Wanafunzi 400 waliokwepa sekondari kusakwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Khalidi Mandia kwa kushirikiana na viongozi wa wilaya hiyo wameanza kampeni ya kuwasaka wanafunzi zaidi ya 400 waliofaulu kuingia kidato cha kwanza ambao baadhi yao wanadaiwa kuolewa na kushindwa kuripoti shuleni.
Akizungumza katika mkutano na wananchi wa kata ya Lobosoiti, Mandia alisema tayari wameshaanza kampeni katika kukabiliana na tatizo hilo na wanawashirikisha viongozi wa ngazi zote wakiwemo wa mila kuendesha msako wa nyumba hadi nyumba kuwatafuta watoto hao.
Alisema wazazi wote wakatakaobainika kuhusika na utoro huo kwa namna moja ama nyingine watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupelekwa mahakamani.
Akizungumzia suala hilo, Mbunge wa Simanjiro, Christopher Olle Sendeka alisema uchunguzi umeonyesha kuwa pamoja na utoro wa kawaida baadhi ya watoto ambao hawajafika shule ni wale yatima na wanaotoka katika familia zisizo na uwezo.
Alisema tatizo hilo ni kubwa zaidi kwa wazazi ambao waliathiriwa na janga la vifo vya mifugo kwa kiasi kikubwa na kwamba wameshaanza kuchukua hatua za kuwasaidia wananchi hao.
Alitaja baadhi ya hatua zilizoanza kuchukuliwa kuwa ni pamoja na kuunda mfuko wa kuchangia elimu unaowashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa mila na wameshaanza kuendesha kampeni za kuchangisha fedha.
Tatizo la wanafunzi wa jamii za wafugaji kukatishwa masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo ya kuolewa lilishaanza kupungua kutokana na mwamko wa wazazi kupenda elimu ambao umeiwezesha wilaya hiyo kushika nafasi ya kwanza kimkoa kwa kufaulisha wanafunzi.



SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
 
Back
Top Bottom