ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,017
- 7,220
- Thread starter
- #21
walifunga barabara ili wananchi waelewe na wafahamu kilio chao, na hakuna hata abiria mmoja aliyekasirika na kitendo hicho cha wanafunzi, mimi nawaunga mkono kabisa kabisa, maana bila mgomo hakuna haki nchi hii..
Manyanza,
Unaposema hakuna abiria aliyekasirika unakuwa unakosea heshima uvumilivu na uungw'ana wa watumiaj wa barabara. mimi mwenyewe nilikuwa miongoni mwa watu waliojitahidi kuwazuia vijana watano walioshuka kwenye toyota pickup moja wakitaka kuwa confront wanafunzi hao kabla polisi hawajafika. Watumiaji wa barabara walikasirishwa sana na tumenusirika kuwa na vurugu pale.
Utashi wako wa kisiasa isiwe sababu ya kutetea maovu yote yanayofanywa na unaowashabikia.
Na kufunga barabara ili mtu mwenye safari yake aelewe kilio chao, wao wanajua hao wasafiri wana kilio gani? Je kama kuna mjamzito anawaishwa hospitali? na yeye asikilize kwanza kilio cha mikopo ya wanafunzi kabla ya kujifungua?
Manyanza, kuwa makini na maoni unayotoa. Mtawapoteza vijana hawa. Tuungane kuwaambia kuwa waekosea, ili siku nyingine wawe makini zaidi.