa sana......nakumbuka eti kina Ridhiwani ndio waliweka mkakati wa kuwateka hao vijana na kuwalaghai kwamba eti kila kijana wa UDOM ni lazima awe mwana CCM...huku wakiwadanganya kwamba bila CCM basi UDOM isingekuwepo ......SHAME ON CCM
 
Back
Top Bottom