Wanafunzi SAUT Mwanza: Watoa ruksa CHADEMA kuongoza nchi

Nicholaus Kilunga

JF-Expert Member
Feb 15, 2014
1,188
567
Wanafunzi wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino tawi kuu la Mwanza wameipa ruhusa CHADEMA ya kuongoza nchi,akizungumza na mwandishi wa habari hii mmoja wa wanafunzi chuoni hapo,Valeliani Baleke ,amesema kwa muda mrefu sana CDM kimeonekana kuwa chama sahihi kwa watanzania,chama ambacho kimejipambanua kama chama kinachotetea na kusimamia maslahi ya wanyonge,akitolea mifano ya namna CDM ilivyoibana serikali kwenye issue za EPA,Buzwagi,Meremeta,Escrow na katiba mpya,"huko kote CDM ilisimama kidete kwa ajiri ya maslahi ya wananchi".

Nae bwana Damas Kimenyi ambaye pia anasomea masuala ya sheria pia akiwa ni katibu wa CDM wilaya ya Ilemela,alisema wao kama wasomi wanaiunga mkono CDM sio kwa sababu ya maslahi,bali ni kwa sababu ndicho chama kinachoweza kuitoa nchi korongoni ilipopelekwa na serikali ya CCM,wanafunzi wengi wa chuo hicho walioongea na mwandishi wa habari hii walionekana kukikubali zaidi chama hicho cha upinzani nchini,huku wengi wakionekana kumtaka katibu mkuu wa chama hicho Dr Willbroad Slaa agombee urais kwa tiketi ya chama hicho baadae aungwe mkono na vyama vinayounda UKAWA,wakisema ndani ya CCM hakuwezi kupatikana kiongozi bora kutokana na chama hicho kukithiri kwa ufisadi na kushondwa kusimamia masuala ya msingi ya nchi hii.

Wanafunzi hao walitoa maoni hayo baada ya mwandishi kuwataka wazungumzie ujio wa viongozi wa kutaifa wa chama hicho chuoni hapo,ambapo leo naibu katibu mkuu Zanzibar Salum Mwalim atatikisa katika viwanja vya shule ya msingi Nyamalango,naibu katibu huyo ataambatana na mwenyekiti wa BAVICHA taifa Patrobas Katambi,mwenyekiti wa BAWACHA taifa Halima Mdee,wabunge Wenje wa Nyamagana,Kiwia wa Ilemela,Machemli na Profesa Jay mwanamziki na mtia nia wa ubunge Mikumi kuanzia majira ya saa 9 mchana katika sherehe ya kuwaaga wahitimu wa chuo hicho ambao pia walikuwa ni wanaCHADEMA(CHASO SAUT)
 
Ahsante sana kwa taarifa Mkuu Nick Kilunga, kama ningekuwa Mwanza ningefika Shuleni Nyamalango
 
Last edited by a moderator:
Mbona mimi ni mwanafunzi wa SAUT mwanza!? Na sijatoa ruksa Chadema kuongoza!?

Badilisheni kichwa cha habari andikeni baadhi ya wanafunzi wa Saut watoa ruksa na sio wote.
 
Hakuna mwanasiasa atakayeikomboa tanzania,,, si CCM,CDM,CUF,ACT nk.... NGUVU YAPAMOJA INAHITAJIKA KUFANYA MAPINDUZI YA KIRAIA...
 
wanafunzi wa udom hawako vizuri kifikra make hakuna msomi nchi hii ambaye anawasaport ccm ambao wanamaliza pesa na lasilimali za nchi ambazo zinge tumika kuwapa mikopo chuoni then wana washabikia its a wonderful and shame on them na sasa hivi wame goma eti hawana mikopo ya kujikim miez mitatu na mafisadi wanayo ya saport yanakula butter duuuh wasomi wa nchii ni shida hongera SAUTI kwa kujitambua
 
Nguvu ya pamoja ukisa nyuma ya keybody ya pc ama simu yako?

Hiyo ni fikra yako halafu inaonekana unachokisema ndiyo ukifanyacho.... nina alama mbili za majeraha ndani ya mwili wangu na nimeshawahi kuwekwa selo mara mbili kwa kupinga uonevu na si kutetea chama,,, nanimefanya hivyo huku nikiwa na kipato kizuri na maisha mazuri tu,,,, unatuaminisha hayo utuambiayo huku ukijua huna dhamira ya dhati ila ni tamaa ya kuwa fulani na njaa ya tumbo tu...
 
Hahaha Baleke nae katoa mawazo? Eti nae anataka jimbo la Shinyanga mjini? kila la heri makamanda

Cha ajabu hapo sasa ni kipi?ama kutoa mawazo kwamba CDM inapaswa kuongoza nchi sasa?na jimboni Shinyanga ndo wataamua na si wewe
 
Hiyo ni fikra yako halafu inaonekana unachokisema ndiyo ukifanyacho.... nina alama mbili za majeraha ndani ya mwili wangu na nimeshawahi kuwekwa selo mara mbili kwa kupinga uonevu na si kutetea chama,,, nanimefanya hivyo huku nikiwa na kipato kizuri na maisha mazuri tu,,,, unatuaminisha hayo utuambiayo huku ukijua huna dhamira ya dhati ila ni tamaa ya kuwa fulani na njaa ya tumbo tu...

Kama uyaandikayo nu kweli,heko kwako na pole,bt kama ni walewale ambao daima wanapenda mambo yanyoke ndani ya nchi hii ,bt ukiwambia watoke front tupambane kuung'oa mfumo wanazingua,wao wapo bize tu nyuma ya keybody
 
Wanafunzi wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino tawi kuu la Mwanza wameipa ruhusa CHADEMA ya kuongoza nchi,akizungumza na mwandishi wa habari hii mmoja wa wanafunzi chuoni hapo,Valeliani Baleke ,amesema kwa muda mrefu sana CDM kimeonekana kuwa chama sahihi kwa watanzania,chama ambacho kimejipambanua kama chama kinachotetea na kusimamia maslahi ya wanyonge,akitolea mifano ya namna CDM ilivyoibana serikali kwenye issue za EPA,Buzwagi,Meremeta,Escrow na katiba mpya,"huko kote CDM ilisimama kidete kwa ajiri ya maslahi ya wananchi".

Nae bwana Damas Kimenyi ambaye pia anasomea masuala ya sheria pia akiwa ni katibu wa CDM wilaya ya Ilemela,alisema wao kama wasomi wanaiunga mkono CDM sio kwa sababu ya maslahi,bali ni kwa sababu ndicho chama kinachoweza kuitoa nchi korongoni ilipopelekwa na serikali ya CCM,wanafunzi wengi wa chuo hicho walioongea na mwandishi wa habari hii walionekana kukikubali zaidi chama hicho cha upinzani nchini,huku wengi wakionekana kumtaka katibu mkuu wa chama hicho Dr Willbroad Slaa agombee urais kwa tiketi ya chama hicho baadae aungwe mkono na vyama vinayounda UKAWA,wakisema ndani ya CCM hakuwezi kupatikana kiongozi bora kutokana na chama hicho kukithiri kwa ufisadi na kushondwa kusimamia masuala ya msingi ya nchi hii.

Wanafunzi hao walitoa maoni hayo baada ya mwandishi kuwataka wazungumzie ujio wa viongozi wa kutaifa wa chama hicho chuoni hapo,ambapo leo naibu katibu mkuu Zanzibar Salum Mwalim atatikisa katika viwanja vya shule ya msingi Nyamalango,naibu katibu huyo ataambatana na mwenyekiti wa BAVICHA taifa Patrobas Katambi,mwenyekiti wa BAWACHA taifa Halima Mdee,wabunge Wenje wa Nyamagana,Kiwia wa Ilemela,Machemli na Profesa Jay mwanamziki na mtia nia wa ubunge Mikumi kuanzia majira ya saa 9 mchana katika sherehe ya kuwaaga wahitimu wa chuo hicho ambao pia walikuwa ni wanaCHADEMA(CHASO SAUT)
Hivi unategemea nini wanafunzi wa chuo cha Kanisa watatoa kauli gani dhidi ya Chadema.
 
sisi wanafunzi wa SAUT tupo kwenye jembeka festival ccm kirumba hao ulowasema hapo labda watawakuta wanafunzi wa nyamalango shule ya msingi sisi tuna kula bata huku tulipewa complementary na seba Ndege!!
 
Wewe bado kweli bado uko na tabia ya kuongwa kanga na wali na kusahau kesho balaa jingine hili.

swissme
 
Back
Top Bottom